LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Hebu ww tuambie angetumia njia gani zaidi ya hii wakati mazungumzo yalikuwa yamesha feri?

Ndiyo hatumii nguvu kubwa ukitaka kulijua hilo angalia kiwango cha uharibifu kwenye makazi ya watu na miundo mbinu ni kidogo na vifo vya raia ni kidogo.

Urusi ingekuwa inatumia nguvu kubwa maelfu ya watu wangekuwa wamesha uawa na uharibifu wa miundo mbinu ingekuwa mkubwa sana.

Hivi Ukraine ingekuwa inapata presha ya mashambulizi ya anga makali kama yale Urusi aliyo yafanya Aleppo unadhani ni maelfu ya watu wangapi wangekuwa wameuawa?

Katika dunia ya sasa hakuna mteremko na Putin analijua hilo na amejipanga.
 
Ndani ya masaa 48 Kiev itakombolewa na warusi na huyo rais comedian atatimua mbio za mwaka!
 
mkuu mbona kama ujeruman amekuwa mgumu kutoa sapoti kwa ukrain ana maslahi gan
maana hata kwenye baadhi ya vikwazo amekuwa kikwazo kuviidhinisha dhidi ya urusi.
Ujerumani imekuwa ikiisapoti Ukraine katika masuala mengine mengi. Kuhusu silaha; Ujerumani ina sera ya muda mrefu ya kutopeleka silaha za mashambulizi katika maeneo yenye migogoro.

Licha ya hilo, pia ni miongoni mwa nchi ambazo zimekuwa na mahusiano ya kiuchumi na Urusi hasa kupitia mradi wa gesi kutoka Urusi wa Nord Stream unaopitia bahari ya Baltiki.

Ujerumani hapo awali ilitazamia kuumaliza huu mgogoro kwa njia ya mazungumzo, hata kansela wao alikwenda mpaka Moscow pamoja na Kyiv kufanya jitihada za kuzuia hii vita. Baada ya hapo, Ujerumani haikutarajia kama hali itabadilika na kuwa kama sasa ila iliweka wazi kuwa itaisapoti Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Kusitishwa kwa hiyo sera ya kutopeleka silaha katika migogoro kunatokana na hali ilivyo kwa sasa baada ya mazungumzo kushindikana. Hivyo Wajerumani wanaona hakuna sababu tena ya kuzuia misaada ya silaha ukizingatia aina ya mgogoro ambao unaweza kutishia zaidi usalama wa Ulaya. Hata mradi wa bomba la pili la gesi (Nord Stream 2), Ujerumani imeusitisha.
 
Hawana choice.
Wanayo. Masaa kadhaa yaliyopita Russia wameendelea na mashambulizi sababu Eukraine hawajawa tayari kuzungumza. Puttin aliwaambia wasipigane lakini bado wamechagua kupigana na kuomba kuongezewa silaha. Kwann?
 
mnatuvuruga bore mtuwekee updates sio story ! mfano jeshi la urusi bado kilo 15 kuingia kyiv au ukraine imerudisha miji yote ilokuwa chini ya urusi ! sio story km zile yule waziri wa habari wa iraq mara sahv tumechora mstari mwekundu wakiingia tumewamaliza [emoji23]
 
Ndani ya masaa 48 Kiev itakombolewa na warusi na huyo rais comedian atatimua mbio za mwaka!
Hii ni possible maana ameshabadilisha mwenendo aliokuwa nao awali... Ambapo kila wakati alikuwa akionekana kwenye media... But now hajulikani alipo... So means mapambano yamekuwa mazito
 
Urusi harudishagi maiti za Askali wake. Maiti za Wanajeshi wa Urusi zimezagaa Kiev mpaka Rais wa Ukraine amewaomba shirika la Msalaba Mwekundu kwenda Kuziondoa.
Tuonyeshe, mtaa upi unapoziona hizo Maiti.
 
Urusi anapiga na NATO allies akiwa anajua ni Ukraine.

Watu wanaona Rais wa ukraine anakunywa kahawa na kupiga selfie hata hawashtuki.

Urusi, inabidi afanye Tathimini upya.
 
kaangalieni hii vid twitter ndo mtajua russia sahv kachafuka ! wengi mnaona takwimu za russia kupigwa sabubu hashtag ya ukraine inapostiwa sana na watu wanaonea huruma ukraine na wengine wanafanya propaganda
 
aaah wapi nacheki france 24 muda huu wanjeshi wa rusia wamevamia ambulance iliobeba majeruhi na wamemuua dereva na kuilipua kabsa
mrusi hakuna anachokifanya cha maaana hapo ukraine zaidi ya kuharibu miundombinu na kuua raia
 
Urusi anapiga na NATO allies akiwa anajua ni Ukraine.

Watu wanaona Rais wa ukraine anakunywa kahawa na kupiga selfie hata hawashtuki.

Urusi, inabidi afanye Tathimini upya.
Kha yamekuwa hayo tena mkuu ama....usinambie kuwa Nato ashapeleka wanajeshi huko Ukraine...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…