LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
EU wamesema watatoa fighter jets kwa Ukraine. Huu sasa ujinga kuendeleza mgogoro, hii vita ilibidi iishie kwenye mazungumzo yatakayofanyika ila Westerns wanazidi kutuma silaha. Ukraine hawajui kuendesha ndege yoyote inayotumika na EU members ukiachana na members kama wawili hivi wenye Mig-29 zilizozeeka hazina hata spare parts. Ukraine wanatumia Mig-29 ambazo walirithi baada ya Soviet Union. Sasa hizo ndege za EU nani ataendesha kama sio wao, mbona kama wanalazimisha vita iwe ya Russia vs NATO.

Vita ingeisha mapema kwa mazungumzo
 
wewe jamaa bana kisa kufungwa anga la ULAYA ndio ndege zisipite kweli?
 
Zamu ya Urusi usiku

Videos on social media captured what appears to be a HUGE artillery assault apparently launched by Russian troops

Nimewaona wale wajeda wa Chechen jamaa wanamizuka walikua wanasubiria kwa hamu vita
 
Ona huyu. Kesho njoo hapa na mikono kichwani, Zelensky will not step down. He will not bow down to Putin
 
Kwa hiki kinachoendelea hivi sasa kati ya Ukraine na Russia nadhani lama raisi wa Marekani angekuwa Donald Trump saa hizi Russia ingekuwa imeshafutika kwenye uso wa dunia hii
Unamzungumzia Trump huyu ambae chini ya utawala wake ndege zake za kivita (sio chini ya moja) Meli za kijeshi na kambi zake za kijeshi zilishambuliwa na Iran kule Iraq au Trump yupi? Labda ungesema Bush hapo ningeelewa, maana jamaa anapenda vita kama wazaramo wapendavyo mdundiko.
 
Bado Sana kwa nchi yetu.

Mfano kwa Marekani,ikitokea Jeshi lake lote limeshindwa na adui kaingia ndani ya Marekani kabisa,Serikali haitakuwa hata na kazi ya kuwapa raia bunduki. Litakuwa TANGAZO moja tu kutoka kwa Rais.

'''Kila mwananchi wa Marekani beba bunduki yako toka ndani Pambana na adui"" hapo Adui atakimbia kurudi alikotoka.

Nchini Marekani,Raia wanamiliki Siraha Milioni miatatu (300M). Idadi ya Raia wa Marekani wanaomiliki Siraha ni zaidi ya idadi ya Wanajeshi wote Duniani.
 
UN Security Council votes to convene an emergency special session of the General Assembly on Monday to discuss Russia's operation in Ukraine - this is the first time a move like this happened since 1982.

RT
Chairman wa UNSC ni Russia na sasa balozi wake nadhani anamaliza muda wake kesho. Kuna uwezekano Russia ikaondolewa kwenye UNSC
 
Nimerudi.
Kuelewana tunaelewana na pia tukubaliane kuwa, Ukraine anastahili heshima. Pamoja na hayo matatizo yaliyomkuta ila na yeye kamuingiza kwenye matatizo makubwa kaka yake Russia mpaka akasema washeni nuclear. Si tunakubaliana?😀😃😃
 
Angepiga tu kelele kama kwa korea kaskazin
Trump mwenyewe chini ya utawala wake meli zao ngapi zilishambuliwa na Iran na hakuingia vitani, hapo sijataja zile ndege zao zisizokuwa na rubani zilivyolipuliwa mchana kweupe na Iran pia zile kambi zao za jeshi zilizoshambuliwa na Iran kule Iraq hadi kusababisha vifo na majeruhi kibao wa jeshi. Angalau jamaa angemzungumzia Bush hapo ningemuelewa.
 
Upumbavu ni wa Ukraine... Kafanywa kuwa uwanja wa vita yeye anahisi anasaidiwa..?? ww jiulize hizo jets atashambuliwa ndani ya Urusi ama nchini mwake
 
Trump ni muelewa na sio mgomvi, always anatafuta suluhu. Kama aliweza kukaa meza moja na KIM, huyu Putin ingekuwa rahisi zaidi. TRUMP alifanikisha hata NORTH na SOUTH Korea kukaa meza moja zaidi ya mara moja.
 
EU na NATO wameshamuona PUTIN kateleza kwahiyo hapa hapa ndio pakummaliza. Putin aliingia vinginene kakutana nahali nyingine, alinua eazy tu anapiga anafukuza raisi anaweka wake, hakwenda kwa total war, akawa anajitahkdi kukwepa kuumiza raia, akajua akikamata viwanja vya ndege, akipiga maghala ya siraha na sekta muhimu tayari kawanyong'onyesha, mambo yamekuwa magumu, hapa ni aidha ajitoe akili apigane total war au akubali kuvuka nguo kitu ambacho sidhani atakubali. sasa kitu kibaya kwamba na raia nao wakuwa wajeda wasaidizi, haoa ndio pagumu.

Marekani hii situation alikuwa anaitaka kwa hali na mali, kote kwake faida urusi akiingia hata akishinda anakula vikwazo si mchezo, wakati huo yeye na washirika wake wanatoa msaada kimya kimya ili kuzidi kumnyong'onyesha mrusi.. Toka awali nilihisi ukraine bila kufanya maamuzi sahihi nchi yao ndio itakuwa uwanja wa vita, watu watakuja kutestia mitambo yao hapo.

Putin hali tete, akichomoka hapa ndio nitajua huyu kichwa.

Nimejifunza vitu viwili, Dunia bila unafiki haiendi mmarekani mtu mbaya sana, ukiwa na pesa hata ukiwa na sura kama ya nani utaambiwa we ni handsome, alichokifanya putin MMAREKANI kaishakitenda mara zisizo na idadi ila wapi, sasa putini kajitela, ananuka ubaya tu.
 
Chairman wa UNSC ni Russia na sasa balozi wake nadhani anamaliza muda wake kesho. Kuna uwezekano Russia ikaondolewa kwenye UNSC
Uwezekano wa Urusi kuondolewa uanachama wa UNSC hivihivi si rahisi.

Labda Baraza Kuu lifanye mabadiliko ya UN Charter kwanza, maana hakuna kifungu chochote kilichoweka utaratibu wa kuiondolea nchi uanachama wa kudumu. Hata hivyo, Urusi itapinga uidhinishwaji wa hayo mabadiliko kwa veto.
 
Acha kudanganya watu mtu mzima kiwa uko upande gani ivyo vikwazo tangu mwanzo hawasikii kwani

Unachoshindwa kuelewa ni ivi hii ni operation vya kijeshi ishu iliopo raisi wa ukraine ametengeneza mazingira kuingiza wananchi mkenge maana yeye anajua ndio anatafutwa na familia yake ndo watakuwa hatarini ndo hapo anajitia uzalendo wa kutorudi nyuma hata mazungumko hataki anajua ni mtego

Unadhani russia wanatetemka ngoma nzito bado wanachofanya ni kusambaza propaganda wala russia hatumii nguvu kama mnavyodai anaenda kwa target asilete maafa makubwa kama unabisha hao USA wadeclare vita uone hao wakina lil waume hutowasikia tena patakuwa majivu nchi nzima the same kwa russia itakuwa hali mbaya

Wabongo Mnakuwa nyuma kwa vile hamjui uhalisia ni kushabikia kisa wewe mkristo ndo unajifanya unamjua mmarekani na UN mara hawa wako palestine kisa ni waislamu

Hyo sio vita ni operation kama ya USA kumtoa Gaddaf kule libya na wakafanikisha

Sasa kama una akili je huyo Russia yuko sahihi kwa hali iyo au una akili za kufuatilia season tu tumia akili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…