Special thread: Kwa waliosoma shule moja na viongozi mbali mbali tukutane hapa kujua vituko vyao shuleni

Special thread: Kwa waliosoma shule moja na viongozi mbali mbali tukutane hapa kujua vituko vyao shuleni

Me mimesoma na John,nakumbuka alikua mchoyo sana darasani

Siku moja bhana ilikua mtihani wa mid term nimekaa nyuma yake nikaomba anisaidie swali la 3(nafikiri atakumbuka hili tukio)akasema hajajaza kumbe kamaliza maswali yote,sasa cha ajabu siku majibu yanarudi ana 0% kumbe alikariri paper lililopita akidhani yatakuja vile vile
.
.
Ni mchoyo tangu shule hataki mwingine afanikiwe ilihal mwenyewe anaharibu
😀 😀 😀 😀 😀 😀
 
Dah kumbe kufoji mmeanza kitambo Lumumba. Anyway mi nilisoma na kingunge, alikuwa anakuja na ngozi ya mkia wa mbuzi siku ya mtihani ili kupigia mstari kwenye mtihani mana alikuwa ameinyoosha ngozi ile na kuikausha kama rula,
😀 😀 😀 😀 😀 😀
 
Deo Filikunjombe(RIP) John Nchimbi,Kichele(tra) wapo kama walivyo sasa ila more advanced.
Pia nimesoma na majambazi napaswa kuwataja maana nao ni viongozi katika himaya zao?japo wengi marehemu sasa na marehemu hatajwi kwa mabaya
 
Nkmesoma na Makonda anapenda.

Ni mzuri kwa somo la kiswahili na kingereza tatizo anapendaa uongozi. Mambo ya security w shule anayapenda sana na anapenda kuheshimiwa KUZID hata headmaster
Kumbe
 
Nimesoma na kufanya kazi kwa muda mfupi na Ndugai.
nilimshauri auze gari lake ili awekeze katika siasa maana alipekuwa akipenda sana siasa.
Twambie tabia yake nzuri ambayo uliipenda akiwa shule, na madhaifu yake , usimuonee wala kumpendelea
 
Habari za wana jf naona ni vema

Tukiwa wanafunzi tuliamini kwamba labda kijana Fulani kutokana na usmartness wake atakuwa kiongozi Fulani wizarani, au anaweza kuwa kiongozi mkubwa baadae,

Kwa upande wangu nimebatika kusoma shule moja na ridhiwani kikwete

Huyu sifa zake ni kwamba
1. Alikuwa anajituma sana na ni mtu anaye weza sana masomo darasani,

2. Alikuwa Ana hekima ya kulelewa, haikuwa rais kugundua kama ni mtoto wa waziri kipindi kile, na aliweza sana kuficha identify hiyo,

3. Sikuwahi kuona anapewa adhabu au kuadhibiwa kwa makosa ya siyo kuwa ya msingi. Kama anapata adhabu basi hiyo ilikuwa ya kulikumba darasa zima,

4. Kuna mwalimu mmoja alikuwa anatwambia kwamba siku akikuta waliofanya makosa na ridhiwani yumo basi alikuwa na kigugumizi hata kutoa adhabu, na kama anasamehe kundi basi ni kwa sababu kuna kijana mwenye adabu,

Nakumbuka siku moja tulikuwa na utani sana darasani tukafoji muhuri Fulani ili tuwatanie vijana tarehe moja April siku ya wajinga, tukaandika kuwa wamelipa Ada yote hawadaiwi, sasa kwa ujinga hatukujua kama ni kosa ,

Mimi nikawa nagawa zile receipt kwa wanafunzi tunaoona ni mazuzu, wakapeleka nyumbani lakin wajanja wajagundua tunawatania,wakazichana, sasa ziku ya kufukuza Ada ikafika akaja mwalimu maarufu kwa jina Walter wakaanza kusoma ambao hawajalipa Ada, kuna mdada mmoja mjinga mjinga kumbe Ile receipt kaiweka kwenye shati. Akasema nimeshalipiwa na ridhiwani na **** , msaala ukaanza tukaitwa mpaka kwenye ofis ya mkuu wa shule naye alikuwa mtata kweli, alivyoanza kutuadhibu mwalimu mmoja akaja kwakuwa alimuona ridhiwani pale akasema hata barua zile tulizokuwa tumeandikiwa kufukuzwa wakakaa kujadili. Wakatusamehe ila viboko tukapokea, na mwalimu akatwambia kuwa mmesamehewa kisa huyu,

Si kwamba kwa kuwa ni mtoto wa waziri bali nidhamu yake
Wakati huo tulikuwa na watoto wa vigogo wengi wanafukuzwa tu,


Hivyo tunaomba waliosoma na Makonda,

Waliosoma ma magufuli

Waliosoma na kikwete

Waliosoma na Nape

Au kiongozi yeyote weka hapa na tabia yake ya utotoni
Mimi nilisoma na makonda lakini sio huyu mkuu wa mkoa, makonda alikuwa na akili sana darasani, chakushanganza eti alimuuzia vyeti Albert bashite
 
Nimesoma na Kamanda mpya wa Traffic jamaa wa Musoma Mara.
Ubabe wake tangu chuo. Mpirani sasa! Mtemi kweli.
Upolisi unamfaa.
Vema sana ni kamanda nani, mpunga au nani
 
Nilisoma na Julius Mtatiro, alikuwa kiongozi wa chakula alafu mtata kweli yule mkurya. Alikuwa akimdate dada mmoja anaitwa Grace na ilijulikana hadi na walimu ila hata hakufanywa lolote. Sijui ndio alikuja kumuoa!!
 
Nilisoma na Julius Mtatiro, alikuwa kiongozi wa chakula alafu mtata kweli yule mkurya. Alikuwa akimdate dada mmoja anaitwa Grace na ilijulikana hadi na walimu ila hata hakufanywa lolote. Sijui ndio alikuja kumuoa!!

Ha ha ha, Mtatiro alikuwa kiongozi wa Mambo ya Mikopo UD, jamaa alikuwa anapenda issue za migomo sana, yaani yeye utatuzi wake wa swala lolote ni mgomo tu.
 
Rtd General Davis Mwamunyange......Mawenzi Secondary School:1967 to 1970.
Alikuwa mpole na kichwa yake imejaa vitu....ni namba moja tu miaka yote hiyo,hajawahi kuwa wa pili.
Hekima na busara tokea shule alikuwa nazo.
 
Me mimesoma na John,nakumbuka alikua mchoyo sana darasani

Siku moja bhana ilikua mtihani wa mid term nimekaa nyuma yake nikaomba anisaidie swali la 3(nafikiri atakumbuka hili tukio)akasema hajajaza kumbe kamaliza maswali yote,sasa cha ajabu siku majibu yanarudi ana 0% kumbe alikariri paper lililopita akidhani yatakuja vile vile
.
.
Ni mchoyo tangu shule hataki mwingine afanikiwe ilihal mwenyewe anaharibu
ha ha ha haaa!!!! atakuwa John mnyika huyo.
 
Back
Top Bottom