LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Tunajua Ukraine yupo vizuri na hii yote ni baada ya USA kumjenga kijeshi kwa mda mwingi ila akumbuke tu Urusi sio level yake. Amuulize vaba yake USA na mama yake NATO achana na dada zake Poland na UK na Ufaransa
 
Kumbe hujui historia ya Putin vizuri

Jamaa Alikuwa KGB mzuri SANA na lipelekwa Station ya German na kule hawatamsahau maana aliwatandika sawa SAWA
Hata mimi nilikuwa naamini hiyo stori hiyo unayosema lakini ni ya juu juu sana iliyokuzwa baada ya yeye kuwa rais. Ni kweli alipitia mfunzo ya KGB na kwa kipindi fulani alikuwa askari wa KGB lakini hakuaminiwa kufanya kazi sensitive za u-spy kwa vile alionekana alikuwa na mapungufu makubwa katika maamuzi yake; kwa hiyo akabaki askari wa kawaida mwenye uniform ndani ya KGB. Ingawa alionekana kuwa ni mtu msiri sana, ambayo ilikuwa sifa nzuri klwa spy, lakini pia alionekana kutokuwa sensitive na hatari, jambo ambalo waliona siyo zuri kwa spy wa KGB. Kwa hiyo hakuwahi kuwa na assignement zozote za u-spy, na akabaki ni uniformed military officer ndani ya KGB. Kuna vitabu kama viwili vinaweka biography yake sawasawa na yeye mwenyewe akiithibitisha.
 
3 days ago nilisema hivi kuhusu Russian army hasa. Kumbe nilikosea, uwezo niliodhani wanao kwenye hii comment bado ni mkubwa.

Sasa ninaamini jeshi la ardhini na la anga vyote ni tia maji tia maji, hakuna jeshi serious pale. Russia mpaka sasa hawajashambulia jeshi la anga la Ukraine na kulimaliza, CNN na news outlet nyingine reliable imesema Ukrainian Airforce iko intact bado, hawajaharibu airbases hata. For comparison mwaka 1967 Israel ilifanya shambulizi kwa usiku mmoja na kufly sorties tatu tu ikaharibu ndege zaidi ya 200 za Egypt na kuweka craters kwenye airbases zao zikawa hazitumiki tena.

Bado kwenye counter drone technology Russia hawajaonesha makali. Sikuamini kuona eti Russia watu ambao wamekumbwa na Bayraktar TB2 za Uturuki mara nyingi zaidi kuliko jeshi jngine wangekosa countermeasures mpaka leo wakati walijua watavaimia Ukraine na inazo. Bado hawana electronic countermeasures kama jamming, inaripotiwa wanajeshi wa Urusi wakiona drone angani wanajaa woga. Inaweza kuwa inashambulia, inatambua convoy kupanga ambush mbele au inapata coordinates ili kuita artillery fire.

Russian Airforce haijanishawishi sana. Hawajafanya dogfights kuwaona uwezo wao ila kama wangekuwa na uwezo mkubwa wangefanya precision strikes nyingi zaidi badala yake strikes zimegoma wakategemea cruise missiles kina Kalibr ambazo zimeongeza uharibifu kwa civilian infrastructure. Mazoezi yao kwa kawaida huwa ni machache kuliko NATO, hata India huwa ina mazoezi makali.
Sanasana wanatumia Su-25s ambazo ni ground attack ila MANPADs zilizotolewa kwa wingi zitazisumbua. Su-25 naona uwezo wake wa kuhimili kushambuliwa ni mkubwa. EU imesema ndege zitafika ndani ya lisaa wapewe Ukraine, sijajua walisema ikiwa saa ngapi.

Russia kwenye inventory yake uko kwake ana silaha za maana kazitunza. Huku Ukraine kaja kawaida ila mpaka sasa alipoona mambo magumu ingeshaonekana analeta silaha bora zinafanya kazi kubadili matokeo. Tangu tarehe 24 leo tarehe 28 na ni kuvuka mpaka mmoja tu
 
Urusi kwenye ile charter inatambuliwa kama Soviet Union. Kipingamizi kinaweza kuwa Urusi sio Soviet Union wala hana mamlaka rasmi ya kurithi nafasi hiyo wakati kuna members wengine wengi tu. Ila Russia wataweka veto kama ulivyosema, hata China pia hapa lazima amtetee Urusi
 
kabisa jamaa anatakiwa apeleke moto kwel kwel
 
Ni kweli jamaa yuko overated, sovit haitarudi tena na yeye ndio anacho amini. Siasa za ujamaa na maxism ni upuuzi mtupu, watu wana taka uhuru sio serikali ku control kila kitu
 
Sasa wewe umuwekee urusi kikwazo una nini cha msingi? Tz hatufanyi biashara yoyote na hao jamaa

Sasa dunia ni Tz peke yake?!

Hivi China, India , Brazil, South Africa, Indonesia, Saudia, Argentina, Colombia, Nigeria, Egypt, Mexico,Chile, Peru, Algeria, Korea ,Vietnam,Philippine, Bahrain, Emirates, Qatar,Iran, Pakistan, and so on and so on, umeshazisikia zikiiwekea vikwazo Urusi?! Kwahiyo hizo nchi sio dunia?! Bali dunia ni nchi za magharibi tu?! Au hazina biashara na urusi?! Tuache mahaba ya ajabu!
 
Mbona team zao znacheza UEFA
 
Nili chaguliwaga kwenda urusi ila nilivo fatilia hao washkaji ni wabaguzi balaa yani kuna mitaa mtu mweusi hukatizi

Kwahiyo nchi za magharibi sio wabaguzi????!!!

Ni nchi gani ambazo watu weusi wanauawa kila kukicha kama nchi za magharibi?! Umeshasahu watu weusi wanavyo uawa na police wa marekani kila mwezi?! Hata sasa kuna kesi kibao zinaendelea marekani kwa mauaji ya wa marekani weusi!!

Jana hujaiona video clip ya watu weusi wakizuiwa kupanda treni kule Kiev, Ukraine?! Ubaguzi uko kila mahali tena nchi za magharibi ndio mkubwa zaidi!
 
Hapa ukiwekewa vikwazo nchi za ulaya magharibi huchomoki, zina miliki uchumi wa dunia. Ivi ulisha jiuliza thamani ya pesa inatoka wapi?
 
Hapa ukiwekewa vikwazo nchi za ulaya magharibi huchomoki, zina miliki uchumi wa dunia. Ivi ulisha jiuliza thamani ya pesa inatoka wapi?
The actual price ya pesa ni gold, marekani ana gold reserve mara tatu ya nnchi zote duniani combined
 
Ndio maana Nuklia haitakiwi kumilikiwa na vichaa, hayo ndio madhara yake..

USA kapigana vita nyingi miaka mingi hajawahi kuzungumzia nuklia kabisa, sasa huyu na kaukraine tu tayari anazungumzia Nuklia..
Nagasaki's na Hiroshima ilikuwa aina gani ya bomb walitupiwa na USA ?
 
Kama uchumi unapigana WAAMBIE USA AKAIVAMIE CHINA, SI WANA UCHUMI MKUBWA KISHINDA CHINA?? HUNA AKILI KICHWANI
China wanapiga Sana kung fu jet lee na Don watamaliza USA
 
wewe jamaa umekuaje[emoji848][emoji848][emoji848]
au kuna mtu kakuibia simu yako nini?
Russia yuko UN Security Council kama permanent member ila ile nafasi ni ya Soviet Union. Russia sio Soviet Union, aliipata ile nafasi kama successor wa USSR. Sasa ikiletwa hoja kwamba ni vigezo gani kwenye UN vinatambua successor anatakiwa arithi kiti, na ni vigezo gani walitumia kusema Russia ndio mrithi wa Soviet Union.

Options zinaweza kuwa:
1. Kwa nini mrithi awe Russia na asiwe Ukraine au member yeyote wa zamani, kigezo cha kukataa asiwe Ukraine kwa nini kisiwe kigezo cha kukataa asiwe Russia.
2. Kwa nini tusitafute permanent member mwingine kwa sababu basically, USSR ceased to exist.

Kwenye documents na makabrasha ya UNSC kwa sababu ni permanent members hata dosc hazibadiliki, unakuta walipoandika USSR wanaipa Russia juu kwa juu.

Msidhani haiwezekani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…