NATO HAINA UWEZO WA KUPIGANA VITA NA URUSI
Mkuu, nadhani tukubaliane kutoafikiana.
Vita havina macho. Ndiyo maana hata wanajeshi wanaweza kuwahofu wanamgambo tu, au maaskari wakatimka mbio na kujificha mbele ya majambazi wenye mapanga tu.
Katika karne hii ya 21 hakuna mbabe halisi wa vita.
Yeyote atakayethubutu kupima upepo huo ni mpumbavu, mwehu na adui wa dunia nzima.
Wanaodai eti NATO haina uwezo wa kupigana na Urusi, au Urusi hana uwezo wa kukabiliana na NATO ni watu wa kupuuzwa tu.
Kiongozi yeyote anayetambua wajibu mkubwa wa kulinda uhai duniani, anastahili kupongezwa na kuungwa mkono.
Mashabiki koko wanaotamani ^mvua inyeshe ili tuone panapovuja,^ ni kundi lingine la vichaa wasiojitambua.
Iwapo Marekani, NATO au Urusi au hata China na NK wangeamini vinginevyo, kitambo sana wangeshakinukisha.
Nadhani ubabe halisi duniani ni kujua una silaha na ulinzi bora, lakini ukajizuia kuzitumia ili kuwaangamiza wengine.
Katika hili, Urusi inastahili pongezi kubwa. Si ajabu watu wanajiuliza mengi bila kuwa na majibu dhahiri:
Kwa nini Zelensky angali hai hadi sasa? Kwa ni vita vimechukua muda mrefu kiasi hicho? Kwa nini anawahurumia vile? Kwa nini hajaisambaratisha ngome ya Kiev mara moja?
Bila shaka hiyo ndiyo sababu mojawapo.
Katika vita vya Ukreni vs Urusi, kwa jinsi Ukreni ilivyopondwa, ukimtathmini Zelensky kwa makini au hata baadhi ya washirika wake wa karibu kama Polandi, wanatamani Urusi afanye kosa hilo la ^kurusha jiwe la kwanza^ ili wazame wote.
Lakini imethibitika tena na tena kwamba Putin anajua fika hesabu zao chafu kiasi kwamba mara kwa mara amevunja matarajio yao na kuwapoteza maboya.
Mustakabali wa dunia utakuwaje? Muda wenyewe utaongea.
Tusisahau kwamba Marekani na NATO bado ni mataifa yenye nguvu duniani, na hivyo kuaibishwa vile ni hali inayoweza kuwafanya wachukue maamuzi ya woga ya mfamaji.
Yote kwa yote, Mungu aepushie mbali mauaji ya mamia ya raia wasiokuwa na hatia.