Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Kweli sababu ukigusa unakuja page ya jamii forum yenye categories mbalimbali hapo ndipo naishia na sijui pakwenda.
Tumia njia hii.

1-select hiyo reply unayotaka kuona video
2-nenda kulia juu kuna dots 3
3-bonyeza hapo kisha chagua Open in Browser
4-Pop up itatokea utachagua browser yako kisha yenyewe itaload tu hiyo post
 
Daraja la Antonovskiy limeshambuliwa leo Usiku huko Kherson. Hili Daraja linaunganisha Kherson na Crimea ambayo ipo chini ya Urusi tangu 2014.

Inaonekana air defence systems zimeshindwa kudaka hata missile moja iliyokuwa inaelekea darajani. Ukriane wakifanikiwa kuliharibu hili daraja, inamaanisha Njia ya Kuretreat kwa Urusi itakuwa haipo, itabidi wajisalimishe. Pia hakutakuwa tena na Ugavi wa Silaha, chakula na risasi.

Wakijaribu kutengeneza daraja la makeshift, watapata maafa makubwa kwani Jeshi la Ukriane lishajua ndo kitu pekee chaweza fanyika

Wanajeshi wa Urusi waliopo Kherson wanauoga, hawajui waende wapi.

Maana yake hii ni sawa na kuzungukwa.. Mbele huendi, nyuma huendi. Kumbuka HIMARS imeshaharibu Maghala yote ya Sikaha za Urusi ya Kherson. Huu Mkoa kazi imeisha.. Twende zetu Donetsk kisha tumalize na Luhansk. Ukraine itakuwa imemaliza Vita.
Your browser is not able to display this video.
 
Amelitafuta mwenyewe wacha limpate,

Mwenzake lavrov yupo Uganda anatafuta uungwaji mkono kweli wamechanganyikiwa

Wapelekewe Moto tu.
 
Hawa wanajeshi wanasaidia Frontline ya Ukraine huko Kherson na wanatokea Georgia. Wamesema wapo tayari kulinda daraja kama litabomolewa. Wanataka wapewe vifaa wanavyotaka halafu kazi waachiwe wao kuhakikisha nzi hakatizi kurudi Urusi. Makomandoo huwa wanajiamini sana
 
Vile vifaru vilivyoletwa vya Ujerumani aina ya Gepard, vikiwa kazini hivi ndivyo vinatema risasi.🤣🤣🤣🤣 Ndege haikatizi wala kitu chochote kinachoruka angani. Asanteni sana Ujerumani
Your browser is not able to display this video.
 
HIMARS nyingine hizi hapa, zinakaribia kufika Ukraine. Zinakija zikiwa loaded. Zinakimbia kama vieite tu🤣🤣

Kumbuka hayo magari madogo yana Wanajeshi wanaozilinda zisitekwe.. Battalion nzima ipo hapo. Wahandisi, Madaktari, Manesi, nk.. Kwamba zilikuja na Ukinzi pia wa Snipers 12.

Hayo magari madogo yalowasha taa, yote yanalinda HIMARS zisiangukie mikononi mwa adui. Zoom kuona picha vizuri
Your browser is not able to display this video.
 
Ni ngumu kwa air defence za Urusi kushambulia makombola ya himars sababu makombola haya husafiri kwa muda mchache na spidi kubwa
Husafiri kwa 3000km/hr yanasafiri urefu wa km 80, ndani ya sekunde 94 tu yanakuwa yashafika kwenye target. Na pia haya husafiri kimo kifupi hivyo radars haziwezi ona kirahisi na kufanya maamuzi
 
Well done. 👏👏👏👏
 
Yaani Daraja la Antonovsky nilitamani lishuke kabisa. Ila naona kuna nondo bado zinashikilia japo hamna kifaa kizito kinaweza kukatiza. Ukraine tujipange upya waondoke na nguzo.. Si haba. Urusi kama wana akili wakimbie haraka. Ikipigwa hapa tena, hapasalii kitu
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…