Special thread: Kilimo cha umwagiliaji (Irrigation)

Finally, naona dalili za waTanzania kuanza kubadilika na kuona maana ya maendeleo kwa upana wake. Dunia ya leo, kwa asilimia kubwa sana, hakuna mipaka kwenye vitu vingi sana, hasa uzalishaji wa chakula. Lakini kabla ya watu wengi sana kufikia jinsi ya kuzitafuta hizo soko, tuanzie hapo kwenye uzalishaji. Na hizi juhudi za mtu mmoja mmoja kuanza kufunguka na kuwa na moyo wa ku share information za kufanikiwa kwenye hatua za uzalishaji kupitia mbinu za kisasa kwa bei nafuu, ni mfano wa kuigwa.

Tusisahau kwamba changamoto za zahiri na zilizo jificha haikosekani popote pale! Kwa hiyo, pale inapojitokeza/zinapojitokeza, tusianze kuogopa na kurudi nyuma kwa visingizio za kusema/kufikiria kwamba tulikuwa bora tulipo tokea kwani ni ndani ya uelewa wetu au uwezo wetu (in other words, "comfort zone")

Maendelo hayaji kirahisi rahisi tu. Lazima juhudi, fikra na uthubutu haswa ziwepo kwenye hiyo listi ya kufanya, ili kitu kipya kionekane.

Big up! Tanzania mpya tarajiwa na waTanzania wapya watarajiwa pia.
 
Najiunga na huu mtaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kitu kinachohitajika katika kilimo ni maarifa na mifumo madhubuti (ikiwemo mifumo ya umwagiliaji) ya kilimo! Kwa namna yeyote mwezi wa 11 mpaka wa wa tatu mwakani bei za mazao ya chakula zitakua juu!! huu ndio muda muafaka wa kuanza kuwaza kilimo!!!

Karibu mkuu!
 
Somo zuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inbox ya nini mkuu... bora ukasema wote tukaelewa, come on buddy!
 
SWALI:
Mimi nahitaji design kwa na usimamizi katika kilimo cha pilipili mbuzi katika eneo langu dogo lenye upana wa 30m x 25m...

Inaweza kugharimu kiasi gani kwa miundombinu?
MAJIBU:

Cha kwanza je chanzo chako cha maji ni kipi? kisima au mto? au mfereji? je eneo lako liko mkoa/au sehem gani?

Haya ni makadirio ya vitu utakavyohitaji:

1. Drip lines (drip pipes)

Umesema eneo lako lina upana wa 30m kwa urefu wa 35m!, roughly ni kama nusu eka!

Hapa nimechukulia spacing ya mimea ni mstari kwa mstari iwe mita moja na mmea paka mmea iwe 60cm au 50cm!

Mahitaji ya drip lines yatakua 30*35 = 1050m, so utahitaji drip line yenye urefu wa mita 1050 (approx. 1500 au bunda mbili zenye 1000 mita kila moja)! sasa kwa sababu maduka mengi wanauza bunda moja yenye 1000m net, incase ukipata wanapoweza kukupa mita 1500 au kama ukikosa unaweza chukua bunda 2 kwa usalama zaidi!!

2. Tank moja

Kwa eneo lako utakua na mimea sio chini ya 2100 na kila mmea utahitaji sio chini ya lita moja za maji kwa siku so utahitaji tank lenye ujazo sio chini ya lita 3000 na ukipata kubwa zaidi itakua vyema zaidi!

3. Koki atleast 3pcs

Hii ni mwimu maana ndiyo utakua unafungua na kufungia maji na pia utatumia kama pressure requlator, usinunue zile za bombani, nunua zile ambazo ziko wazi pande zote! uwe makini maana hapa size zake zitategemea size za main (inayochukua maji kutoka kwenye tank) na submain pipe inayopeleka maji kwenye drip shambani!

4 .Filter (tumia disc filter)(size ya hii itategemea size ya main pipe yako ambayo itatoka kutoka kwenye tank mpaka kwenye submain, ila by any chance itahitajika 3/4inch au 1 inch). Kuna capacity ya filter hii ni ya mwimu sana ukazingatia! nyingi zinaanzia 100mesh mpaka 200mesh au zaidi!! inategemea na usafi wa maji yako, ila ukipata 150mesh au 200mesh ila ukipata kubwa zaifi ya hapo itakua vizuri zaidi.

NB: Kama maji yako ni machafu unaweza ukahitaji sand filter na disc filter kwa pamoja au DISC FILTER YENYE UWEZO MKUBWA ZAIDI!

5. Main pipe. hii itatoa maji kutoka kwenye tank mpaka kwenye submain yako. unaweza chuku 3/4inch au 1inch. NB chukua nyeusi maana kuna part utaifukia ardhini!
6. Sub mains. hizi zipo special za drip, ila kama ukikosa unaweza chukua hata PVC nyeusi si mbaya. NB: kama ukichukua main pipe ya 1inch basi hii iwe 3/4 inch (three quoter ich)! kama utachukua main ya 3 quota submain iwe ndogo yake ili kumaintain pressure. Kama ukikosa kabisa unaweza chukua zinazofanana haitakua mbaya sana! last time nilinunua zilikua zinachezea 90k mpaka 110k kwa bunda moja la 100mita.

7. T-Joint na Elbow joint! hizi sintaweza sema utahitaji ngapi maana itategemea na configuration ya system yako, again bei zake ni kuanzia 3000 mpaka 5000 maeneo mengi hapa bongo!

6.Driller au puncher/punch. hii utahitaji moja tu, ukiwa na submain za drip utahitaji puch ambayo raisi ila ukitumia PVC ngumu utahitaji driller ambayo kidogo ni ghali, all in all ukifika dukani watakupa mwangaza zaidi!

7.Manati. haya yatatumika kuzuia leakeges inacase zikiwepo!

8.Pipe taper (nimesahau jina kamili). ila ni nyeupe na laini zinatumia kwenye joints za pipe kama ukiunga ili kuepuka leakage!

9. End-cap na Connectors: makadirio zisiwe chini ya 30 maana zote zitategemea configuration ya shamba lako!

NB: Kwa sababu hautumii pump kupeleka maji shambani moja kwa moja, then sizani kama utahitaji complicated pressure regulators, back flow preventers and all those stuffs...

Haya ni makadirio na tutapata actual approximations kama tungefika site na kuona shamba!!
 
Mleta uzi huu ubarikiwe sana, wachangiaji mbarikiwe sana,
Nimeelewa vitu vingi kwenye huu uzi,
Yote ni yote SHUKRANI ZA KIPEKEE KABISA ZIMFIKIE @ cumins
Mkuu unaroho ya kitajiri! Unaroho ya kusaidia, unaroho ya kupenda mwende na wenzako sio kwenda peke yako!
Maana nimesoma humu watu wametoa contact za China unapiga unakutana na Mtu kati nae aweke cha juu,,
Ila @ cumins hajataka mizunguko amemwaga mchele uwanjani mwenye kuhitaji anajichotea tu.hakuna cha mtu kati wala wa pembeni.
BARIKIWA SANA,
Kweli maendeleo tutayaleta wenyewe tukishirikiana.
 
Mimi nahitaji mwongozo/hatua za ujenzi wa gh,vipimo na kiasi cha material na pa kuyapata nataka nijenge mwenyewe niko katavi
 
Naomba namba ya simu.
 
ekari moja ukitaka kumwagilia kwa drip irrigation unaweza kutumia tank au lazima utumie pump moja kwa moja ili maji yafike mpaka mwisho naomba jibu lako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…