Hapo ni sawa useme Toyota Harrier na Land Cruiser LC 200 (V8) hazina utofauti sana kisa zote ni SUV.
Unachokisema kuhusu ubora wa rubani ni sawa kabisa ndio maana Marekani marubani wake wana average flight hours kubwa duniani. Huwa nasema ndege ni kama gari, ukimchukua dereva wa daladala ukashika Nissan Civilian naye akashika hiyo mkashindana atakupoteza vibaya mno. Ndege inahitaji mafunzo na uzoefu mkubwa. Hivyo hoja ya mafunzo tunaipiga chini kwa kuwa huwezi nitajia nchi yenye mafunzo ya marubani kuizidi Marekani, labda ifuatiwe na Israel.
Mafunzo ya rubani yanahusisha na simulators. Microsoft ndio mabingwa wa kutengeneza flight simulators, bado kuna makampuni mengi Marekani pale. Simulation inakuwa kila kitu sawa na ndege: mitikisiko, mizunguko, kelele, cockpit, G force na kila kitu sawa na ndege. Marubani wanakaa sana kwenye latest generation simulators na bado wanakuwa na flight hours nyingi zaidi. Sasa njoo kwetu sisi, simulators naamini hatuna na bado jet zetu zikiruka huwa najiuliza kuna nini tena. Mimi ni plane spotter, nishagundua F-6 zikiruka mara nyingine kunakuwa na tukio la kiserikali. Mara ya mwisho jet zetu zinaruka hapa Dar es Salaam ni siku mbili kabla Jenerali Mabeyo hajastaafu. Hazijaruka tena
Kufundisha rubani ni muda na gharama. Airframe inachoka kadri inavyoendeshwa. Bado kuna operation cost nyingine kama mafuta na malipo ya training.
Muulize Captain akupe best performing fighters. Akupe kill to loss ratio, mfano nakupa ya F-15 Eagle ni 104 to 0. Imeua ndege 104 kwenye aerial battles na haijawahi dondoshwa na ndege ya adui. Hapo ni kwa sababu Marekani ana kila kitu kinachohitajika. Mambo ni mengi sana hatutayamaliza kuandika.
Uwezo binafsi wa ndege ni muhimu sana. Mfano Chinese J-10D ni 4th generation ya kawaida kwa superpowers, ukiikutanisha na hizi Chinese F-6 zetu ni kwamba J-10D inakuona ukiwa zaidi ya kilomita 100 angani na AESA radar yake. Huwezi iona kabla, inaweza engage zaidi ya ndege 6 wakati mmoja wakati hizi F-6 sina uhakika kama kwanza zina uwezo wa beyond visual range (BVR). J-10D moja ikiwa packed to the teeth inaweza poteza F-6 sita zikiwa hazijui kama kuna adui. Kwanza hazina missile warning system, zina PESA radar, hazina shoot and forget, zina radar cross section kubwa.
Dunia inaelekea kuachana na dogfights ambazo ndio hutegemea zaidi uwezo mkubwa wa rubani. Niko na Shenyang J-16 ya Mchina ina PL-15 long range air to air missile uniletee ujinga wakati kombora langu linaweza piga ndege iko hata kilomita 180. Niko na Dassault Rafale ya Mfaransa ikiwa na MBDA Meteor inaweza kukupiga kilomita 150 sasa yanini nikusogelee tutumie cannon kupimana nguvu. Na bado long range missiles zikifeli kuna range za 60km au 30km