LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
On the evening of March 5, the Russian armed forces hit 61 military infrastructure facilities of the Ukrainian troops with a massive strike, the Russian Defense Ministry said.

 
Hapo ndipo unajitekenya na kucheka mwenyewe, unaizungumzia air defense ya Ukraine bila kujua ni mfumo wa warusi . Hapo unakubaliana nami na kila mtu kwamba Russia ana silaha bora sana za mfumo wa ulinzi wa anga. Unajua kwa nini Russia ilipoingia Ukraine kazi yake kubwa ya kwanza ilikuwa ni kuiharibu mifumo hiyo? Russia anaijua hiyo mifumo kwa sababu ni yake na ipo strong sana
 
Kwanza huyo Putin hajawa vocal kama unavyotaka kutuaminisha hapa, actually West ndio wameongea mapovu tangu mwanzo and the man is quiet, hata haongei ovyo kama vibaraka wa mabeberu na hao mabeberu.

Kama air defence force ya Ukraine ingekuwa na nguvu, Russia asingeweza kuingia na kushambulia pamoja na kuteka miji tofauti huko Ukraine, air defence force ingekuwa imara hizo nuke zisingetekwa, kumbuka katika nuke tatu, mbili tayari zipo under Russia control, na hiyo moja iliyobaki haina mda itakuwa chini yao, hiyo air defence unafanya kazi gani hadi Russian forces ziingie jikoni, are you nuts?

Acha kutuletea propaganda za BBC na CNN hapa.
 
Aliyekuambiwa Ukraine kuna vita nani, Ukraine kuna operation tu ya kijeshi tu, naweza kusema ni operation ndogo sana. Ulishawahi kuona vitani pande zote wanaomba kusimamisha mapigano kwa ajili ya jambo jingine?
Eti operation ndogo tu,ingekuwa hivyo basi hiyo panic yote pale Kremlin isingekuwepo.
 
Mzee hapa unaongea na mazezeta yamekuzwa na vyakula vya makopo. Genes nyingi kwenye miili yao zimeharibiwa.
 
Actions in support of the Russian military special operation in Ukraine continue throughout the country.

Drivers put Z's on their cars and run car races. Today they drove through the streets of several cities, including Novosibirsk, Yekaterinburg, Irkutsk, Vladivostok.
Your browser is not able to display this video.
 
URUSI HAITAKAA IWEZE KUICHUKUA UKRAINE IWE SEHEMU YAKE, HATA IPAMBANE MIAKA MILIONI.
HIZO NI NDOTO NYEVU TU ZA PUTIN.
 
hii threads sasa imejaa ngonjera nyingi na mipasho badala ya mjadala kuhusu mgogoro wenyewe
 
URUSI HAITAKAA IWEZE KUICHUKUA UKRAINE IWE SEHEMU YAKE, HATA IPAMBANE MIAKA MILIONI.
HIZO NI NDOTO NYEVU TU ZA PUTIN.
Nimesema ratizo vijana wengi mmekuzwa na maziwa ya makopo. Nutrients nyingi mmezikosa kwenye miili yenu. Uwezo wenu wa kuchanganua mambo ni mfinyu mno.

Kwanza lengo la Putin siyo kuchukua Ukraine.
Pili unavyoandika kwa herufi kubwa ni kigezo tosha kwamba kichwa chako hakiko sawa.
 
Instagram zipo clip za kutosha za hao marubani wanakamatwa kama kondoo,tena wengine walikuwa kwa ile operation ya Syria,Ukraine wanakuonyesha clip ya rubani na wanaambatanisha na picha yake akiwa Syria na kina Assad,wale wa kusema ni propaganda za Ukraine wamebaki kimyaa,maana wanawekewa na proof hapo hapo za hao Marubani wa Russia.
 
Kanuni ya vita ni Man 2 Man!

Wanachokifanya Ukraine baada ya kukimbia kambi wameamua kujimix na raia so wanapiga kwa kuvizia. Ni sawa na ulingo wa boxing unapigana na mpinzani wako kwa kujificha mgongoni kwa refa. Unashambulia akirudisha unajificha nyuma ya refa.

Wa Ukraine wanatumia raia kama Kinga kujificha kwenye mgongo wa raia. Putin kashawaambia waache utoto huo wa kujificha kwenye migongo ya raia waone show.
 
Wa Ukraine hilo hawataki ila kitakachofata Putin ataamuru tu kwa muda aliotoa umetosha kwa watu ku evacuate kama kuna waliobakia ata assume ni waasi!

Paper two sasa itakuwa ya kukata na shoka😅
 
hii threads sasa imejaa ngonjera nyingi na mipasho badala ya mjadala kuhusu mgogoro wenyewe
Inabidi twende hivyo hivyo baada ya Pro Putin kutaka kuiteka thread hii na propaganda zao nyingi kutoka RT,wamehama kwenye mada yenyewe wameamua kuwa mareporter wa Kremlin.
 
Uko sahihi Urusi akilazimisha kuweka kibaraka wake Ukraine itakuwa machafuko matupu na nchi isiyotawalika. Watu wa Ukraine wamejulikana kama watu wabishi na wa mapambano karne zote, hawatakubali kuwa watumwa wa Urusi bila kupambana kufa na kupona kwa miaka mingi.
 
Alisema anaenda Ukraine kuuondoa utawala wa Kinazi na kufanya "peace keeping mission "ila alipofika Ukraine hakupokelewa hata na raia mmoja wa kawaida na ua mkononi kumkarubisha na kumshukuru kuja kuwaondoa hao wanazi, Kinyume chake raia wa kawaida wamebeba silaha kuungana na rais wao Zelenskyy na wengine wameyakimbia majeshi ya Urusi.
 
Ukraine ni taifa la kale zaidi kabla ya Russia.
Kyiv ilikuwa jiji kubwa muda mrefu sana wakati Moscow ikiwa kijiji tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…