Bome-e
JF-Expert Member
- Jan 3, 2014
- 17,662
- 27,112
Je,bila msaada anaopewa Ukraine kuanzia silaha, intelejensia,pesa ya kuendeshea vita,mafunzo na misaada mingine ya kibinadamu,Je,Ukraine ingekuwa imesimama mpaka Leo?Jibu Hilo swali kutoka moyoni mwako na usiendeshwe na hisia na mahaba!Tumeona pia mercenaries wengi kutoka US,UK na nchi mbalimbali wakiwa battle field hapo Ukraine!Mkuu je una mashaka kwamba jeshi la Urusi lingeshapigwa kabisa kama lingepambana na vikosi vya NATO yenyewe? Kwa sasa tunaona tu jinsi gani jeshi kubwa la Urusi linajitahidi kushika mita chache hapa na pale dhidi ya jeshi la ukraine ambalo ni ndogo zaidi. Pia jeshi la Ukraine kimsingi hutumia silaha za kale za kisovyeti, pamoja na mifumo kadhaa ya silaha za kisasa kutoka NATO. Lakini bila askari au vikosi vya NATO, na bila kupewa silaha bora za NATO.
Kabla ya uvamizi watu wote waliamini Urusi ina jeshi la kutisha likiwa ni jeshi lenye uwezo mkubwa. Imani hiyo imepotea.
Ndiyo, nchi za NATO zinasaidia Urusi lakini hazipigi Urusi. Hata wanatuma pesa nyingi Urusi kwa kununua mafuta na gesi yake hadi leo. Na Urusi inawauzia mafuta wanayohitaji kuendesha viwanda vyao, pamoja na viwanda vya kuzalisha silaha zinazotumwa Ukraine.
Unaweza kusema ni ajabu, au kichaa, ila hivyo ndivyo dunia yetu.
Ila nchi za NATO hazikuanza kupiga Urusi. Hali ingekuwa tofauti sana.
Na tukumbuke nani alianza kushambulia maeneo ya nchi nyingine.
Huwezi kudharau uwezo wa Russia kivita eti kisa ukraine mpaka Sasa imesimama,lazima utambue pia na msaada anaopatiwa Ukraine ndio umesababisha iendelee kusimama mpaka Sasa!
Hebu tueleze US na washirika wake walitumia muda gani huko Iraq,Afghan,Vietnam ambako hawakuwa na advanced weapons!
Halafu Usisahau hiyo ni SMO tu,sio vita kamili!
Ingekuwa vita kamili,Russia angefanya mashambulizi ya anga Kwa kila kilichosimama!