Kwa kujazia tu japo swali siyo langu! Russia hasingeweza peleka drones kherson kwasabu hizo drones ni kwa ajili ya stationary targets kwenye targets ambazo zinatembea hazina ufanisi wowote! Maana wanajaza Co_ordinates za targets kabala haijaondoka.
Pili: kuhusu Siraha za kupiga Moscow, nafikiri sababu ni kuu mbili. Kwanza lengo namba moja la aliyevamiwa ni kumwondoa adui kwenye aridhi yako; Rejea vita yetu na Amini, majeshi yetu hayakuigusa Uganda hapo mwanzo maana lengo mama lilkuwa ni kumtoa mvamizi kwenye nchi yetu lengo hili lilipotimia ikaonekana Amini bila kutoka madarakana atajipanga na kutuvamia tena ikabidi sasa tumfuate huko huko kwake. Kwa mantiki hiyo hata Ukraine lengo mama hajalifanikisha bado, lengo ni kumrudisha mvamizi kwake.
Sababu ya Pili: Uwezo wa kijeshi wa Russia; kwa sasa Russia anapigana Kama aliyevamia nchi ya watu kwahiyo kuna hatua anakosa haki za kisheria na kimedani kuzichukua maana yeye ndiye mchokozi hajachokozwa. Kwa maana hii ukimshambulia kwake atakuwa na haki kujitetea kwa nguvu zake zote maana umemfuata kwake. Hili West wanalijua na Uwezo wa Russia wa kujitetea wanaufahamu ndiyo maana hawawezi mruhusu Zelensky kushambulia Moscow mpaka pale wajilizishe kwamba Russia amewekwa kwenye kibano kiasi kwamba hawezi furukuta kwa maguvu yake. Mwisho: wakati USA anaanza kumsaidia Ukraine Biden alisema" Tambueni kwamba tunapambana na Moja ya Majeshi bora Ulimwenguni kwahiyo akili na maarifa ni muhimu kuliko jambo lolote"