Special thread: Kilimo cha umwagiliaji (Irrigation)

ekari moja ukitaka kumwagilia kwa drip irrigation unaweza kutumia tank au lazima utumie pump moja kwa moja ili maji yafike mpaka mwisho naomba jibu lako
Kwanza kutumia pump sio lazima. Sasa naomba tuangalie hizi kesi!

Kwa kutumia pump, faida na changamoto zake...

Kwanza utaweza kufikisha maji shambani kwa urahisi pili hauta ingia gharama za tank incase ukiamua kutumia pump moja kwa moja! (japo unaweza nunua tank incase ukihitaji kuhifadhi maji ili utumie wakati maji yamekatika)

Changamoto kubwa ya pump ni katika gharama yaani lazima ununue mafuta au utumie umeme, pia lazima uwe na pressure regulators ambazo zitahitaji pesa kiasi fulani!

Kwa kutumia tank

Hapa utachohitaji ni tank moja lenye ujazo wa kutosha pia utahitaji pump hata ndogo ya kupeleka maji kwenye tank lako!

Uzuri wa tank ni kwamba japo utahitaji kutumia gharama za kulinunua ila ni rahisi kutumia! na unaweza ukawa na maji kwenye tank hasa wakati maji yamekatika!

Kwa hiyo kama eneo lako ni dogo unaweza tumia tank, pia itafaa zaidi kama eneo lako liko tambarare au liko level maana tank linahitaji gravitation force ili maji yaweze ku flow na kumaintain uniformity!!

USHAURI

Unaweza ukaanza na tank na itapendeza kama ukipata la kubwa itakua vizuri zaidi!! na hata kama usipokua na uwezo wa kununua tank kubwa unaweza ukagawa shamba lako sehemu nne au mbili then ukawa unazimwagilia kwa awamu kulingana na ukubwa wa tank lako!!
 
asante sana mkuu,sasa elevation ya tank kama unataka umwagilie eka 1 kwa drip system si itabidi tank liwe juu ili distribution iwe even
 
Dogo hongera kwa kutumia elimu vizuri
 
Mrejesho wa spacing katika Tikiti wenye ufanisi UPI.!
Mimi nataka kutumia 0.6*0.6*3.5m double row umwagiliaji wa mfereji itafaa.?
 

Kwa spacing ya 0.6*0.6*3.5-4 double row kwa umwagiliaji wa mfereji itafaa kwa MKURANGA.?
 
Mungu angekuwa mbinafsi kama sie angetengeneza drip raining system...purposely kwa mimea tuu iliyopandwa
Hakika ingekuwa faida sana kwa mabepari na dunia ingekuwa sehemu ya kutisha sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…