The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,942
- 20,077
Hii ni mojawapo ya kauli ama ushauri wa kipumbavu sana hua unatolewa humu JF magari kwa mtu anaetaka kununua gari.
Mtu anamshauri mtu anunue gari halafu spear atakua anaagiza online ama Dubai.
Watu wengi wanaokuja humu kuomba ushauri wa kununua gari mara nyingi hua ndio gari yao ya kwanza, hivyo hana uzoefu wa gari yoyote, ndio anataka aanze kuonja ladha ya gari halafu anaambiwa nunua gari yoyote, akiuliza spear anaambiwa ataagiza online baada ya wiki 2 ama 3 zimefika.
Ushauri wa kununua gari ambayo spear zake utaagiza online unapaswa kutolewa kwa watu ama pre conditions za kua na gari ambayo spear zake huwezi kuzipata kwa urahisi katika mazingira yako hadi uagize online, kwanza, hiyo gari isiwe primary car yako, kwa maana kwamba isiwe ndio gari pekee unayotumia kwenye shughuli zako za msingi, kwamba ikiharibika, wakati unasubiria spear kutoka Dubai shughuli zako hazikwami. Kwa msingi huo ni lazima uwe na gari zaidi ya moja, unaendelea na mishe zako kama kawaida huku ukisubiri spear kutoka online ama popote ulipoagiza.
Kumiliki gari ambayo ikipata mushkeli, unarudi kwenye daladala huku ukisubiria spear itoke Dubai ama China kwa wiki 2 ama 3 hizo sio akili, ni matope.
Kwenye gari, nunua gari ambayo ni convenient kwako, kwa maana haikupi usumbufu wala kukupoteza muda mwingi kwenye kuirudisha katika hali yake ya awali baada ya kua imepata mushkeli.