Special kwa waliowahi kufukuzwa au kunusurika kufukuzwa shule

Special kwa waliowahi kufukuzwa au kunusurika kufukuzwa shule

Alonso14

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2017
Posts
1,785
Reaction score
1,817
Baada ya kukaa na kumbuka maisha ya Shule na ugumu wake naomba kila mwana JF aje aseme njia alivyofukuzwa au alivyonusulika kufukuzwa Shule

Mimi binafsi nikikumbwa na msala kwa kusingiziwa kuvunja office ya decline master na kuiba simu na vitabu tulikuwa kma 8 iv kwenye huu msala aisee hili suala kuisha nadi ilibidi niende kwa mchungaji kuombwewa na msala ukiaisha juu juu japo tulikuwa tunakaribia kufukuzwa hii ilikuwa A level Shule flan iv hapo wanapoishi wanaume wa Dar
 
Hatari...
Moja..tv na server ya shule villiibiwa usiku,mimi ndo nilikua na funguo za tv room (wezi walitumia master key)..nilifukuzwa ila nikaandika barua ya kukataa kufukuzwa ikakubalika.

Mbili..likizo ya mwezi wa sita,nilivuta nikarudi mwezi wa kumi...hahaha,head master alikosa adhabu ya kunipa ikabidi inipe barua ya kurudi nyumbani nikae bila kikomo,nikaandika barua ya kuomba kabadilishiwa adhabu,nikapewa adhabu ya kufyatua tofali elfu 2000 na kuzichoma,du!..nikafanya hiyo adhabu,ila nilifanya nusu kisha nikapewa msamaha sababu kulikua na mashindano ya debate interscchol na mimi ndo nilikua puff leader wa debate shule nzima.

Tatu...nilishitakiwa kwa kosa na kujihusisha na mapenzi na headgirl,nikaitwa office ya nidhamu nikahojiwa masaa matatu,baadaye nikaitwa staff nikahojiwa masaa mawili,baadaye ikagongwa kengere ya zarula tukaitwa mbele mimi na headgirl,wanafunzi wakaulizwa,je hawa ni pair au siyo pair,wote wakacheka...bahati nzuri akaitwa kiranja wa taaluma akaulizwa aseme ukweli mbele ya wanafunzi..akasema hawa ni wapenzi ila hawafanyi ngono,mapenzi yao ni ya kimasomo na kirafiki tu..
Walimu wakachekaaa...basi headmaster akasema tuendelee hivohivo ila tunachunguzwa.

Nne...saa nane usiku sipo bwenini...nimeenda kwenye show ya mr blue,nilipewa suspension miezi mitatu..ila nikaomba nipunguziwe adhabu kwasababu mock ilikua karibu...ombi langu likasikilizwa,nikapewa adhabu ya kusafisha dinning hall miezi mitatu.

Nitaendelea siku nyingine
 
1- Tukiwa 4M4 tuligoma kunywa uji usiokuwa na sukari ksb walimu wa msosi walikuwa wanatuibia kwa kushirikiana na kiranja wa msosi tukazuia watu wote wasinywe tukaa kwa distance kidogo tukiangalia nani ataenda kunywa uji madogo wa form one wakaenda kunywa tukakusanya form one wote tukachukua uji kidogo tukaongezea maji form one km 40 na zaidi na wengine tukawakusanya mabweni yote na fimbo juu wakawa wanapokezana kunywa uji uliochanganywa na maji kidogo ukipungua tunaongezea maji hivyo hivyo na viboko juu mnisamehe sana madogo sasa hv nimekuwa ilikuwa jpili siku hiyo. ..jtatu vichwa 10 tukafukuzwa kwa muda wa siku 21 nakuleta wazazi nakumbuka sikwenda home baada suspension nikamleta mama yangu mdogo mke wa baba mdogo ambaye kiumri hakuweza kunizaa nikasingizia alinizaa akiwa bado shule[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] tulivyorudi mock kufanyika ilikuwa imebakia km wiki moja nikapiga division one ya pt-17 hapo ndo kiburi kikazidi.....adhabu nilipewa kufukia barabara iliyoharibiwa na maji ya mvua kufukia kifusi ksb nilikuwa monitor mkondo A wangu wote usiku wakachukua ndoo kufukia kifusi huku mm nikikodi mkokoteni kazi ya siku tatu tukaifanya usiku mmoja hadi makamu mkuu wa shule alijisemea mkirudia nikufukuza tu ksb adhabu hazitusaidii[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
2. Mshikaji wangu alizuiwa kwa kusukumwa na mwl wa chakula ilikuwa siku ya wali aisee fujo ilizuka tukawazuia form 5, wote wasile kabla yetu japo ilikuwa zamu yao mwalimu alipomzuia mshikaji kwa kumsukuma jamaa akawaka na mwalimu tulikuwa hatumpendi tukalianzisha jiko likafungwa mshikaji wangu km alipigwa akawa analia aisee wenye miti,kuni kutaka kumpiga mwalimu wakaja kikanuka kweli headmaster hakuwepo asee hadi niliota tumefukuzwa nikawambia washikaji hawakuamini...tukahojiwa walimu& wafanyakazi wakagawanyika wapo waliosema tuko sahihi wengine wakisusa kwamba tusipofukuzwa watamwachia headmaster afundishe peke yake[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]kesho yake suspension miezi 3 hadi kuja kufanya necta ukitokea nje ya shule kuanzia 8-11....tukaenda kupanga ghetto vichwa sita usiku tukaenda tukaiba viti shule tukaenda kupeleka uraiani ghetto na pia tulimwachia mwenye nyuma yule mama abarikiwe maana alitujali sana km watakatifu kumbe wanini.....
Nashukuru mungu nilipata division two nikatusua advance hadi chuo ila my bro & mzee waliwaka sana but wanisamehe kwa yote..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahahahaha.

Ilikuwa 4m 3 kitambo hicho tulipiga mawe walimu wa field.

Ilikuwa hatari sana ilibaki kidogo tufukuzwe shule.
 
Hatari...
Moja..tv na server ya shule villiibiwa usiku,mimi ndo nilikua na funguo za tv room (wezi walitumia master key)..nilifukuzwa ila nikaandika barua ya kukataa kufukuzwa ikakubalika.

Mbili..likizo ya mwezi wa sita,nilivuta nikarudi mwezi wa kumi...hahaha,head master alikosa adhabu ya kunipa ikabidi inipe barua ya kurudi nyumbani nikae bila kikomo,nikaandika barua ya kuomba kabadilishiwa adhabu,nikapewa adhabu ya kufyatua tofali elfu 2000 na kuzichoma,du!..nikafanya hiyo adhabu,ila nilifanya nusu kisha nikapewa msamaha sababu kulikua na mashindano ya debate interscchol na mimi ndo nilikua puff leader wa debate shule nzima.

Tatu...nilishitakiwa kwa kosa na kujihusisha na mapenzi na headgirl,nikaitwa office ya nidhamu nikahojiwa masaa matatu,baadaye nikaitwa staff nikahojiwa masaa mawili,baadaye ikagongwa kengere ya zarula tukaitwa mbele mimi na headgirl,wanafunzi wakaulizwa,je hawa ni pair au siyo pair,wote wakacheka...bahati nzuri akaitwa kiranja wa taaluma akaulizwa aseme ukweli mbele ya wanafunzi..akasema hawa ni wapenzi ila hawafanyi ngono,mapenzi yao ni ya kimasomo na kirafiki tu..
Walimu wakachekaaa...basi headmaster akasema tuendelee hivohivo ila tunachunguzwa.

Nne...saa nane usiku sipo bwenini...nimeenda kwenye show ya mr blue,nilipewa suspension miezi mitatu..ila nikaomba nipunguziwe adhabu kwasababu mock ilikua karibu...ombi langu likasikilizwa,nikapewa adhabu ya kusafisha dinning hall miezi mitatu.

Nitaendelea siku nyingine
Mmmmh wewe mwenzangu yako yamenizidi lol

invest what you are willing to loose
 
Baada ya kukaa na kumbuka maisha ya Shule na ugumu wake naomba kila mwana JF aje aseme njia alivyofukuzwa au alivyonusulika kufukuzwa Shule

Mimi binafsi nikikumbwa na msala kwa kusingiziwa kuvunja office ya decline master na kuiba simu na vitabu tulikuwa kma 8 iv kwenye huu msala aisee hili suala kuisha nadi ilibidi niende kwa mchungaji kuombwewa na msala ukiaisha juu juu japo tulikuwa tunakaribia kufukuzwa hii ilikuwa A level Shule flan iv hapo wanapoishi wanaume wa Dar

= alivyonusurika

Kwa mwandiko huo na ni wa A level?!

Unazidi kunihakikikishia kuwa shule za kusomea ujinga zipo.
 
Back
Top Bottom