PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Mratibu wa Polisi Jamii Wilaya ya Ukerewe, Mkoani Mwanza, SP Raphael Ganchira, ametoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Bwilo kuhusu umuhimu wa kutunza amani.
Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika Oktoba 21, 2025, katika kisiwa cha Bwilo, SP Ganchira alisema lengo la elimu hiyo ni kuhamasisha jamii kuthamini na kulinda amani, akisisitiza kuwa pale amani inapopotea, waathirika wakuu ni watoto, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu.
Aidha, aliwataka wananchi kuwa mabalozi wa amani kwa kuwa amani ni msingi wa maendeleo, ustawi na usalama wa jamii nzima.