Hizo drony zilitoka kumuua pootin zitakuwa za NATO/USA
Hapana ni drones za Ukraine.
Ukraine wamekuwa wakidevelop UAVs za range mbalimbali na wamekuwa wakiitaka sana Marekani waridhie majaribio yanoingia ndani ya Moscow.
Wakifanyacho ni kuokota zile UAVs ambazo wamefankiwa kuzidungua za Russia au Iran na kwingine na mara moja huingia maabara kuzifanyia kazi na kuzitengeneza na kuziboresha. Sasa wakimaliza kazi hutafuta pa kuzijaribia.
Lakini hapa pana nadharia mbili:
Kwanza, kuna kipindi nyuma gazeti ya New York Times liliandika kwamba Ukraine walikuwa wakiomba sana kufanya majaribio hayo.
Hivyo tukio la juzi kule Crimea kwenye matanki ya mafuta na hili la Kremlin yanaweza kabisa kuwa yamepata baraka za Marekani au pia hayajapata baraka hizo ndo maana Marekani nao wamechanganyikiwa kwani hawakutegemea kama Ukraine yaweza kufanya hivi.
Pia nadharia ingine ni kwamba huenda watu ndani ya Russia ambao hawajaridhika na hatua ambazo Russia imefikia katika vita hii na kuona kwamba Putin anasita sana kufanya maamuzi magumu, wanataka kumlazimisha Putin kuchukua hatua kali ambazo ni kufanya mashambulizi makali khasa kuelekea Jumatatu ambayo ni siku muhimu kwa Russia.
Katika historia tarehe 9 May 1945 Russia ilitangaza ushindi dhidi ya Ujerumani ambapo siku moja kabla yaani tarehe 8 May 1945 majeshi ya kinazi ya Ujerumani yalitangaza kujisalimisha na wakatiliana saini na Russia kwamba wamejisalimisha.
Tarehe 9 May 1945 ndo siku yale mataifa madogo 16 yaliungana na ikazaliwa USSR.