LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
kitendo cha RUSSIA kuingia vitani tu ilikua lazima akutane na hayo anayokutana nayo sababu pale hakuenda harusini MKUU
 
Reactions: Tsh
Jamaa kakupa hasira sana ila uhalisia ndo huo. Amesimama na Eukraine mpaka mwisho.
 
marekani hadi kumkamata tu sadam alitumia wiki tatu. kule afghan hadi wameondoa wanajeshi na taliban wakabeba nchi. unajua kilichotokea kule kwa wenye vimacho vidogo.
Marekani anatokea wapi tena Mkuu,hapa tunarejea tambo za Pro Russia siku chache kabla ya vita kuanza, tuliambiwa hapa vita haitochukua hata msaa 24.
 
Na wanavyohold na Russia nae anakutana na vikwazo vipya ambavyo ni vibaya sana kwa raia wake. Kama hivi vya leo vi3 ni mwiba kwa Russia
kusolve issue ya vikwazo ni raisi zaidi kuliko kusolve ujenzi wa nchi iliyofanywa magofu. Russia hapo akitoka, jua yeye pia ni superpower, akiamua kujizila akaamua kusapoti ikijeshi na kwa nuke maadui wa magharibi kama iran tu na north korea, wataomba poo manake west wataona anataka kuimarisha maadui zao wakubwa, watarudi mezani na kuyamaliza. hivyo vikwazo vinawekwa kwa ajili ya aibu tu kwamba west wamesikia kilio cha comedian jana aliposema wamagaribi aliotegemea watamsaidia wote wamemwacha peke yake, sasa wafanyeje? wajifanye kuweka vikwazo tu. china ipo kimya, india ipo kimya, asia yote ipo kimya, china anahitaji sana gas na mafuta, hivyo russia hawezi kosa soko, so is india. ila russsia akikata bomba la gas ujerumani watatumia kuni kupikia kama enzi za ujima, na vinu vyao vya nukes vitakosa nguvu na umeme utakata. russia amehesabu gharama san akuamua kufanya alichokifanya. mimi siku zote nipo upande wa capitalism na huwa sipendi communism kwasababu walikuwa atheists, lakini kwa hili najua russia atashinda. na kwa utabiri uliopo kwenye Bible, inaonyesha russia hawezi kufa, kwasababu ndio jeshi la mashariki la al magedon na gogu wa magogu litakaloshuka kupitia black sea/caspian sea kuishambulia israel hapo baadaye na Mungu mwenyewe ataashuka na kuwahukumu kwa kuwaangamiza 2/3 ya majeshi yake. njia ipo nyeupe kwa urusi sasaivi kupigia Krimea na uturuki ambao sio maadui wake, ni marafiki na watampa njia kwasababu turkey hawaipendi israel kwasababu ya mzozo wa palestina waislam wenzao, na unabii kibiblia unaonekana wazi. kama hujampokea Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako fanya hima, kuja kwake ku karibu. na hapo ndio utajua kuwa Biblia ndio kitabu pekee cha Mungu, vingine vyote magazeti tu ya waongo.
 
toka dunia imeumbwa hakuna kinachokubaliwa na.wote wala kinachopingwa na wote
kumbe basi kama ni hivyo basi pande zote kuna wanaopinga pia,iwe Ukraine or Russia,nilimuuliza mtoa comment maana naona kajikita kutuletea tu negative issues za Ukraine kana kwamba kule Russia wao wote wanakubaliana na kinachoendelea.
 
Vikwazo vya kiwango hicho vina matatizo sana kwa nchi. Esp kwa nchi kubwa kama Russia. Closed economy kwa nchi ambayo ina uwezo mkubwa wa kuexport ni hatari sana. Hapo anatakiwa aombe China asimsaliti.
 
Vikwazo vya kiwango hicho vina matatizo sana kwa nchi. Esp kwa nchi kubwa kama Russia. Closed economy kwa nchi ambayo ina uwezo mkubwa wa kuexport ni hatari sana. Hapo anatakiwa aombe China asimsaliti.
Russia itakuwa closed west tu, ila east bado ni open. na ukifunga mlango kwa magharibi jua east kwa wachina na wahindi kupo wazi. pia jua russia ana silaha nyingi, watu watajipeleka wenyewe kwake kupata silaha. ukiwa na kitu unawezafanya jeuri yeyote mkuu. pia, as long as still una k kitu kidogo mkononi sio kwamba hauna kabisa, unayo nafasi kujipanga wakati wa vikwazo, either kufanya retaliation ili adui yako alegeze kwa kusapoti maadui zake n.k, na yote yanawezekana. kwani unafikiri siku zote west huwa wanampenda russia? siku zote wanatamani afe kabisa ili marekani tu na ulaya wabaki superpower, wangekuwa na uwezo huo wangeshammaliza zamani sana. nakuhakikishia kwa vikwazo hivi wataumia muda mchache lakini sio muda wote. pia kama vikwazo vinafanya kazi siku zote Iran sasaivi ingekuwa somalia.
 
Mkuu sote tunaangalia hizo channel,lakini unapenda kutafsiri vile wewe unataka iwe,ila kama ni unaangalia aljazeera au France 24,hapana aisee
 
Mkuu sote tunaangalia hizo channel,lakini unapenda kutafsiri vile wewe unataka iwe,ila kama ni unaangalia aljazeera au France 24,hapana aisee
france24 wapo biased mno, al jazeera wapo biased pia. wanachagua habari za kuonyesha, ngoja tuone wiki mbili ziishe ndio tutaongea mengine, ila ukweli ni kwamba wanaitesa tu ukrain, vita haina faida hasa ikipiganwa kwenye viunga vya nyumba yako. hata ikiisha huwezi kuwa mshindi.
 
Unateseka na nchi ya watu.
Halafu mbona ccm mnaogopa sana beberu lkn mkipewa misaada mnawalamba miguu?
 
Wakishamdaka huyo kibaraka rais mwizi wa Ukraine wamsafirishe hadi Moscow wakamuhukumu huko ikiwezekana anyongwe hadharani kwa makosa ya kuwageuza raia ngao za vita kinyume na sheria za kimataifa...
hawawezi kumwacha hai, tatizo lake yeye anafikiri yupo kwenye comedy, marekani wamemshauri akimbie, yeye ameamua kubaki ati awe shujaa, shujaa asiyetumia akili hata vizazi vijavyo vitakuja kusema jamaa alikuwa shujaa mjinga. hivi unaweza kuwa shujaa unajirusha kwenye mdomo wa simba ati hata ukitafunwa utajulikana umekufa kishujaaa? si umburura huo?
 
Russia itakuwa closed west tu, ila east bado ni open. na ukifunga mlango kwa magharibi jua east kwa wachina na wahindi kupo wazi. pia jua russia ana silaha nyingi, watu watajipeleka wenyewe kwake kupata silaha...
EXPORTSThe top exports of Russia are Crude Petroleum ($123B), Refined Petroleum ($66.2B), Petroleum Gas ($26.3B), Coal Briquettes ($17.6B), and Wheat ($8.14B), exporting mostly to China ($58.1B), Netherlands ($41.7B), Belarus ($20.5B), Germany ($18.9B), and Italy ($16.7B).

China hapo ndo anategemewa na Russia angalau kupigana na hivi vikwazo. Akibadilika tu He is in trouble. A very big one. Tayari yupo in trouble ila China akimsaliti he is in big big big so big trouble.
 
Mkuu sote tunaangalia hizo channel,lakini unapenda kutafsiri vile wewe unataka iwe,ila kama ni unaangalia aljazeera au France 24,hapana aisee
Naangalia Aljazeera sana na BBC kidogo hata sasa ni saa tisa kasoro ndicho ninachofanya. Huyu mshkaji inavyoonekana haipendi USA. Sasa inasababisha aichukie Eukraine na raisi wake.
 
Belarus ndiko putin anatumia kama stuli ya kusimama kutungua pia, china hana shida, shita ni nchi tatu tu, Uholanzi, italy and germany ambao unaona asilimia zao ni za chini, lakini hata kama ni za chini wanawategemea mno ndio maana wamesuasua hata kwenye kuweka vikwazo, ni leo tu ujerumani imetangaza kutoa silaha na kuweka vikwazo baada ya kulaumiwa mno na wanauro wenzake. ila anafanya hivo akiwa muoga kwasababu anajua sio muda yeye pia ataumia urusi ikiamua kufanya yake.

maumivu urusi sio kwamba hatayapata kabisa, wakipiga swift ataumia sana ila hatakufa na atasimama tena, wakati nchi yake sio magofu kama itakavyokuwa ukrain. ukrain hata bila vikwazo tayari ameshaumia kwasababu ataanza kukusanya matofali ya majengo yaliyosambartishwa na kuanza ujenzi upya kwenye maendeleo aliyotumia muda mrefu kuyajenga.

ndio maana hata kwa maisha ya kawaida, ukiona unaendela brand new MBW acha kushindana na toyo au bajaj, mkikwanguana itakuletea usumbufu tu utakayeumia ni wewe uliyejenga kitu cha thamanu mda mrefu ukakwanguliwa na mtu ambaye haumii kama wewe.
 
Ndugu yangu. Eukraine baada ya kupigwa atasaidiwa kuinuka. Hata sasa bajeti kubwa sana imeshapitishwa kwa ajili yake. Hii ni endapo Russia ataachana na vita.

Jambo lingine ambalo Russia ana kazi kubwa kama hataachana na vita ni kubaki pale Eukraine akisimika utawala wake utakaomtii yeye bila kelele kutoka ndani na nje na bila machafuko ya waasi masalia huku akipambana na vikwazo na kuwatuliza raia wake ambao wanaumia na vikwazo.
 
Naangalia Aljazeera sana na BBC kidogo hata sasa ni saa tisa kasoro ndicho ninachofanya. Huyu mshkaji inavyoonekana haipendi USA. Sasa inasababisha aichukie Eukraine na raisi wake.
trust me, naipenda USA, nimeshafika USA na mimi nimefaidika sana na wamagaribi, lakini nawafahamu walivyo, namna wanavyopenda kuwatumia wengine ili wafaidike. na ukrain inatumiwa. huu ndio ukweli. na ukrain inaumia, raia wanaumia bila sababu za msingi. mtu anayekwambia upiganie vita nyumbani kwako atakusaidia, halafu akiona unapigwa anakuletea gari ati kimbia uache nyumba yako magofu, haji kukusaidia, huyo anakutumia. na anatesa familia yako bila sababu. naipenda sana ukrain, kwanza kwasababu mimi ni pro-israel, na kule mfano Odesa kuna wayahudi wengi sana, asilimia kubwa ya wayahudi ukrain wanaishi odesa. ukrain ndio eneo ambao wayahudi walikimbilia kama haven wakati wa holocost, pamoja na maeneo mengine ussr kipindi hicho. juzi pm wa israel aliomba wakati wa vita putin amruhusu kuwachukua wayahudi, na kweli wengi wamekimbilia israel tayari. ila wapo waliobaki wanaumia bila sababu na wanalazimishwa kupigana, fikiria rais anasimama anasema hata vijana kati ya 16 hadi 18 hakuna kutoroka nchi, wabaki wapigane? akili au matope unalazimishwa kupigana? hiki ndio kinanifanya nimwone comedian hana maana.
 
ati atasaidiwa kuinuka? umejenga nyumba yako, umejenga madaraja, umejiimarisha kiuchumi, alafu jirani anakushauri pigana na mtu akiharibu nyumba yako nitakusaidia ujenge nyingine? kumbe anajua nitapigwa, anachotaka kwangu nini sasa? raia watakaokufa watafufuka? wamagaribi wanajua fika kuwa at the end of the day ukrain itashindwa na itakuwa magofu na watampa hela aanze kujenga. raia na wanajeshi waliokufa watafufuka? hadi ujenge miundombinu ni leo? wawekezaji watakaokuwa wamekimbia utawarudisha? watakuwa wana uhakika kuwa russia hatarudi tena soon? unaona namna wamagaribi wanavyomtumia kama condom ukrain ili kutest uwezo wa russia kwa faida yao? do you think this is fair?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…