SPECIAL THREAD: Uzi maalumu kwa wapenzi wa usafiri wa anga

SPECIAL THREAD: Uzi maalumu kwa wapenzi wa usafiri wa anga

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Wakuu salaam,

Huu ni uzi maalum kwa ajili ya kujadili na kupeana updates kuhusu usafiri wa anga, historia, na yajayo kwenye sekta hii.

Karibuni sana wanazi wenzangu.

===

Kwa kuanza tuanze na story kubwa zaidi kwa sasa ambayo ni majaribio ya ndege aina ya Airbus 350-1000ULR.

1. Safari ya Kuvunja Rekodi hewani!

Mnamo Julai 2026, ndege mpya na maalum ya Airbus inayojulikana kama A350-1000ULR (Ultra Long Range - yaani masafa marefu zaidi) ilifanya safari yake ya majaribio ndefu zaidi kuwahi kutokea. Iliruka moja kwa moja kutoka Toulouse (Ufaransa) hadi Melbourne (Australia), na kisha ikarudi. Fikiria ndege kukaa hewani kwa saa 24 na dakika 24 mfululizo bila kutua, ikivuka umbali wa maili za baharini 12,460!
SaveClip.App_759373278_18612454597014103_1970663245150480800_n.jpg


2. Kwa nini walifanya majaribio haya?

Lengo kuu lilikuwa kuthibitisha kuwa ndege hii inaweza kuhimili mikikimikiki ya kuruka kwa zaidi ya saa 23 mfululizo. Hili ni jambo muhimu sana kwa shirika la ndege la Qantas lenye mpango uitwao "Project Sunrise," ambao unalenga kuanzisha safari za kibiashara za moja kwa moja zinazochukua hadi saa 21 (kama vile kutoka Australia hadi Ulaya), bila kusimama popote kubadili ndege au kuweka mafuta.
1785738488354.png


3. Siri ya Tanki la Ziada

Ili ndege iweze kusafiri umbali wote huo bila kuishiwa mafuta, imeundwa na tanki la ziada la mafuta lenye uwezo wa kubeba lita 20,900! Wataalamu walitumia safari hii kuhakikisha kuwa tanki hili na mifumo ya mafuta inafanya kazi barabara ukiwa angani kwa muda mrefu sana.
1785738512108.png


4. Faraja na Kupokezana Zamu

Kuruka kwa saa 24 sio mchezo, marubani wanaweza kuchoka sana! Hivyo, kulikuwa na jopo la marubani kutoka Airbus wakishirikiana na marubani wa Qantas. Ili kuepuka uchovu, waliweka utaratibu mzuri wa kupokezana majukumu kila baada ya saa mbili. Pia, walitumia nafasi hii kupima ubora wa hewa ndani ya ndege (air conditioning) na ubora wa vyumba maalum vya kupumzikia marubani (Rest Compartments) ili kuhakikisha wanalala kwa amani bila usumbufu.
1785738449109.png


Kwa ufupi:

Majaribio haya yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa na ni habari njema sana kwa wasafiri. Inamaanisha kwamba katika siku za usoni, kusafiri dunia nzima bila kulazimika kusimama vituo vya njiani kutakuwa jambo la kawaida, salama, na la kustarehesha!

Source Airbus

1785738414829.png
 
Nimekumbuka AIR CONCORD, ni ndege ya kwanza kuwa na speed ya hatari, ilipelekea kupiga chini ushindani wa makampuni mengine. Eneo ambalo ilikuwa ni masaa 8 kufika, yenyewe ilichukua masaa matatu

Tatizo ilikuwa ni nauli kubwa sanaa
 
Nimekumbuka AIR CONCORD, ni ndege ya kwanza kuwa na speed ya hatari, ilipelekea kupiga chini ushindani wa makampuni mengine. Eneo ambalo ilikuwa ni masaa 8 kufika, yenyewe ilichukua masaa matatu

Tatizo ilikuwa ni nauli kubwa sanaa
Yes mkuu lakini pia inaelezwa chuma zilikuwa zina gharama kubwa ya uendeshaji mana zilikuwa zinatumia mafuta mengi sana, halafu zinabeba abiria wachache wasiozidi mia.

Kwa mara ya mwisho Concord iliruka safari yake ya mwisho Oktoba 24, 2003 kwa safari za abiria na ya mwisho isiyo na abiria ilikuwa Novemba 26, 2003
 
Mradi uligharimu takribani dola bilioni moja na uliiweka Boeing kwenye hatari ya kufilisika ikiwa ndege hiyo ingeshindwa.

Safari ya kwanza ya kupaa kwa ndege ya kwanza ya aina ya Boieng 747 (N7470).
1785911892191.png

Shirika la ndege la Pan Am lilihitaji ndege kubwa ya abiria na ndipo walipowafuata Boieng kwa ajili ya jambo hilo na ndipo wazo la ndege aina ya Boieng 747 lilipoanzia. Kwa wakati huo hakukuwa na kiwanda duniani kilichoweza kuijenga.

Na hapo ndipo Boeing ilisafisha msitu kaskazini mwa Seattle na kujenga kiwanda cha Everett, jengo kubwa zaidi duniani kwa ujazo.

Ndege hiyo iliundwa na wafanyakazi 50,000 ambao walijiita "The incredibles". Mradi huo uligharimu takribani dola bilioni moja na uliiweka Boeing kwenye hatari ya kufilisika ikiwa ndege hiyo ingeshindwa.

Na kwa mara ya kwanza ndege hiyo mpya iliruka Tarehe 9 Februari 1969, ikiwa na marubani Jack Waddell, Brien Wygle na Jess Wallick, ndege hiyo iliruka kwa saa moja na dakika 15 bila matatizo.
1785911908186.png

Baada ya kutua, Waddell aliita Boeing 747 “ndoto ya rubani,” akisema ilikuwa rahisi kuiendesha. Boeing baadaye ilijenga ndege 1,574 za aina hiyo. N7470 leo ipo kwenye Museum of Flight, Seattle, ikiwa kumbukumbu ya uvumbuzi uliobadilisha historia ya usafiri wa anga.
 
Ndege kubwa ya kwanza ya umeme yafanya safari ya majaribio.

Kampuni ya Heart Aerospace imefanikiwa kurusha ndege yake ya majaribio ya X1 yenye ukubwa kamili kwa mara ya kwanza, na kukamilisha safari ya majaribio ya dakika 27 kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Plattsburgh huko New York.

Wakati wa safari hiyo, ndege hiyo ilipaa hadi futi 1,100 juu huku injini zake nne za umeme zikizalisha zaidi ya megawati 1 ya nishati. Ikiwa na mabawa yenye upana wa futi 106 na uzito wa zaidi ya ratili 25,000 wakati wa kuruka, Heart inasema X1 ndiyo ndege kubwa zaidi inayotumia betri za umeme kuwahi kuruka angani.

Safari hiyo iliyoongozwa na rubani ilifanywa chini ya cheti cha majaribio cha uidhinishaji wa usalama wa ndege kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga (FAA) na ilijumuisha majaribio ya kuruka, kupaa, kuongoza mwelekeo, na kutua.

Ndege ya X1 haikukusudiwa kwa ajili ya huduma za kibiashara za kubeba abiria. Badala yake, inatumika kama chombo cha majaribio kwa ajili ya ndege ya kikanda aina ya ES-30 yenye uwezo wa kubeba abiria 30 iliyopangwa na Heart Aerospace, ambayo imeundwa kutumia mfumo wa nishati ya betri za umeme sambamba na mfumo mseto (hybrid). Kampuni hiyo inalenga kupata cheti rasmi cha idhinisho kwa ajili ya ES-30 ifikapo mwaka 2031.
 
Back
Top Bottom