LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Achana na propaganda za nchi za magharibi hizo.

Kwanza, China ndo walomtosa US kwa kumwambia Putin kwamba US walikuwa wakiteta nao ili wambembeleze Putin asiivamie Ukraine.

Pili, kusikia hivyo Putin (kama wafuatilia) akaenda China mwanzoni mwa michezo ya Olimpiki na akahakikishiwa taarifa hizo (za kuhusu US) kwamba Biden alikuwa akiwaomba China tangu mwezi November 2021 waongee na Putin, China akakataa.

Tafuta gazeti la New York Times wameandika habari hii.

Tatu, nimeeleza mara nyingi humu kwamba Russia hawakupanga jambo hili(kuivamia Ukraine) jana au juzi ni jambo la kitambo tangu 2014 na wengine wasema ni nyuma zaidi ya hapo walikuwa wakiwasoma Ukraine kwa ukaribu.

Saa hii majeshi ya Russia yapo ndani ya Kyiv na kufikia jumamosi au jumapili tutasikia habari zingine.
Unatumia nguvu kubwa utapata faida gani Russia akishafanikiwa lengo lake jumapili/jumamosi la kuvamia hizo nguvu ungeziwekeza kwenye mambo ambayo yanatija kwako
 
Kwanza kabisa nilikuwa miongoni mwa watu ambao wanashabikia Vita hivi vya Urusi na Ukraine Kama mechi ya Simba na Yanga. Lakini baada ya kuona jinsi Wanajeshi wa Ukraine wanavyoteketea Basi nakili kwamba,Vita ni mbaya Sana.

Putin nakuomba simamisha Vita vya Ukraine,huu ni unyama mkubwa dhidi ya binadamu.

Naomba nitoe tahadhari. Hii video ni hatari Sana,Picha na Video zinakirihisha. This is Madness. Binadamu wote tupinge Vita hivi.

View attachment 2130972
Daaah jamani😪😪😪 , hii video inatisha, wakae mezani amani ipatikane jamani.
 
Back
Top Bottom