Hatari...
Moja..tv na server ya shule villiibiwa usiku,mimi ndo nilikua na funguo za tv room (wezi walitumia master key)..nilifukuzwa ila nikaandika barua ya kukataa kufukuzwa ikakubalika.
Mbili..likizo ya mwezi wa sita,nilivuta nikarudi mwezi wa kumi...hahaha,head master alikosa adhabu ya kunipa ikabidi inipe barua ya kurudi nyumbani nikae bila kikomo,nikaandika barua ya kuomba kabadilishiwa adhabu,nikapewa adhabu ya kufyatua tofali elfu 2000 na kuzichoma,du!..nikafanya hiyo adhabu,ila nilifanya nusu kisha nikapewa msamaha sababu kulikua na mashindano ya debate interscchol na mimi ndo nilikua puff leader wa debate shule nzima.
Tatu...nilishitakiwa kwa kosa na kujihusisha na mapenzi na headgirl,nikaitwa office ya nidhamu nikahojiwa masaa matatu,baadaye nikaitwa staff nikahojiwa masaa mawili,baadaye ikagongwa kengere ya zarula tukaitwa mbele mimi na headgirl,wanafunzi wakaulizwa,je hawa ni pair au siyo pair,wote wakacheka...bahati nzuri akaitwa kiranja wa taaluma akaulizwa aseme ukweli mbele ya wanafunzi..akasema hawa ni wapenzi ila hawafanyi ngono,mapenzi yao ni ya kimasomo na kirafiki tu..
Walimu wakachekaaa...basi headmaster akasema tuendelee hivohivo ila tunachunguzwa.
Nne...saa nane usiku sipo bwenini...nimeenda kwenye show ya mr blue,nilipewa suspension miezi mitatu..ila nikaomba nipunguziwe adhabu kwasababu mock ilikua karibu...ombi langu likasikilizwa,nikapewa adhabu ya kusafisha dinning hall miezi mitatu.
Nitaendelea siku nyingine