LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Wakuu, Baada ya Russia kupeleka jeshi kubwa mno kwenye mpaka wake na Ukraine, mataifa makubwa Duniani yalihamaki yakiongozwa na Marekani.

NATO ilisema wazi kwamba haitaiacha Ukraine ikiwa yatima,na tayari muungano huo wa kujihami wa Ulaya magharibi na Marekani umeimarisha vikosi vyake Poland na Estonia.

Russia imepeleka zaidi ya wanajeshi 130,000 kwenye mpaka wake na Ukraine na wakati wowote wanasubiria amri ya Rais Putin Kuivamia Ukraine.

Baada ya Russia kuimega Crimea na Dunia kukaa kimya,Putin alidhani itakuwa rahisi pia Kuivamia Ukraine na kufanya lolote sasa mambo yamekuwa Tofauti.

Uingereza imepeleka shehena kubwa mno ya silaha mbalimbali Ukraine na makomandoo wa kikosi maalumu cha SAS.

Canada nayo imesema haitaiacha pekee yake Ukraine itaipa misaada yote ya kijeshi dhidi ya uvamizi wa Russia. Kwa hiyo Russia inafikia hatua wanaogopa wakijua wazi kwamba kushinda vita kwao itakuwa ngumu mno.

Na hakika Russia ikijaribu kuivamia Ukraine haitashinda hii vita zaidi ya kuharibikiwa kiuchumi. Russia ni nani hasa hata ashinde vita dhidi ya Marekani, Uingereza, Canada na mataifa mengine mengi ambayo yanaisaidia Ukraine bila kuitangazia Dunia.

Mengine yabakie ushabiki tu, lakini Russia haitashinda hii vita na wao wameshaliona hilo.

View attachment 2119949
Mbona hao wamemkimbia Ukrain mkuu. Raisi wa Ukrain anawapigia sim wanaogopa hata kupokea.
 
Kimsing Ukraine kaingizwa mkenge na NATO. Yeye alidhani atakubaliwa kujiunga NATO, kama ingetokea angekua salama na Urusi isingemgusa ila Putin kahack mchongo. Wote walioahidi kumlinda are nowhere to be seen.

Russia ana kila sababu za kuivamia Ukraine kwa usalama wake. Ukraine ilikuwa inawapa NATO easy access to RU including kukubali NATO waweke majeshi na nyenzo za kivita kwenye ardhi yake. Nchi yeyote inayojielewa haiwezi kukubali hili.

Kumekua na chokochoko za Znz kujiengua JMT ili wasaidiwe na mataifa mengine yenye mrengo tofauti na JMT. Nashauri wachukue notes toka kwa Ukraine ili wasije ingia mkenge kama wao.
 
Tz ina nguvu gani itakayo yafanya hayo mataifa yaliyo kinyume chake wamuogope?
Maana Urusi inaogopwa kwa sababu ya nguvu zake.
je ss tunazo hizo nguvu.
 
Bora angeandika tu #UziTayari akatembea mbele kuliko kuandika pumba na kuzidi kujiaibisha.
Kaka unajua nyuzi ilipotokea au umedakia tu baada kuona mods kuunganisha kwenye hiyi nyuzi mi sikuuongelea uzi huu tunaukoment saiz kuna nyuzi imeungwa humu ambao ndio niliouchangia huku mods wamefanya kutuleta tu
 
Kwanza kabisa nilikuwa miongoni mwa watu ambao wanashabikia Vita hivi vya Urusi na Ukraine Kama mechi ya Simba na Yanga. Lakini baada ya kuona jinsi Wanajeshi wa Ukraine wanavyoteketea Basi nakili kwamba,Vita ni mbaya Sana.

Putin nakuomba simamisha Vita vya Ukraine,huu ni unyama mkubwa dhidi ya binadamu.

Naomba nitoe tahadhari. Hii video ni hatari Sana,Picha na Video zinakirihisha. This is Madness. Binadamu wote tupinge Vita hivi.

View attachment 2130972
Kaka chek pm yako

Sent from my Infinix X609 using JamiiForums mobile app
 
Kwanza kabisa nilikuwa miongoni mwa watu ambao wanashabikia Vita hivi vya Urusi na Ukraine Kama mechi ya Simba na Yanga. Lakini baada ya kuona jinsi Wanajeshi wa Ukraine wanavyoteketea Basi nakili kwamba,Vita ni mbaya Sana.

Putin nakuomba simamisha Vita vya Ukraine,huu ni unyama mkubwa dhidi ya binadamu.

Naomba nitoe tahadhari. Hii video ni hatari Sana,Picha na Video zinakirihisha. This is Madness. Binadamu wote tupinge Vita hivi.

View attachment 2130972
Kivyovyote vile vita ni mbaya sana.

Kuna watu humu hawaipend USA na washirika wake basi wanatumia vita hii kuwadis na kushangilia umwagaji damu unaoendelea Ukrain. Na kuna watu wanaikubali sana Urusi nao hivhivo wanatumia vita hii kuisifia zaid.

Lakini pia kuna wadini nao pia wanajifanya kuiingiza Israel hapa na sababu zao za kidini wakati Israel ikivamia wao huwa upande wa hao wauwaji wa Israel ila tu udini unawasumbua.

Vita ni mbaya jama ni mbaya jama, hao njemba hapo wameacha wajane na yatima huko mtaani, wamewaliza wazazi wao pia.

Ni bora njia za kidiplomasia zikasuluhisha huu mgogoro. Yote mwa yote Marekani ni wa kwanza kuwaingiza mkenge wenzao na wao kukaa pembeni.
 
Hizo zilikuwa nchi moja kwenye muungano wa Kisovieti..
Kuna makubaliano kadhaa ya ki usalama kati ya Urusi na baadhi ya nchi zilizokuwa USSR.
Yaliingiwa lini hayo makubaliano? Mie naona Putin na RUSSIA anaceheza u kaka mkubwa tu
 
Tz ina nguvu gani itakayo yafanya hayo mataifa yaliyo kinyume chake wamuogope?
Maana Urusi inaogopwa kwa sababu ya nguvu zake.
je ss tunazo hizo nguvu.
Urusi haiogopwi ,ndo mana wameamua kumpiga tu kiuchumi , Hana mchongo wwte wa kuwafanya wahuni wapoteze Askari wao,aliyechochora ni Ukraine Kwa kukubali kugeuzwa toilet paper na hao NATO
 
Atachoka sana., Amemwaga mboga.....
Wakati nchi kama China Brazil India zinaendelea kukuza uchumi wao na kuendelea kuwa kwenye top Ten kwa maana ya GDP Russia (ambaye top ten hayupo) anapambana na vikwazo vya kiuchumi kwanza mpaka aje atoke hapo kachoka hatareeee.
 
God bless ukraine
Screenshot_2022-02-25-19-43-02-545_com.instagram.android.jpg
View attachment 2131092
 
Back
Top Bottom