LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Urusi na team yao huku namtumbo hawaamini wanachokiona, walitegemea itakua nyepesi tu siku moja wamemkamata rais vita imeisha, wapi hahahaa wanaume wamesimama tambo za bure yani Ukraine anakuweka siku 4 unapambana tu halafu mnasema super power.
Wameshaanza kuleta blah blah zao hapa za Urusi alipisha mazungumzo
 
Huko kiev hali si shwari... Kuna group la Ukraine wanalalama kwamba jamaa Mrusi anatupa vitu vizito
Leta na group za Russia vile Putin anavyohangaika kuwadhibit wanaoandamana kupinga vita pia,wao wanasemaje au unadhani Wananchi wa Russia wote wanafurahia kinachoendela kwa sasa?
 
Wameshaanza kuleta blah blah zao hapa za Urusi alipisha mazungumzo
marekani hadi kumkamata tu sadam alitumia wiki tatu. kule afghan hadi wameondoa wanajeshi na taliban wakabeba nchi. unajua kilichotokea kule kwa wenye vimacho vidogo.
 
Eukraine ni mtoto sana kwa Russia.
 
Putin yeye hana colateral damage? Chapwa hii ni vita ya nchi mbili. Russia Anaivamia sababu ni taifa weak na lililotokana na Russia hivyo anaona linatakiwa lifuate maelekezo yake. Otherwise lingekuwa na nguvu kama China Puttin angeliheshimu na asingelipangia.
 
View attachment 2132455Eukraine ni mtoto sana kwa Russia.
ni mtoto kupigana kwenye uwanda, ila kupigana kwenye corridor za mitaa hakunaga hiyo comparison, kwasababu pale ili kupiga unatakiwa kufanya mahesabu makubwa sana ili usivunje sheria za kivita ukimaliza vita uanze kusumbuliwa, jua hayo ni civilian residence hivyo huwezi kupiga tu. chukua mfano wa israel vs hezbulah na hamas, wakianza kupigania mitaani kwenye majengo lazima israel hawezi kupiga tu hovyo la sivyo anaweza kudondosha majengo yote. ndicho kinachotokea kwa russia, alipotoka kwao ameingia nchini ukrain kirahisi tu kwa kutumia ndege na helcopter, ila alipofika kiev na miji mingine ukrainians ndio wamejificha na kujipanga kwenye mitaa ya majumba, hivyo inatumika akili kupigana huwezi kurusha tu makombora, kwa sheria za kivita, kibaya ni kwamba vyovyote atakavyofanya au whatever time it will take, ni kwamba anapigania nyumbani kwako kwahiyo kama kuna kitu kinavunjika ni vyombo vyako na kuta za nyumba yako.
 
Putin yeye hana colateral damage?
damage alizonazo ni kwa vifaru na wanajeshi tu ambao ni kitu cha kawaida kufa au kupotea, lakini sio miundombinu ya kijeshi, miundombinu ya raia na majengo, maafa ya raia, miundombinu ya kiuchumi n.k. kule nyumbani kwake russia kupo salama, ila ukrain majengo yanadondoka, vituo vya kijeshi vyote vimesambaratishwa, umeme wameteka, anayepoteza zaidi ni nani? kwanza putin hayupo vitani analala fresh nyumbani kwao, ila comedian yupo vitani mtaani halali hata kulala.
 
it is very challenging, marekani na wadau wake wanamshauri dogo adindishe kwa putin, halafu kikinuka hawaji kumsaidia, na hawawezi kumpa silaha bora kwasababu wakimpa tu Russia ataziteka na kuondoka nazo kwenda kuzifanyia maboresho kuwa na silaha bora kuliko wao, wanaishia kumpa malonya tu. wamemshauri apigane, halafu waliopoona amepondwa wanaleta gari wanamshauri akimibie nchi, hivi kweli wapo serious? akimbie nchi halafu je? si ili aiache nchi yake mikononi mwa russia? na ili wanajeshi wake watekwe na russia? Marekani amemshauri jamaa akimbie, unafikiri marekani ameona nini?
 
Russia ni super power, huwezi mlinganisha na Eukraine. Pili Eukraine imejimega kutoka Russia. Ni sawa na Tanganyika iivamie Zanzibar halafu tutegemee Zanzibar ishinde.
Kitendo cha Eukraine kuhold on mpaka sasa kunamuumiza Russia sababu kunawapa nafasi maadui zake kumwongezea mavikwazo. Leo wamemuongezea mavikwazo matatu.
 
Kukikucha tutakaa meza moja kupata kifungua kinywa.
 
Russia ni super power, huwezi mlinganisha na Eukraine. Pili Eukraine imejimega kutoka Russia. Ni sawa na Tanganyika iivamie Zanzibar halafu tutegemee Zanzibar ishinde.
hata marekani ni superpower lakini imesumbuliwa na wataliban tu kwa miaka mingi hadi wakaamua kuondoka, maelfu ya wanajeshi wa marekani wameuawa na taliban, na walikuwa hawapiganii kwenye mitaa ya majengo kama ukrain, walikuwa jangwani huko na kwenye milima, ila US hakuwamaliza, sasaivi wanaongoza nchi yao. on the other way, Ukran imekuwa trained na NATO tangu 2014, wamepewa silaha kadhaa na nato, kama ambavyo huwezi kulinganisha USA na afghanistan au iraq, ndivyo ambavyo hutakiwi kuidharau ukrain dhidi ya russia, sio mtoto kihivyo hata kama russia ni superpower.
 
Tuachane na wamarekani. Russia yupo vitani na Eukraine. Wamarekani na wao wanaangalia kwenye Tv kama sisi. Sijaidharau Eukraine, nawaona wapo vizuri na wanasababisha Russia aumie. Wasingehold on mpaka leo Russia Banks zisingekutana na majanga ya swift na asset kuwa freesed.
 
Tuachane na wamarekani. Russia yupo vitani na Eukraine. Wamarekani na wao wanaangalia kwenye Tv kama sisi.
mimi mwenyewe hivi ninavyoandika naangalia al jazeera, france 24, bbc na RT ya urusi. kiukweli kila palipo na vifaru vilivyoteketezwa au magari yaliyoteketezwa naona ni vya ukrain, na hapo jua media za magharibi zinajitahidi sana kuficha ukweli ili kuonyesha kuwa ukrain wameleta substantial resistance. ila wanabutuliwa mno on the ground. magari yao, vifaru, ndege etc wanapigwa mno hasa usiku wa sasaivi. majengo na miundombinu vinafumuliwa na hii ni mbaya kwa maendeleo yao.
 
Na wanavyohold na Russia nae anaumia kwa kukutana na vikwazo vipya ambavyo ni vibaya sana kwa raia wake. Kama hivi vya leo vi3 ni mwiba kwa Russia.
Raia wake Roman Abr tajiri wa chelsea tayari vita inamuumiza.
Uwekezaji wa wana russia uliopo nje ya russia upo mashakani
Hawana access na fedha kubwa nne zenye nguvu. N.k nk
Kufungiwa SWIFT ndo kabisa itamuumiza
 
Leta na group za Russia vile Putin anavyohangaika kuwadhibit wanaoandamana kupinga vita pia,wao wanasemaje au unadhani Wananchi wa Russia wote wanafurahia kinachoendela kwa sasa?
toka dunia imeumbwa hakuna kinachokubaliwa na.wote wala kinachopingwa na wote
 
Wakishamdaka huyo kibaraka rais mwizi wa Ukraine wamsafirishe hadi Moscow wakamuhukumu huko ikiwezekana anyongwe hadharani kwa makosa ya

Kuwageuza raia ngao za vita kinyume na sheria za kimataifa

Kuibia nchi yake zaidi ya dola bilioni 5

Kusababisha vita vya Ukraine kwasababu ya ushenzi wake

Kutaka kuiuza Ukraine kwa mabeberu kwa kisingizio cha Nato

Kuipaka matope Russia na kuuchafua ujamaa kimataifa

Mimi naona hata wakimtia viboko live itakua ni fundisho kwa wanazi wengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…