Emen
JF-Expert Member
- Jun 22, 2021
- 2,069
- 3,516
Tatizo hawa Euro na west kwa ujumla sitaki kutumia neno unafiki ila kuna kitu wao wanadhani wao ni superior kimawazo kuliko watu wengine wote na wamestaarabika kuliko watu wote hapa ndio tatizo. Maisha yao ni ghali kuliko maisha ya wengine na lazima waungwe mkono hata zile tasisi ambazo kwa miaka hawakutia siasa katika michezo kama FIFA na OIC wamewashurutisha mpaka wamachagua upande. Mtu yoyote akienda kinyume na mawazo yao huyo mbaya wanahubiri democracy lakini ni hawa hawa wakati Hamasi wameshinda vote wakaleteta fitna wakatolewa hapo Egypt alishinda uchaguzi Morsi yaliyotokea tunajuwa. Ok ni kweli Hamasi ni wabaya hilo halina ubishi lakini si wamepigiwa kura? Morsi alishinda lakini kwa kuwa hakubaliki na wao wakamtoa na mwisho kufa. Kama ndio hii safari tumeanza kama yake ya Bush either uko na sisi au na wao hakuna netral ndio tunaambiwa. Uhuru wa kuongea ndio nyimbo zao leo hii wanafunga media mpaka internet ili watu wasiongee. Nadhani uhuru wanaohubiri ni ule wanaoutaka wao kutaka mila zao lazima tuzikubali maana wao ndio civilized sisi wengine mapaka tu hatuna ustaarabu. Hakuna sehemu walitia mguu kukawa na mafanikio sio Libya, Iraq hata Syria wameacha majanga kwa watu.
“Civilized”