😂😂😂Mwaka huu tutaona mengi. Ukraine wameanza kutumia nguvu ya Giza (uchawi) kutungua mabomu ya Urusi .
View attachment 2960292
Meanwhile, in Odessa, the use of the latest air defense system was recorded - a combat Ukrainian witch who is trying to shoot down Russian missiles with magical passes.
Ha ha haa.
Hii ni marudio Mkuu.
Wakati vita TU inaanza watiibuka watu huko Ukraine waliandikwa kama wachawi wa Ukraine walikusanyika ili kumroga Vladimir Putin ili afe.
Lkn Leo ni mwaka wa pili Putin anadunda.
Propaganda nazo zilichukua nafasi kubwa.
Wakaibuka majasusi wa M16 wao wakasema Putin alishakufa kitambo,huyo aliepo sio. Ni kafanyiwa "clones" .lkn Putin ndio huyohuyo orijino.
Wengine wakasema Putin anaumwa ugonjwa wa ajabu na hata hukua muda atakufa,Mwamba yupo TU.
Wakaja watabiri wa west na hata wa humu JF,mfano Kuna bwana mmoja anajiita Tumainiel yeye alisema mwezi hauishi Dunia itashuhudia kifo Cha ghafla Cha kiongozi mmoja mkubwa hapa Duniani,kwani hawezi kucheza na intelligence ya west na akabaki salama.kwq maelezo ya huyo mnajimu uchwara wa humu JF aliweza hata kumtaja kua Putin ni lazima atakufa.
Mwamba yupo hai Hadi Sasa hivi.
Unaweza kudhani ni hao TU,la hasha.kuna majasusi wa west walisema Putin atapinduliwa,mwamba yupo na ameshinda uchaguzi kwa kishindo huko Urusi.
Kuna watu wakati vita inaendelea walisema Kuna Putin wawili,orijino kajificha kwenye handaki maalumu na Putin fake ndio anaeonekana hadharani,ukweli ni kwamba Kremlin walisema mwamba ni yeye,na ilifikia wakati mwamba alisafiri kwa ndege Hadi uarabuni wakati vita ikiendelea.
Propaganda na uongo wa nchi za Magharibi uliwaaminisha watu kua majeshi Bora na majasusi wanaoongoza ni kutoka nchi za west.
Ukiuliza shirika Bora la ujasusi duniani watakutajia nchi ya kwanza Hadi ya Tano ni kutoka nchi za west halafu watakutajia Urusi ni nchi ya SITA kwa ujasusi duniani.
Mfano TU,watakutajia
CIA ya USA,
MI6 ya UK,
Mosad ya israel
Watakuambia ISI ya Pakistan,
Watakuambia ya ujeremani
Na baadae watakumabia ya Urusi.
Sasa kiuhalisia na kwa mshangao ukitoa Pakistan hao wengine walobaki wapo kuisaidia Ukraine,sio TU kivita hata kuratibu na kuharibu uchumi wa Urusi.
Kwa mfano wali design vita mbili Kwa mara moja,mseto wa vita ya kijeshi na kiuchumi ili kuidhoofisha Urusi,kwa kuiwekea vikwazo maelfu ili ishindwe kuendesha vita na kuipa Kila aina ya misaada Ukraine ili iishinde Urusi,lkn matokeo yake imekua kinyume chake,wao ndio wedhoofika na Urusi ndio kwanza imestawi kiuchumi na hata kijeshi,pia imejikuta inapendwa na kuaminiwa kimataifa.
Ajabu kuu katika vita hii mseto.
Tulikua tunaaminishwa mabigwa wa uchumi wako west,na majeshi Bora Yako west,mashirika Bora ya ujasusi Yako west Sasa Cha kushangaza ni kwa Nini mkusanyiko wa wataalamu wa ujasusi wa kiuchumi kwa umoja wao wameshindwa kuidhoofisha na kuipigisha magoti Urusi?
Matokeo yake wao ndio wanaipigia magoti Sasa,maana Urusi kawaamuru wanunue gesi kwa pesa yake tofauti na zamani walikua wananunua gesi kwa pesa Yao,yaani Dola.
Nakumbuka kabla ya vita kuanza Urusi ilizunguka west yote kuwaomba Ukraine isijiunge NATO,wakakaidi na Biden akaiambia Urusi iachane na mipango yake ya kutaka kuivamia Ukraine la sivyo isahau mradi wa Bomba la gesi NS2.
Urusi ikavamia.
Nashangazwa na umoja wa wataalamu wa kijeshi wa nchi za NATOplus.maana Sasa NATO imeongezeka kutoka nchi zilizokuwepo kabla ya vita na Sasa hivi kwani Kuna nchi amabazo sio wanachaama wa NATO nazo zimeungana na NATO.
Zilizoungana na NATO wakati wa vita ni Ukraine, Sweden,Finland,na Australia.
Wataalamu wa nchi hizo wa masuala ya kivita au majenero wao wameshindwa na jenero mmoja TU wa Urusi.
Mfano wanaoendesha mitambo yote ya msaada ya silaha,ni wao ndio wanaoendesha mitambo hiyo,mfano Mifumo ya patriot inaendeshwa na wamarekani,storm shadow inaendeshwa na waingereaza,Mifumo ya rada na satellite inaendeshwa na walioitoa iwe wa USA ua wa UK au wafaransa au wajerumani n.k Hawa wote wamezidiwa na waendesha mitambo kama hiyo wa urusi.nilitegemea kwa umoja.wao wangekua na matokeo chanya,lkn kifupi Urusi anachukua maeneo kuanzia Kanda ya donestk,luhanak,mikoa,wilaya,tarafa,kata ,vijitu na hata mitaa ya Ukraine Kuelelekea mkoa wa Odessa na kyiev.
Kitu Cha kweli kabisa ni kwamba majasusi wa kijeshi na kiraia wa nche za west hususan baba lao CIA hawakua wanaijua Urusi vizuri,hawakua na taarifa za kutosha za Urusi.
Maana ni kama wameingia Cha watu wa jinsia tofauti.
Mfano mdogo TU,tuliambiwa kua Urusi Haina silaha na fedha za kuweza kupigana kwa miezi SITA,Urusi Haina silaha Bora,oooh inatumia vifaa vya washing machine kutengeneza silaha,Warusi hawamuungi mkono Putin atapinduliwa,machafuko yatakuja Urusi,masupamarket yameishiwa bidhaa,Urusi itatengwa kimataifa.
Ukweli ni kinyume chake.
Sasa hapa ndugu zangu ni mashirika yapi Bora kabisa ya kijasusi kati ya mashirika ya west na ya Urusi?
Nakuambia tulidanganywa humu,kuna watu walisema jeshi la Urusi haliana nidhamu,ooh Urusi Haina jeshi Hadi inatumia jeshi la kampuni la Wagner,ha ha haa,wengine wakasema Urusi Haina jeshi na jeshi lake nidhaifu Hadi inatumia jeshi la Chechnya,utadhani Chechnya ni nchi mojawapo huko Asia ya mbali.
Ooh Urusi inasaidiwa silaha na Iran.
Dah ni pengine hatujui yaliyo nyuma ya pazia,inawezekana
au pengine Iran iliiomba Urusi ijaribu drone zake katika uwanja halisi wa vita ili kuona uwezo wake,au pia Urusi ilinunua droni hizo ili kutunza silaha zake zisiishe mapema.
Lkn hata hivyo ni uoga wa USA na genge lake,inakuaje wao wanashirikiana kuishinda Urusi,lkn wao hawataki Urusi ishirikiane na marafiki zake? Huu ni uoga wa Karne.
Sasa vita inaenda kuchukua sura mpya, ufaransa anawashauri wenzake waingie mazima waache kutuma silaha.
Tutaona.
Lakini wamesahau vita hii Urusi sio TU ni mashine ya kusaga nyama za watu,Bali pia ni mashine ya kuchoma silaha za adui na kuzigeuza kua vyuma Chakavu.
Kwani kama mtakumbuka vizuri wakati vita vinaanza silaha zilikua zinashushwa Kila siku hapo Ukraine Kwa kitumia madege,maroli,mameli na matreni.sasa je zote hizo zimeenda wapi?
Pia mamluki kutoka Kila pande ya Dunia walikua wanatiririka huko Ukraine walikuja maelfu kwa maelfu,Kuna mtu alikua akiitwa Wali,huyu alisifiwa kama mdunguaji Maarufu na Bora kabisa hapa duniani je alipotelea wapi?
Je hao mamluki waliishia wapi?
Ndugu zangu hebu tuangalie walichokipata NATO huko Afghanistan wakipambana na kikundi Cha Watalaban kisicho na satellite,rada,mizinga,vifaru,bulletproof, helmet, air force, air defense,navy,fedha n.k
Sasa hivi wanapambana na jeshi lenye Kila kitu kama wao.
Huko Ukraine ni ukweli ni kwamba NATO+ walichoweza ni kupunguza TU spidi ya Urusi ya kuchukua majimbo Kwa haraka,lakni kuizuia wameshindwa.
NATO+ ndio watachagua kupigana vita kubwa kwa kuingiza majeshi ili kuizuia Urusi isisonge mbele au la, lakini Urusi ni lazima itaichukua Odessa.