LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Propaganda ni hii ya kwako hapa mkuu, umeandika unavyotaka, report za kwanza zinasema 12,000 lakini nyengine za UN wamekadiria 3000 hadi 6000, kwa ufupi elewa russia wana kibarua kigumu ukrain na wewe changanya na zako, hii hapa chini ni mifano na hali halisi ya hii vita

View attachment 2147794View attachment 2147798
Nipo pamoja na wewe, hakuna mwanajeshi wa Ukraine amekufa. Russia wana hali mbaya sana.
 
Hapana mkuu, Russia wanakwenda na plans wana AB na C

Plan A iliishamalizwa na sasa wapo kwenye plan B ambayo ni kuizunguruka kabisa Kyiv yote na asitoke hata panya, na ndo maana raia wote waliambiwa waondoke.

Plan C ni kuhakikisha mji warejea katika hali yake yaani umeme, askari wa Russia mitaani na kutangazwa raisi mpya.
Mwamba inaonekana walikushilikisha kwenye plans zao[emoji16]
 
Duh hizi data sijui umeztolea wapi...

2021 Russia World Rank by GDP ni ya 11....

Sasa hyo 91 umeitolea wapi na ata kama ni GDP per Capita haijafika uko... Nia ya 64 data zingine zinaonesha 57... Ila cha kunote ni kua GDP per Capita huathiriwa na Idadi ya watu...

Mfano USA ndo anaongoza kwa GDP Nominal kwa 19.8Trillion Dollar's ila inapokuja kwa GDP per capital kaachwa mbali na mataifa ambayo kwe sura ya Dunia kwa walio wengi yanachukuliwa poa...

Mfano anayeongoza list ya GDP per capita ni Singapore, kuna Luxembourg, kuna Qatar kuna Macao... Je hao Uchumi wao wanamzidi Mmarekan?

So per Capita n wastan wa kichwa kimoja kimoja sio wastan wa Nchi husika.

Pitia link hyo ukaongezee GDP by Country - Worldometer
Asante, kuhusu GDP pekee unasema kweli, hapa Urusi ni nafasi ya 11 duniani (kwa sasa, tuone mwaka ujao baada ya vikwazo walivyojipatia). Ila hii ni pamoja na biashara ya gesi na mafuta, inayoweza kucheza sana (nimeona ni asilimia 60% ya GDP).
Upande wa Pato la Taifa GDP kwa kila raia unasema kweli pia, nchi ndogo ziko juu. lakini linganisha chanzo hiki (inaunganisha data za IMF, Benki ya Dunia na UM) utaona Urusi kati ya nafasi 80-85 (nilikosea kuhusu 92, ilikuwa ya zamani), Marekani nafasi ya 6-10, Ufaransa 24-29. Pato kwa raia inasema kidogo kuhusu utajiri halisi ukiangalia ugawaji wa mali ndani ya nchi, ambayo huko Urusi ni kati ya nchi zenye tofauti kubwa sana kati ya matajiri wachache na maskini wengi (ni vibaya kote duniani, lakini hapa vibaya zaidi).
Ukiangalia si mapato bali mali, ninakuta hiyo: Wealth inequality is even more drastic, with the richest 10 percent of Russians owning 87 percent of the country's wealth, making it the most unequal of the world's major economies.
 
Sijui ni kwa uzembe au walichukulia Ukraine poa hadi kujiamini kwamba wanaweza kuingia kundi lote ndani ya lifti na kupanda hadi juu ya jengo, lifti ilizimwa umeme na mwenye jengo jamaa wakabaki wamechanganyikiwa humo, hadi pale wanajeshi wa Ukraine walikuja na kuwakamata mateka, hamna kitu kigumu kama kuingia upigane na watu kwwenye nchi yao...

=======================

A team of Russian soldiers wanted to use the elevator to reach the roof of an office building. The Ukrainian administration of the building trapped them inside by cutting off the electricity. The Ukrainians also used an industrial camera to take this commemorative photo.

FNGYBATWUAMz1dX
Wawachinje hakuna jinsi apo
 
Asante, kuhusu GDP pekee unasema kweli, hapa Urusi ni nafasi ya 11 duniani (kwa sasa, tuone mwaka ujao baada ya vikwazo walivyojipatia). Ila hii ni pamoja na biashara ya gesi na mafuta, inayoweza kucheza sana (nimeona ni asilimia 60% ya GDP).
Upande wa Pato la Taifa GDP kwa kila raia unasema kweli pia, nchi ndogo ziko juu. lakini linganisha chanzo hiki (inaunganisha data za IMF, Benki ya Dunia na UM) utaona Urusi kati ya nafasi 80-85 (nilikosea kuhusu 92, ilikuwa ya zamani), Marekani nafasi ya 6-10, Ufaransa 24-29. Pato kwa raia inasema kidogo kuhusu utajiri halisi ukiangalia ugawaji wa mali ndani ya nchi, ambayo huko Urusi ni kati ya nchi zenye tofauti kubwa sana kati ya matajiri wachache na maskini wengi (ni vibaya kote duniani, lakini hapa vibaya zaidi).
Ukiangalia si mapato bali mali, ninakuta hiyo: Wealth inequality is even more drastic, with the richest 10 percent of Russians owning 87 percent of the country's wealth, making it the most unequal of the world's major economies.
Mzee Russia siyo Zimbabwe.
 
Ukiona generali kauawa basi ujue Askari wengi wa Russia wameuawa sababu generali hulindwa na Askari wengi

Nampongeza aliyeua huyo generali wa Tatu wa urusi
Ukiona ivyo ujue NATO washazama mule. Wakati wanaenda kujitolea wale makomandooo waliostaafuu, watu waliwadhani watalii wale kisa hawajavaaa makombati ya kutisha tisha wananchi. Na wale makomandooo waliostaafuu wameenda kwa ajiri ya kumalizia maisha yao pale. Kwa iyo tutegemeee mengi sana
 
Russia-Ukraine conflict could trigger global food shortage – UN​

Following a dramatic global food shortage due to the Covid pandemic, disruption to agricultural production in Russia and Ukraine due to the ongoing military conflict could seriously exacerbate global food insecurity, said Qu Dongyu, director-general of the United Nations Food and Agriculture Organization (FAO).
 
Hizi habari unapata wapi, generals 9 wameuliwa? General mwenye 4 stars anaenda kufanya nini Ukraine. Hata Lt. General na Major General si rahisi aende
Bora umesema mana nimekaa nikaona kuna watu hata uwaeleweshe propaganda imewaingia sana yani high ranking senior officers hao waende front ? Labda wa Adf Nalu huko
 
Mzee Russia siyo Zimbabwe.
tuko pamoja. Tumeanza kwenye swali ni nani anayepeleka silaha nyingi duniani (na hivyo kuwajibika kwa mauaji duniani, pamoja na kusaidia nchi kujihami). Hapo Urusi ina nafasi ya pili kabla ya Marekani na mbele ya China.
Nimeona kwamba nafasi kubwa ya Urusi ya kusambaza silaha duniani hailingani sana na nguvu yake ya kiuchumi halisi, yaani sekta ya silaha ina nafasi kubwa kwenye uchumi wake.
Ambayo si rahisi kujenga maendeleo thabiti, maana silaha hazizalishi kitu, tofauti na tasnia nyingi nyingine.
 
Hii documentary inaelezea kwa kina namna mgogoro wa Ukraine tangu miaka ya nyuma na nani huwa ndio wapo nyuma yake. Humu wamehojiwa Maraisi na Viongozi wa juu ambao wamewahi kuiongoza serikali ya Ukraine na kupinduliwa. Hii video imekuwa-banned kwenye Social Media mbalimbali. Kwenye hii video kunaoneshwa mbinu mbalimbali zinazotumiwa na Westerners(USA) kupindua serikali.
Inaitwaje niitafute

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom