Special Thread: Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB). Karibu tukusikilize

Tume inafanya kazi zake kwa mujibu wa Ibara ya 130 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 pamoja na sheria ya Tume Sura ya 391 ya sheria za Tanzania. Mafanikio, changamoto pamoja na muonombele unaweza kuyapata kwenye taarifa zake zinazopatikana katika Tovuti ya THBUB
 
Viongozi wa Tume na watendaji wake wanapatikana kwa mujibu wa sheria ya Tume ikisomwa pamoja na Kanuni zake.
Maana ya Tume kuwa huru ni kitoingiliwa na mtu yeyote katika utendaji wa kazi zake. Tume iko huru katika utendaji wa kazi zake na haipokei maelekezo kutoka kwa mtu yeyote na haingiliwi na mtu yeyote wakati wa kutimiza majukumu yake
 
Tume Haki Binadamu(THBUB)
Hii Tume ndo mnaotetea haki za mashoga na u feminist? Kama ni ndio mpuuzwe na kila mwenye akili timamu.

Sijawahi msaada wenu wala kupaza sauti kukemea watekaji nk
Tume ya Haki za Binadamu haifanyi kazi za uhanarakati bali inafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria za nchi. Sidhani kama una ushahidi kuhusu jambo hili. Tume itaendelea kuhamasisha ulinzi wa haki za binadamu nchi kama zilivyoainishwa kwenye Katiba ya nchi, mikataba ya Kimataifa na Kikanda.
 
Naona nyie kwenu kutekana tekana na kuuana siyo uvunjifu wa haki za binadamu ndio maana hamjshughulishi nalo.
Hàmna maana yoyote kama maisha ya binadàmu hayana thamani kwenu.
 
Huduma zetu ni bure,hazina malipo yeyote
daah nyie ni jipu jingine yaani mnahitaji siku nane (8) kujibu swali moja. swali la Dec 11 mnajibu Dec 19, seriously? bahati yenu ke.n.ge nyie maana kwa style hii mtu kama mwendazake angeshawapitia chap kama kipanga.
 
December 11,2024 niliandika mchango wangu kwenye huu ukurasa wenu mnaoita rasmi,post #16,mpaka leo haijajibiwa
Hii inaniacha na mashaka makubwa kuhusu tume yenu:


1_Hamko huru kama mnavyodai,mnaogopa kuchunguza baadhi ya mambo.If this is the case,hamkupaswa kuja public na kuanzisha ukurasa wa kukusanya maoni.Utekaji unaondoa/hatarisha uhai wa watu,raia wa nchi hii,yet tume yenu imekaa kimya kana kwamba hakuna kinachotokea.


2_Au nyie ni sawa tu na ofisi zingine za umma,mmejawa na uzembe,na kutowajibika.Inawezekana hata kuja kufungua page hii ilikuwa ni maagizo ya boss,na yeye hajawahi hata kuulizia hata maoni ya kwenye page aliyoagiza ifunguliwe .
BADILIKENI,FANYENI YALE YANAYOGUSA MAISHA YA RAIA,CHUNGUZENI NA KUTOA TAARIFA KWA UMMA.KWA NJIA HIYO MTAJIJENGEA HESHIMA KWA UMMA.VINGINEVYO FUTENI PAGE HII,MUACHE KUTUSUMBUA NA MAMBO AMBAYO HATA NYIE WATENDAJI HAMUYAAAMINI.HAKI ZA BINADAMU JAMBO NYETI ,ACHENI MZAHA
 
Tume ya haki za binadamu jibuni maswali ya watu
 
Hii taasisi ifutwetu Ili kupunguza matumizi serikalini na kulinda kodi zetu. Au mnasemaje wanajukwaa?
 
Uongo.
Nakumbuka enzi za Jiwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…