Spain ni nchi nzuri kwa kufanya biashara

Ndugu wanaJF,

Nipo Spain kwa muda. Ni nchi nzuri na Kubwa ndani ya Ulaya. Watanzania wengi wanaijua sababu ya mchezo wa mpira, Real Madrid, Barcelona FC na kadhalika. Lakini watanzania wengi pia hawajui ni nchi pia nzuri kwa kufanya biashara kama unajipanga vizuri.

Hapa nakutana na wasenegal wengi, waghana, wacameroon, wacongo waafrika wa magharibi kibao na siyo wote wakimbizi wa uchumi ila ni watafutaji wa biashara. Wote tunajua umaarufu wa vigae (tiles) wa Spain. Pía vyakula vyao kama wine, tapas, chorizo.... Lakini si wengi wanajua pia kwamba unaweza kupata spare parts zilizotumika na used na new machinery, na mambo mengi wabongo tumezoea kutafuta Uingereza Uholanzi au Ujerumani.

Nafasi za biashara zipo kwa wale wanaotaka. Mimi binafsi natafuta huko na huko na nawakaribisha mniulizie chochote kuhusu Spain. Ukitafuta makampuni au bidhaa, ukitafuta kujua zaidi kuhusu import na export toka Spain... naelewa lugha na sheria za hapa. Na kama unakuwa serious kibiashara tutaelewana pia.

Hasta luego
Safi sana. Natafuta mitambo ya ujenzi wa barabara je kati ya Spain na China wapi ni more appropriate kuipata kwa urahisi na bei nzuri?
 
Mbona mnauliza maswali kibao utazan huyo jamaa ni wazir wa nchi hiyo... kama unahitaji maelezo zaid nenda ubalozi wa Spain utauliza maswal yote nakujibiwa
 
Sasa swali umeulizwa wewe mkuu? Kwani ni lazima kucomment? Inaelekea hujui hata majukumu ya ofisi za ubalozi. Nyie ndo wale wale!!
 
Mleta uzi naona unatafuta kula

Nafanya kazi na kampuni moja kubwa sana ya huko Spain mwaka wa tatu sasa kitu ambacho kinasababisha niwe na mashaka na huu uzi.

Spain haina hizo sifa. Kwanza watu wake wengi ni masikini.

Kuna mtu kakuuliza uko mji gani? Tunaomba nini
 
Asante kwa comments zote na samahani nilikuwa na shughuli za wikend Jana. Nipo Alicante kwa anayehitaji Kujua, lakini kwa kweli sioni umuhimu wa Kujua napoishi. Kwa ndugu Chardams nafurahi kama unafanya kazi na kampuni kubwa wa Spain. Naomba pía uchangie mawazo yako positive. Nafikiri kama kwamba ukiendelea kufanya kazi nao ni kwa sababu unapata faida fulani. Na kuhusu umaskini naomba kidogo ugoogle uzito wa nchi hii ndani ya umoja wa ulaya. Na nimetamka wazi kwamba shida Kubwa hapa ni unemployment. Zaidi nafikiri kila mmoja ajaribu kuchangia kwa kujenga kwa faida ya wote.

Mmoja alisema nendeni ubalozi WA Spain hapo Dar. Wazo nzuri sana kwamba yeyote anayetaka kujua zaidi. Mpango WA biashara daima unahitaji utafiti wa kina.

Mwingine kasema nahitaji kula. Nimetafakari sana kwa ushangao kidogo maana nafikiri wanadamu wote wanahitaji kula pia tena kulala. Ila kula na kulala kwa jasho na kazi ya wengine ndiyo dhambi kubwa. Wajanja wapo pote duniani.

Nitajaribu kuwajibia polepole. Sheria za import export ni wazi na ni zile za dunia nzima pamoja na kanuni za Umoja wa Ulaya. Kwa mfano import inahitaji kazi kali kidogo ya kucomply Na specifications za Umoja wa Ulaya katika ubora na packaging na sometimes ni ngumu kidogo kucomply. Nitajaribu kupata specifications za alizeti kwa yule aliyeulizwa wiki hii. Kuhusu mitambo za barabara ukihitaji used lakini na ubora zipo nyingi. Nitaandika kesho vizuri a specific comment kuhusu used mashinery na mitambo. Sanaa hapa hazina soko sana. Baisikeli nk kesho nitawapa jibu kuhusu freight FOB na CIF na mengine mtapata data ya kucompare na nchi nyingine za Bara la Ulaya.

Sina siri hapa. Nikiweza kusaidia nitasaidia Na nikiweza kufanya biashara pia nitafanya lakini makubaliano ya biashara si za kutangaza hadharani. Na kama wapo Wanaopata faida Na thread hii Nitafurahi. Leo pia nitapumzika kwa hiyo pengine sitawajibu leo zaidi. Kesho lakini nitakwepo online. Cheers Na nawatakia Jumapili njema.
 
Ndugu yangu naomba kidogo unirekebishe popote unapoona nimesema uwongo kuhusu sifa za Spain. Tumia hard data. Angalia sijafananisha Spain na Ujerumani au UK Kwa uchumi, pia nimetamka wazi shida ya ajira. Pengine unaona umaskini mimi naona strong social system, miundumbinu ya hali ya juu, kilimo bora na watalii wengi sana. Naona Barcelona na Madrid na miji mikubwa naona viwanda vingi vya kila aina.... nirekebishe unapoona nimekosea lakini. Yesu mwenyewe alisema maskini watakwepo kati yetu daima. Spain imepata shida sana na ajira tango 2008 mpaka Sasa (ilikuwa 25% saizi 17% bado shida).
Asante na Jumapili njema.
Je unaongea Español?
Mleta uzi naona unatafuta kula

Nafanya kazi na kampuni moja kubwa sana ya huko Spain mwaka wa tatu sasa kitu ambacho kinasababisha niwe na mashaka na huu uzi.

Spain haina hizo sifa. Kwanza watu wake wengi ni masikini.

Kuna mtu kakuuliza uko mji gani? Tunaomba nini
Ndugu
 
Ndugu wanaJF,

Nipo Spain kwa muda. Ni nchi nzuri na Kubwa ndani ya Ulaya. Watanzania wengi wanaijua sababu ya mchezo wa mpira, Real Madrid, Barcelona FC na kadhalika. Lakini watanzania wengi pia hawajui ni nchi pia nzuri kwa kufanya biashara kama unajipanga vizuri.

Hapa nakutana na wasenegal wengi, waghana, wacameroon, wacongo waafrika wa magharibi kibao na siyo wote wakimbizi wa uchumi ila ni watafutaji wa biashara. Wote tunajua umaarufu wa vigae (tiles) wa Spain. Pía vyakula vyao kama wine, tapas, chorizo.... Lakini si wengi wanajua pia kwamba unaweza kupata spare parts zilizotumika na used na new machinery, na mambo mengi wabongo tumezoea kutafuta Uingereza Uholanzi au Ujerumani.

Nafasi za biashara zipo kwa wale wanaotaka. Mimi binafsi natafuta huko na huko na nawakaribisha mniulizie chochote kuhusu Spain. Ukitafuta makampuni au bidhaa, ukitafuta kujua zaidi kuhusu import na export toka Spain... naelewa lugha na sheria za hapa. Na kama unakuwa serious kibiashara tutaelewana pia.

Hasta luego
Gracias......
 
Mkuu uki ingia bar tafandhali usipate shida ya kuagiza gambe wewe Sema hivi UNA CERVEZA POR FAVOR huku una tabasamu.
 
Samahani kwa kutokujibu mapema nilikuwa busy sana wiki hii nimesafiri ndani ya nchi.

Bwana Kakande kuhusu baskeli mpaka sasa sijapata jibu naona bei ni kubwa kidogo lakini bei za freights toka bandari Valencia mpaka dar es Salaam ni euro 1715 na around 445 ya logistics na bandari Valencia kwa futi ishirini. Hapo pia inabidi uweke usafiri ya bidhaa kutoka sehemu husika mpaka bandari na gharama ya Certificate of Conformity kwa ajili ya TBS inatlewa na Buerau Veritas au SGS.

Nyota79 Mitambo wa ujenzi used na mpya zipo nyingi sana.
Umemetango, mitambo wa kuanzisha viwanda vidogo zipo pia.
Sajitoo bado naongea na watu wa alizeti nitakuambia.

Kwa ujumla ni afadhali kama mtu anaridhika aje afanye utafiti. Atafute ofa ya flight cheap na baadaye badala ya gharama ya kutumia hotel kubwa atumie airbnb za bei nafuu au hostels. Chakula ni bei poa sana, na usafiri kwa basi ndani ya nchi ni nzuri pia. Tuseme wiki tatu Spain inaweza kugharimu kama milioni tano inategema unafanya nini, pamoja na gharama ya visa na ya ndege. Mimi binafsi nikiwa na muda naweza kumsaidia mtu yeyote (Akiwa anagharimu lakini matumizi yangu nikiwa naye) mwenye nia njema.

Ukitafuta bei ya chini sana lakini afadhali China, ukitafuta ubora Ulaya ni sawa. Mambo yote ni kupanga, na kujipanga bila haraka ili kuhakikisha biashara inafaa. Binafsi navutia sana biashara ya spares za malorri, naona inafaa sana, lakini bado sijapata muda ya kuanza kushughulika.
 
Vip kuhusu ubaguz wana stor za ubaguz vip haithiri shughul za utaftaji? ?
 
Hapana. Hakuna wakimbizi sana na ubaguzi si shida sana. Polisi anaweza kukuomba PAPELES (passport na visa) mara kwa mara liking ukiwa na visa hakuna shida. Pía biashará wamezoea waafrika. Wajinga lakini wapo pote duniani na lazima kwa tayari kupambana nao lakini kibiashara si shida.
 
Ndugu wanaJF,

Nipo Spain kwa muda. Ni nchi nzuri na Kubwa ndani ya Ulaya. Watanzania wengi wanaijua sababu ya mchezo wa mpira, Real Madrid, Barcelona FC na kadhalika. Lakini watanzania wengi pia hawajui ni nchi pia nzuri kwa kufanya biashara kama unajipanga vizuri.

Hapa nakutana na wasenegal wengi, waghana, wacameroon, wacongo waafrika wa magharibi kibao na siyo wote wakimbizi wa uchumi ila ni watafutaji wa biashara. Wote tunajua umaarufu wa vigae (tiles) wa Spain. Pía vyakula vyao kama wine, tapas, chorizo.... Lakini si wengi wanajua pia kwamba unaweza kupata spare parts zilizotumika na used na new machinery, na mambo mengi wabongo tumezoea kutafuta Uingereza Uholanzi au Ujerumani.

Nafasi za biashara zipo kwa wale wanaotaka. Mimi binafsi natafuta huko na huko na nawakaribisha mniulizie chochote kuhusu Spain. Ukitafuta makampuni au bidhaa, ukitafuta kujua zaidi kuhusu import na export toka Spain... naelewa lugha na sheria za hapa. Na kama unakuwa serious kibiashara tutaelewana pia.

Hasta luego
De nada
 
Back
Top Bottom