Soya, mbaazi, mahindi, ni mazao yanayotupa umaskini sababu ikiwa ni serikali.

chotera

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2016
Posts
6,560
Reaction score
15,864
Wakuu habari.
Huku nikiwa nalia na mbaazi ndani , bado naangalia soya inavoozea ndani, na bado naangalia mahindi bei ilivo chini ambapo ukiuza gunia mbili ndio unapata mfuko mmoja wa mbolea naomba watu wa serikali mvae viatu vyetu wakulima muone kama mtafurahi, mnaudhi sana muda mwingine, tujengeeni chuki na sisi tutawalipa chuki uvumilivu unamwisho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
pole sana mkuu.
hapo ndipo watu wa serikali wanapaswa kuonyesha maana ya uwepo wao ktk kuwezesha uhakika wa mzunguko wa biashara unaomsaidia mkulima.
 
Serikali inahusika moja kwa moja na haya yanayoendelea wamepiga marufuku hata mbao za miti anayopanda mkulima zisiuzwe nje huku wakiwa hawana soko wala uwezo wa kununua chochote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali inaongozwa na wasomi waliokalili maandishi,elimu hawana kabisa! Ni aibu nchi kushindwa kutafuta soko la bidhaa inayozalisha,sasa sijui hivyo viwanda wanavyosema bidhaa wataziuza wapi kama wameshindwa kutafuta soko la bidhaa za kilimo
 
Wizara zipo na ka mwaka zinatengewa bajeti ila hatuon umuhimu wake,kuna baadhi ya Nchi ukanda huu zina njaa,kungekuwa na uwajibikaji na kujitambua kwa viongoz husika wangeweka utaratibu wa kuwa tunawauzia chakula,hilo nalo limeshindikana,tumebaki kuuziana sisi kwa sis(Soko la ndani),na wakati mwingine Serikali tena Mkopo,tusitegemee jipya kwa kwel,kuna mabwana shamba na mabwana mifugo,hawajibiki vya kutosha,Mkulima anaanda shamba mpaka anavuna bwana shamba hajaonekana kwa ushauri,yaani ni hatar na mabwana mifugo nao ni wale wale

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2020 fanyeni kweli. , hata wakiiba kura hesabu zikatae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…