RTI
JF-Expert Member
- Dec 20, 2018
- 2,423
- 7,155
Hebu ww tuambie angetumia njia gani zaidi ya hii wakati mazungumzo yalikuwa yamesha feri?Hatumii nguvu kubwa kivipi?....au sababu hajatumia nuclear?
Kwani kilikuwa hakuna mbinu zingine za kuizuia Ukraine kujiunga Nato mpaka Vita?.
Hii Vita itaifanya Nato kujiimarisha zaidi huko Ulaya mashariki hasa kwenye mataifa yaliyokuwa chini ya ushawishi wa Ussr.
Ndiyo hatumii nguvu kubwa ukitaka kulijua hilo angalia kiwango cha uharibifu kwenye makazi ya watu na miundo mbinu ni kidogo na vifo vya raia ni kidogo.
Urusi ingekuwa inatumia nguvu kubwa maelfu ya watu wangekuwa wamesha uawa na uharibifu wa miundo mbinu ingekuwa mkubwa sana.
Hivi Ukraine ingekuwa inapata presha ya mashambulizi ya anga makali kama yale Urusi aliyo yafanya Aleppo unadhani ni maelfu ya watu wangapi wangekuwa wameuawa?
Katika dunia ya sasa hakuna mteremko na Putin analijua hilo na amejipanga.