Special Thread: Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB). Karibu tukusikilize

Karibuni sana jamvini.. kuelekea uchaguzi mtatufaa sana.. muwepo lakini
Ombi: Kwenye mifuko ya Jamii kuna jambo Moja namba mlifanyie kazi tafadhali sana ,nalo ni hili:Mtu anapaswa achangie miezi 180(miezi mia na themanini),Lakini ukienda kama ulifikuzwa kazi unaambiwa haumo Labda kama ulilipwa mapunjo!Sioni kama ni kumtendea Haki huyu Mwananchi
1.Kalitumikia Taifa hata kama alifukuzwa kazi, maana kuna mambo mengi kazini,majungu,fitina nk Na wengi wao walienda mahakamani na wakashinda kesi na kumalizana na waajiri wao Kwa Amani.
2.Kuwanyima mafao ya Kila mwezi ni kuwahukumu mara ya pili(2)Na kuwnyanyapaa!Kwani ni Watanzania na hawana ajira Tena.
3.Waliopunguzwa makazini wao hulipwa wakifikisha huo umri wa kustaafu kwa hiari,yaani miaka Hamsini na Tano(55),Hivyo na Hawa wa kufukuzwa/Kuachishishwa wawe pia miongoni mwao wa wanufaika wa mifuko hiyo ili kuwapunguzia maumivu ya Maisha.
Ahsante kwa kusoma,Naamini yatafanyiwa kazi kwa Hekima na Busara.
 
Swali
1. Kama tume yenu Ina nguvu kwanini utekaji Tanzania mmeshindwa kuukomesha hata pengine kuupunguza kwasababu unahusu haki, je hukumu ya mkosaji ni kutekwa na kupotezwa

Swali
2. Haki ni pamoja na kumchagua unaye muamini atakuwakilisha yaani kumpigia kura mtu unayempenda kwanini hii haki inapokwa?
Tumeshuhudia kipindi cha uchaguzi ndiyo kipindi cha watu kupokwa haiki ya kushiriki uchaguzi na kuishi
 
Hamna kazi mnafanya. Ni sawa na dawati la jinsia tu mnaweza kukoromea vijikesi vya kifamilia hasa mwanaume akikosea
 
Wamepotea
 
Nadhani kwa sasa kuna Binadamu na Binadamu sana, Binadamu sana ndiyo wenye haki ila Binadamu hawana haki.
 
Haki kwa Tanzania haina definition
 

Tume hii ni upotevu wa fedha za walipakodi wa nchi hii, ni vyema Sana ikafutwa Mara moja. Hakuna kitu chochote kile Cha maana kinachofanywa na Tume hii. Ni upuuzi tupu.
 
mnalipwa mishahara kwa majukumu yepi hasa maana hali ya haki za raia hairidhishi
 
Msaada: Ikiwa mwajiri ( Mkurugenzi mtendaji wilaya) amemtengenezea tuhuma mfanyakazi wake na akamchukulia hatua. Kifupi Mwajiri amebadilika kuwa mamlaka ya nidhamu, Ni lalamike kwa nani,
 
Ulipoti wapi Au nifuate hatua zipi kumlalamikia mwajiri( Mkurugenzi mtendaji wa wilaya), Msaada tafadhari
 
Unaita utekaji ni uhanaharakati?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…