Okey nimejaribu kuja na majibu haya!
Assumptions i made!
- weather data nimetumia za DSM airport. Zaeneo lako sikuweza pata intime so nimetumia za DSM Airport kama refenrence yetu as ni eneo ambalo liko karibu na wilaya yako na zinaendana katika tabia ya hali ya hewa!
- Disharge au rate ya kutoa maji ya tundu moja la dripline yako (Emitter) nimechukulia kama lita moja kwa lisaa (1.0 L/h).
- Farm area nimechukulia kama eka moja na hamna mvua inayonyesha siku chache kabla au ya kumwagilia.
- Emitter/tundu moja mpaka nyingine ni umbali wa 60cm au 0.6m.
- Crop: tikiti maji/ water melon.
- Spacing kati ya mmea na na mmea ni 60cm, drip line na dripline 2m! (2mx0.6m).
- Soil type: Sandy soil/kichanga.
- Kwakuwa ukubwa shamba ni eka moja then litakuwa na 70mx70m. So ndani ya eka moja utahitaji:
- 35m drip line each with 70 meter
- Jumla utahitaji approx. 2500m (35x70m = 2450m)za drip line (based on my assumption that you have an acre of a field with 70mx70m).
- Number ya plant katika mstari wenye nafasi ya 60cm tundu hadi tundu ni (70/0.6 = 116.6666 crops) 116 plants approx.
- jumla ya mazao ndani ya eka moja ni 116x35 = 4060 plants kama kila shimo utaweka mmea mmoja!
Data kutokana na hali ya hewa.
Crop coefficient at initial stage (Kc) = 0.4
Reference evapotranspiration (ETo) = 4.5mm per day
water requirement (ETc) = ETo*Kc
Water requrement (ETc) = 2mm per day au 0.006mita per day. So utahitaji 2.0 mm za maji kila siku kwa ajili ya mmea wako katika stage ya kwanza ya ukuaji.
So net irrigation water requirement per plant ni ETc * cross spacing ya mmea ambayo itakua 0.002m/day*2m*0.6m sawa na makadirio ya lita mbili kwa siku kwa mmea!!
Generally I can say utahitaji kuanzia lita moja na nusu mpaka lita mbili au mbili na nusu siku. Ukitaka kuapata ujazo kamili au total volume of water kwa eka nzima itakua ni 2lita per plant per day ukizidisha na idadi ya mimea ambapo itachezea kuanzia lita za ujazo 6000 mpaka 8000! Na haya ni makadirio ya stage ya kwanza ya ukuaji wa mmea/Tikiti maji ambayo yatarage kuanzia siku 20 mpaka siku 30 za mwanzo za ukuaji wa mmea! NB: makadirio haya yatabadilika kulingana na ukuaji wa mmea, yaani middle stage ambapo mahitaji ya maji yataongezeka!!
Hapa unaongelea mfumo unaoitwa fertigation katika drip irrigation. kwa mfumo wako utahitaji tank ambapo mbolea ya chumvi chumvi utaichanganya katika tank lako likiwa maji!! sasa hapa nikupe tahadhari, kuna kiwango cha mbolea unatakiwa uweke kwenye kila lita za maji na ukiidisha unaweza usipate matokeo mazuri.
Anyways siwezi ongelea sana mbolea maana mimi sio agronomist kwa elimu zaidi juu ya mbolea kuna uzi uko kwenye stick hapo juu wa
kilimomaarifa.tajiri ameelezea vizuri naimani ataweza pia kukuelekeza ni kiwango gani cha mbolea utahitaji kuchanganya na maji kiasi gani!
No hautamwagilia siku nzima! hapa itategemea na irrigation frequency au interval yako umeiset ya muda gani. hii inahitaji somo lake, nadhani nitaikava kwa undani nikipata wasaa mwingine!!
Karibu.