GE2025 SP Raphael Ganchira: Amani inapopotea, waathirika wakuu ni watoto, wanawake, wazee na Watu wenye ulemavu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Mratibu wa Polisi Jamii Wilaya ya Ukerewe, Mkoani Mwanza, SP Raphael Ganchira, ametoa elimu kwa wananchi wa Kata ya Bwilo kuhusu umuhimu wa kutunza amani.

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika Oktoba 21, 2025, katika kisiwa cha Bwilo, SP Ganchira alisema lengo la elimu hiyo ni kuhamasisha jamii kuthamini na kulinda amani, akisisitiza kuwa pale amani inapopotea, waathirika wakuu ni watoto, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu.

Aidha, aliwataka wananchi kuwa mabalozi wa amani kwa kuwa amani ni msingi wa maendeleo, ustawi na usalama wa jamii nzima.

Your browser is not able to display this video.
 
Wailinde basi hiyo Amani.
Wao wanateka na kuua watu bila kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria, halafu wategemee kuwe na amani.
 
Tutazungumza tukishauvunja vunja vitu
 
Amani ipi?
Unahubiri amani mkononi umeshika panga?
Wao ndo wanaharibu amani ya nchi hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…