Special Thread: AFCON 27, Tanzania, Kenya, Uganda, Maandalizi, fursa na matukio

Nyamesocho

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2023
Posts
487
Reaction score
1,287
Hapa tutaangalia mambo mengi kuhusu maandalizi ya Afcon, viwanja, burudani,fursa za kibiashara, uwekezaji wa mitaji na matukio kuelekea 2027, imebaki miaka 4 na miezi kadhaa.
 
Rasmi Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limepitisha mataifa ya Tanzania, Kenya na Uganda kuandaa michuano ya Afcon 2027

Nchi hizo ziliwasilisha ombi walilobatiza jina la Pamoja Bid na itakuwa mara ya kwanza ukanda wa Afrika Mashariki kuandaa michuano hiyo mikubwa ya soka Afrika

Kamati ya Utendaji CAF imetangaza uamuzi huo nchini Misri leo, pia Morocco imechanguliwa kuandaa Afcon 2025

Kwa kuandaa michuano hiyo maana yake ni kuwa Tanzania, Kenya na Uganda zimejihakikishia tiketi ya kushiriki michuano hiyo na jukumu la Mataifa hayo ni kuhakikisha wanaandaa vyema timu zao ili kuhakikisha kombe la Afcon 2027 linabaki Afrika Mashariki


 
RAIS Samia Suluhu Hassan ameagiza maandalizi ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON) 2027 zitakazoandaliwa kwa pamoja na Tanzania, Uganda na Kenya yafanyike kikamilifu.

Ametoa maagizo hayo wakati akishukuru na kutoa pongezi kwa wote waliohakikisha Tanzania inapata fursa hiyo.

“Nawaagiza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhakikisha tunafanya maandalizi mazuri, ikiwemo kukamilika kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu, viwanja viwili vipya vya kisasa vya michezo Arusha na Dodoma,” amesema Samia.
 
Rais William Ruto amepongeza nchi, Uganda na Tanzania kwa kushinda nafasi ya kuandaa kwa pamoja Kombe la Mataifa ya Afrika 2027.

Ruto alisema kuwa mipango ya kubadilisha Wizara ya Michezo sasa imeanza kutekelezwa.

Alisema nchi hizo zitakusanya kila rasilimali na sekta ili kuleta soka la kimataifa la Afcon.

“Nimetaarifiwa kuwa Kenya pamoja na Uganda na Tanzania wamefanikiwa kuwa wenyeji wa AFCON 2027, naomba niishukuru wizara ya michezo kwamba mipango yote tuliyokuwa nayo ya kubadilisha wizara imeanza kuchukua sura,” alisema.
 


Diamond Platnumz baba wa bongofleva, apewe nafasi ya kutengeneza wimbo maalum wa AFCON 2027.
Ana nguvu ya kututangaza East Africa.

Ana ushawishi mkubwa Africa na duniani.

Ni mbunifu anajua kufanya branding so atatusaidia sana kuuza muziki wetu na culture yetu.

Anapenda sana maendeleo ya michezo na burudani.

AFCON 2027 twende na Diamond Platnumz.

Watanzania tuweke chuki zetu pembeni na roho mbaya ambazo hazitusaidii kupata maendeleo miaka na miaka. Tuungane kumpigania Diamond Platnumz apewe ilo deal na CAF.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Wasafi.
 
Baada ya kutangazwa kuwa washindi Afcon 2027 Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia alimwaga machozi.


 
Viwanja vitakavyotumia Kenya ni

1,Kituo cha Kimataifa cha Moi-Nairobi

2,Kasarani-Nairobi

3,Uwanja wa Nyayo-Nairobi

4,Uwanja wa Kipchoge-Eldoret

Uganga

1,Namboole-Kampala

Tanzania

1,Uwanja wa Benjamin Mkapa-Dar es salaam

2,Uwanja wa Uhuru-Dar es salaam

3,Azam Complex Chamazi-Dar es salaam

4,Uwanja wa CCM Kirumba-Mwanza

5,Uwanja wa Amani Zanzibar-Zanzibar

6,Dodoma-Dodoma

7,Uwanja wa Amani Arusha-Arusha
 
hiyo 2027 mna uhakika atakuwepo??
 
Akiongea na EATV katibu mkuu wa wizara ya utamaduni, michezo na sanaa Greyson Msigwa amesema viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya Afcon 2027 wanaangalia

1,Viwango vya viwanja
2,Hotel kwa ajili ya timu
3,Miundombinu ya barabara
 
Chamazi akiwezi kutumika. Labda wakiboreshe. . Kanuni za caf kundaa michuano ya mataifa kiwanja lazima kiweze kubeba washabiki 20,000 kuendelea
 
Hapa tutaangalia mambo mengi kuhusu maandalizi ya Afcon, viwanja, burudani,fursa za kibiashara, uwekezaji wa mitaji na matukio kuelekea 2027, imebaki miaka 4 na miezi kadhaa.
Nimeshasabukilaibu
 
Watengeneze viwanja waache uhuni
 
Inapendeza na kila la kheri kwa Tanzania...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…