Special thread : Messi Magics

Special thread : Messi Magics

Kuna watu unawazaga kumwomba Mungu awaweke milele wawe wanakupa burudani siku zote za maisha yako ila haiwezekani..

Kuna Messi, kuna Gaucho, kuna Zizzou na kuna Okocha

Hao mafundi wa mpira dunia hii sijui kama tutaona wengine.

Wachezaji wengine wote wakasome.

Honourable mentions..

Luis Suarez huyu jamaa ukiachana na tabia zake za kijinga basi huyu ni mchezaji niliependa sana kazi yake, yani shughuli yake beki zinakuwa zinajijambia mda wote awe na mpira asiwe nao shughuli yake sio mchezo.

Frank Lampard, Chogo Henry, Stevie G... Hawa watu bwana shughuli yao ilikua sio mchezo. Kinachoniumaga ni Stevie G kutoshinda kikombe cha EPL ila huyu bwana nahisi ule mguu wake wa kulia una uzito mkubwa kuliko wa kushoto, sio kwa thunderbolt zile..

Kuna game moja Olympiacos vs Liverpool mwaka 2005 kama sijakose mjinga alipiga duki moja mpaka commentator Peter Drury akabaki kusema "Gerrarddddddddddd...... What a hit son, what a hit"

Pipo Inzaghi, huyu jamaa jina lake halikuwika sanaaa ila huyu alikua mchawi wa fainali, alikua akifunga magoli muhimu tu. AC milan ya wakati huo ilikua na majembe ya kazi.. Vitasa kama akina Nesta, Maldin, Gattuso, Cafu.. Ilikua shida

Baba lao De Lima, chenga yake ya bicycle ile alikua anawavunja viuno mabeki.. Huyu nguli atakumbukwa ila alishindwa kushinda Uefa..


Ricardo Kaka, bwana huyu mlokole alikua anaujua mpira

Kwa vijana wanaokuja..

Huyu Ousmane Dembele ni fundi wa mpira, Coutinho huyu huwa ananikosha kwa magoli yake ya mbali, Anthon Macho huyu atakuwa mzuri sana baadae, Isco Malaga fundi sana huwa naburudika nikimwona huyu kijana. Neymar jr huyu ana kipaji na juhudi, sema huwa namuona kama CR7 (sijawahi kumkubali sana)

Wengine ntaongeza baadae ila hao watu hapo mpira wanaujua ila Mungu wao Messi wengine watakuwa mitume na manabii

Mkuu. Umemsahau Dybala.
 
FB_IMG_1507709703942.jpg
 
Dybala anaujua lakini kuna hii Hapa angalia Messi alichomfanyia




Teh teh teh teh___ndiomaana nikasema "ni dhambi kubwa kumlinganisha KING MESSI na michezaji iliopita na ya sasa. Wengine imefikia kumlinganisha na MAUNO. gaucho/Mauno wapi na KING MESSI wapi___ ni heri ukutane na mbweha lakini sio LION MESSI.
 
Jamaa ana kipaji Na maarifa,speed&accuracy ya kipekee ktk football,Huyu kiumbe anachezesha timu sio utani,anafanya kazi zaidi ya inavyobidi iwe kwa maana MTU mmoja in kama watu 4!
Sijui labda Hugo Pele maana hatukuwahi kumshuhudia kwa miaka hiyo lkn kwa wengi waliofuata hadi sasa,Hakuna kama Messi!
Kwa Mashahidi waliotazama 2nd Leg ya kombe la mfalme Spain usiku wa alhamis hii Barca dhidi ya Espanyol (2-0)Na hata mechi ya barca ya ligi wiki iliopita watakubaliana nami.
 
Back
Top Bottom