Kuna kauli nyingi zimewahi kutolewa kitambo na wanasiasa katika nyakati mbalimbali ambazo baadhi zimekuwa zikijirudia lakini pia nyingine zimetekelezwa kama walivyoziongea hata kama baadhi au wengi wetu yuliona ni za kipuuzi.
Tutumie uzi huu kutupia kauli hizo, tukiwa na video itakuwa poa sana tusaidie hata Gen Z na Alpha kujifunza kutokana na historia wakati wao ukifika wafanye mambo tofauti, na kuacha upuuzi uisyo na maana kando.
Mimi naanza na hii;
Mwenyekiti wa UVCCM Ndg. Heri wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2020 kuwa; "Wewe endelea kuwajaza upepo, wala hatutumii nguvu kubwa, ni sindano pyuuuuu! Na vijana wa Arusha acheni hiyo anawadanganya kwamba polisi watatufanya nini, acheni. Atatangazwa kwa wale walioshindwa kwenye taarifa za habari lakini siyo kwa ushindi wa Urais wa nchi hii.."
Your browser is not able to display this video.
Basi waja tukaunganisha dots kuwa safari hii haitakuwa shambulio la risasi tena bali kupigwa sindano ya sumu. Na huyu jamaa hakufanywa lolote hata baada ya kutoa kauli hii.