Sowah, usajili bora Ligi Kuu kwa vilabu vyote 16 kwenye dirisha hili!

Joined
Jun 10, 2017
Posts
8
Reaction score
14
Namba huwa hazidanganyi. Jonathan Sowah ni mshambuliaji wa kati bora. Akiwa katika Ligi ya Ghana mwaka 2023, alicheza mechi 28 na kufunga mabao 16 na kutoa assisti moja (1).

Nchini Ghana alikua akicheza katika klabu ya Medeama. Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika alicheza mechi nane na kufunga mabao matatu (3). Jumla, alicheza mechi 36 na kufunga mabao 19.

Jonathan Sowah, alianza kucheza kama golikipa katika ngazi ya shule, alipofika kwenye ngazi za juu. Alikutana na mwalimu wake, aliyemwambia atakua bora akicheza kama mshambuliaji wa kati.

Huu ni usajili wangu bora kwenye dirisha hili kubwa kuliko sajili zote. Sababu za kuutaja kama usajili bora ni ubora wa Jonathan Sowah, amethibitisha kwenye Ligi zote alizocheza, hajawahi kukabiliwa na ukame wa mabao.

Kabla ya kujiunga na Singida Black Stars msimu uliopita, alikua akicheza Al Nassir ya Libya, alicheza mechi chache na kufunga mabao saba (7).

Baada ya kutua Singida, alicheza mechi 15 za Ligi na kufunga mabao 15. Katika mechi 13 za Ligi Kuu alifunga mabao 13 na katika mechi mbili (2) za Kombe la TFF, alifunga mabao mawili (2).

Sababu ya pili inayonifanya niuchague kuwa usajili bora katika dirisha hili ni, kuwa usajili uliozingatia mahitaji ya timu. Mahitaji ya Simba msimu uliopita katika eneo la ushambuliaji yalikua ni kupata mshambuliaji wa kati hatari.

Kwa wastani wa kufunga bao moja katika kila mchezo, Jonathan Sowah ni usajili uliokidhi mahitaji ya Simba. Msimu uliopita, Steven Mukwala na Lionel Ateba walifunga mabao 13 kila mmoja kwenye ligi.

Lakini, waliokosa nafasi nyingi, Simba ilipiga jumla ya mashuti 202 yaliyolenga lango na mashuti 187 yasiyolenga lango, katika mshuti hayo, Simba ilifunga mabao 69.

Wastani wa kubadilisha nafasi kuwa mabao kwa Simba msimu uliopita ulikua ni asilimia 18. Washambuliaji wa kati hawakua wakatili mbele ya lango. Simba ilimhitaji Jonathan Sowah.

#ligikuu #simbasc #tanfootball #jonathansowah
 
Attachments

  • 20250906_220339.jpg
    20250906_220339.jpg
    217.1 KB · Views: 57

Mhii labda siyo Tanzania ninayoijua.
1.kagere
2.okwi
3.azii ki.
4. Chama
5.Diara
Hawa ndo waliweza kutendea haki nafasi zao wengine wote wanafail
 
Back
Top Bottom