Soweto Derby: Keizer Chief achezea kichapo, Orlando Pirates watuma salama kwa Simba

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Leo imepigwa moja ya dabi maarufu barani Afrika, nchini Afrika Kusini, inayoitwa Soweto Derby, kwenye uwanja wa FNB Stadium (Soccer City) jijini Johannesburg. Mchezo huo uliwakutanisha Maharamia wa Orlando (Orlando Pirates), wanaojulikana kwa lugha yao kama The Buccaneers, na Machifu wa Kifalme (Kaizer Chiefs), wanaojulikana kama Amakhosi.

Katika mchezo huo, Orlando Pirates wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Kaizer Chiefs. Umiliki wa mpira (ball possession) ulikuwa 52% kwa 48% kwa upande wa Orlando Pirates dhidi ya Kaizer Chiefs. Kaizer Chiefs waliongoza kwa kupiga jumla ya mashuti 14 (total shots), huku mashuti yaliyolenga lango yakiwa 2, ambapo moja lilizaa goli katika dakika ya 30, huku wakimaliza mchezo wakiwa na kadi nyekundu katika dakika ya 91. Kwa upande wao, Orlando Pirates walipiga jumla ya mashuti 12, huku mashuti yaliyolenga lango yakiwa 3 tu, ambapo mawili yali zaa magoli ya ushindi katika dakika ya 24 na 55.

Msimamo wa ligi ya Afrika Kusini kwa siku ya leo umekaa hivi:
Screenshot_20261031_185307_FotMob.jpg

Hii ni kama Salamu kwa mnyama simba, ambapo hizi timu mbili zimewai kumtoa jasho Mnyama. Na sasa watakutana tena Simba na Orlando huku mechi ya kwanza ikianzia Tanzania.
 
View attachment 3702291

Hii ni kama Salamu kwa mnyama simba, ambapo hizi timu mbili zimewai kumtoa jasho Mnyama. Na sasa watakutana tena Simba na Orlando huku mechi ya kwanza ikianzia Tanzania.
Msitutishe
 
Yule kipa wa Orlando kama kafungwa goli like Jana, Taifa atafungwa mengi
 
Kwani simba kumfunga topolo tena na mpira kapigiwa orlando haogopi?
 
Back
Top Bottom