JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Katika mashindano hayo yanayofanyika kwenye viwanja vya sekondari ya Tabora Boys, Special Olympics itawakilishwa na wachezaji wa mkoa huo kama ilivyokuwa kwenye mashindano ya mwaka jana ambayo pia yalifanyika mkoani humo.
Mgeni rasmi katika mashindano hayo alikuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ajiyeambatana na mawaziri na watendaji wengine wa taasisi za elimu hapa nchini.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Special Olympics Tanzania, Charles Rays wachezaji hao watashiriki mashindano hayo katika mfumo jumuishi, ambako wanasubiri ratiba ya ushiriki wao katika mashindano hayo.
Rays alisema wachezaji hao watakaoshiriki mashindano hayo ni kutoka katika shule nne za msingi mkoani Tabora ambazo ni Furaha, Mwenge, Town School na Gongoni.
Aidha Rays alitoa wito kwa jamii kujitokeza kwa wingi kushuhudia timu mchanganyiko wa wachezaji wenye ulemavu wa akili na wasio na ulemavu.
Naye Ofisa Elimu taaluma Mkoa wa Tabora, Pastory Mashiku wamefurahishwa na ushiriki wa wachezaji wenye ulemavu wa akili katika mashindano hayo kwani inaondoa unyanyapaa kwa jamii.
Mashiku alisema pamoja na mambo mengine michezo ni furaha, inajenga afya na pia ni ajira.
Mashiku alisema Special Olympics Tanzania kwa kufanikisha uwepo wa timu shiriki katika mashindano hayo wanajitahidi pia kuendesha shughuli mbalimbali yakiwemo mafunzo mbalimbali kwa jamii.
Wachezaji wawakilishi wa Special Olympics Tanzania, wakifanya mazoezi kujiandaa na ushiriki wa mashindano ya UMITASHUMTA, mazoezi hayo yanafanyika shule ya msingi, Town School mkoani Tabora.