Spare parts za Honda Crossroad

dist111

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2012
Posts
3,758
Reaction score
3,199
Salama wana GT

Kuna jamaa anataka kununua family car, na baada ya search ya muda mreefu amepata Honda Crossroad ila hana uhakika na upatikanaji wa spare parts, so anaomba ushauri kwenye spare parts za hiyo gari.
 
Spare Parts za Honda??????.

Hizo Alama za kuuliza umeweka kama urembo au huwa unatumia kwenye kila sentensi?
 
My favourite but not dream car (dream ingine)!! Hii gari ni mfululizo wa Land rover Discovery, Honda aliruhusiwa kuzalisha Discovery ila mkataba ukasitishwa then Honda alichofanya ni kudesign gari yake kupitia sifa za Discovery.

Huo ndiyo ukawa uzao wa Honda Crossroad ambayo ni 7seater SUV yenye CC chini ya 2000.

Kuhusu spare, dunia imekuwa kijiji sasa. Unaagiza baada ya wiki ushaipata na pia mawakala wanaoweza kukuagizia ni wengi tuu (huo ni mtizamo wangu).

Kuna zile zimefanyiwa body kit ndiyo ninavizia hiwa natembelea mara kwa mara, kuna moja niliiona Be forward body kit yake nzuri ila mileage ilisoma saaana nikasita kuagiza.

Ngoja tuone
 

Yaah, kwa kweli gari inavutia, hizo CC na namba of seats zinavutia saana kwa family car, hasa waswahili wenye familia mzigo.
 
Spare part za Honda sio tatizo, kama upo Dar/ Tanzania kuna jamaa ni dealers wa spare za Honda ni ZIZOU spare parts wapo mkabala na machinga complex.
 
nimepata kuambiwa kuwa bei zake zimechangamka kidogo...ila ukifunga ni mkataba.
 
nimepata kuambiwa kuwa bei zake zimechangamka kidogo...ila ukifunga ni mkataba.
Ni kweli, kwa sababu spea zake nyingi ni mpya, huwezi kupata spea zilizotumika kirahisi labda itokee gari ilipata ajali wakaichinja/kuikata ndio unapata, ndio maana ukiweka spea ni mkataba
 
Mimi ni mtumiaji wa Honda, (Honda Fit) kabla ya hapo nilikua na IST. Tofauti niliyo iona kati ya hizi gari mbili.
Honda iko stable sana bara barani (ukiwa speed 140Km/h na kuendelea haikuhamishi barabarani) ila jaribu kwa IST alafu upishane na roli, utajuta.
Ulani wa mafuta almost zinafanana.
Spare za honda ni expensive ila ni original, spare za IST nyingi ni za kichina.

Honda unaweza funga balljoint, bush, brake pad, zika kaa mwaka mzima, ila IST atleast kila miezi mitatu unabadirisha kwa hizi bara bara zetu.

Mimi nadhani kinachowashtua watu ni bei za haya magari kuwa ndogo hivyo watu wanahisi sio imara. Wanasahau demand and supply power.

IST nilinunua 11 million, Honda nimenunua 7million. Na zote zimetoka Japan, millage iko chini ya 50k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari Mkuu nipe mawili matatu kuhusu Honda Step wagon Spada. Ina ushuru kidogo kuliko Noah. Niko Shinyanga kwa Mwanza upo uwezekano wa kuwa na spears za Honda?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mkuu vp ulifanikiwa kununua hii gari?
 
Mkuu vp ulifanikiwa kununua hii gari?
Hapana Mkuu, nilibadilisha wazo njiani! Mie kazi zangu nyingi za porini na milimani, nikahisi nitaichosha mapema!

Kuna zimwi nililichukua linaninyonya damu balaa ila na enjoy nalo sana safari ndefu na pori!!
 
Hapana Mkuu, nilibadilisha wazo njiani! Mie kazi zangu nyingi za porini na milimani, nikahisi nitaichosha mapema!

Kuna zimwi nililichukua linaninyonya damu balaa ila na enjoy nalo sana safari ndefu na pori!!
Ulinunua gari gani Boss
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…