Kwa tikiti mkoa wa pwani unaweza kulima.Tikiti linapenda Sandy soil,au Sandy clay( kichanga,au Kichanga mfinyanzi, usiwe mfinyanzi tupu, kwa spacing ya tikiti,tumia mita 1 kutoka shimo hadi shimo ndani ya mstari,na mita 3 kutoka mstari hadi mstari. Mbegu nazopendekeza kutumika ni Sukari F1, Zebra f1 ( Balton Tanzania), Kito F1 ( toka Seedco), na Juliana F1 toka Kiboseed .Kiasi cha Mbegu kwa aina ya Sukari F1 tumia gram 150 kwa eka 1 unapanda mbegu 1 kwa shina, kwa kito F1 tumia gram 500 unapanda mbegu 2 kwa shina. ,mbegu zingine gram 300-500 zinatosha kwa eka 1.