Exclusive Update kutoka ndani ya "Fikra" za wanoelekeza vita ya Ukraine.
Kanali Douglas McGregor akihojiwa amesema Ukraine ilianza vita na Russia ikiwa na wanajeshi wa ardhini na mstari wa mbele yaani "frontline" kati ya 300,000 hadi 700,000.
SMO ya Russia na khasa ile iloongzwa na jenerali Surovikin ilipunguza idadi hiyo kwa kiasi kikubwa hadi hadi kuwa chini ya 190,000 na hiyo ilikuwa kabla ya mwezi January mwaka huu.
Makisio halisi ya idadi ya wanajeshi wa Ukraine walokufa vitani, au kujeruhiwa ama kupotea nakhasa pale Bakhmut ni 1,000 kwa siku.
Sasa tufikirie watu walotayarishwa kwa vita ni kati ya 300,000 na 700,000 kwa msaada wa NATO na washirika wake wote na US kwa miaka minane wakitakiwa kuwa katika viwango vya majeshi ya NATO.
Ni wazi kuwa taarifa hizi (za idadi ya vifo) haziwezi kuwekwa wazi na vyombo vya habari vya nchi za magharibi ambavyo vyafuata mwongozo maalum.
Jambo jingine ambalo bado lafichwa ni mpasuko ndani ya vyombo vya ujasusi na jeshi ndani ya Marekani kwenyewe. Mzee Henry Kisinger ambae ni mmoja wa watu ambao wamekuwa nyuma ya NWO na mshiriki mwandamizi ndani ya DS amenukuliwa akikiri wazi kuwa kwa muda mrefu mpango umekuwa ni kuivunja Russia iwe na vitaifa vidogovidogo na kisha kuvifanya vitaifa hivyo viwe tegemezi na mwisho kutumiwa kuiba raslimali zake.
Hili jambo limefafanuliwa mara kwa mara na raisi Putin mwenyewe katika hotuba zake na ndio sababu halisi ya Russia kuivamia Ukraine ili kuvunja mpango huo.
Mzee Kisinger mwenyewe amekiri kwamba mpango huu ni wa hatari sana na hauko imara sana na ametoa ushauri kwamba Russia iachiwe Crimea na iachie miji mingine ya Luhansk na Donetsk ambayo iliamua kujitenga kabla ya Januari 2022 na baadae kutangazwa na raisi Putin kutambuliwa rasmi.
Ni wazi kuwa Russia haitakubaliana na wazo hilo la mzee Kisinger.
Mzee Kisinger ni nani.
Huyu mzee ambae ni myahudi ni mwanadiplomasi awa Marekani ambae alizaliwa Ujerumani na amekuwa waziri wa nchi (Secretary of State) na mshauri wa usalama wa maraisi Richard Nixon na Gerald Ford.
Kisinger ndie ubongo wa Marekani katika sera zake za mambo ya nje na maeshiriki kutengeneza sera nyingi ambazo zingine zimekuwa ni za hatari sana zinohusu hata kuleta vita katika maeneo yalokusudiwa na Marekani kuwa himaya zake na zenye maslahi.
Mzee huyu ameshiriki mission nyingi duniani kuanzia Vietnam, Cambodia, Bangladesh, Pakistani, India, Ulaya Mashariki, mgogoro wa Israeli na Palestina na eneo lote la mashariki ya kati.
Sehemu zingine ni Cuba, Chile, Congo DRC (zamani Zaire), Zimbabwe, Sahara Magharibi , China na sasa Ukraine.
Barani Afrika mzee huyu ambae sasa ana miaka 100 amehusika na sera nyingi za mambo ya nje kuhusu bara hili kuanzia Afrika Kusini, Zimbabwe, Angola, Namibia.
Watu ambao amemsumbua sana mzee Kisinger na harakati zake ni pamoja na chifu Mangosuthu Buthelezi na chama chake cha Nkata, hayati Mwalimu Nyerere na msimamo wake wa kusaidia nchi zilokuwa zikihitaji kukombolew ziwe huru kusini mwa Afrika.
Pia mzee Kisinger katika miaka ya 1970 alikumbana na Russia na Cuba zilokuwa zikiwasaidia wanajeshi wa Angola na chama cha MPLA ambao walikuwa wakipambana na kikundi cha UNITA cha Jonas Savimbi ambacho kilikuwa kisaidiwa na Marekani.