Mimi kuna muda najishtukia na kujiwazia kwa jinsi nilivokua nasikia kuhusu mambo ya vita na watu wa ulaya magharibi nilinganisha kwa sasa wanachofanyiwa na urusi nahisi labda hao nato wanamsoma tu mrusi labda ipo siku kibao kitamgeukia russia maana bado siamin kama nato wamefeli kwa aibu hivi
Uko sahihi kabisa Mkuu millerson.
Hivyo unavyojishitukia na hivyo unavyojiwazia uko sahihi kabisa na watu wengi wako hivyo kwa Hali jinsi inavyoendelea huko Ukraine.
Hali uliyonayo ndio Ile kitu inaitwa mshangao,bumbuwazi au kutoamini unachokiona maana Kwa miaka mingi watu waliamini NATO ndio Kila kitu,ndio wababe wa vita hapa duniani,hakuna kama wao,Leo hii iweje washindwe kuidhibiti nchi moja TU Tena iliyowekewa vikwazo kuliko nchi yoyote hapa duniani?
Hali unavyojisikia wala sio wewe TU,Bali ni mshangao kwa watu wengi hapa Duniani,yaani hawaamini wanachokiona na wanachokisikia.
Kama usemavyo watu wengi wanahisi kama unavyohisi wewe kua NATO wanamvuta TU Urusi ili aingie kwenye kumi na nane zao ili wamle kichwa,lakini ukweli sio hivyo hata kidogo,ngoma imewashinda na hamna namna watamfanya Urusi.
Ukweli uko hivi.
NATO hawana uwezo wa kuipiga Urusi hata kidogo,Bali wanaweza kupigana na Urusi na asitokee mshindi wa wazi.
Vita ya NATO na Urusi sio vita kama Ukraine na Urusi.
Vita ya Urusi na NATO itakua ni vita ya kuangamizana kabisa maana Kila upande hautatoa hata nafasi ya kujisalimisha,kwa sababu wote wanaogopa aibu ya kushindwa na hawako tayari kua chini ya mwenzake (koloni,mtumwa au mateka)baada ya vita,wanaona ni Bora wapotee wote.
Ishu ya kusema eti NATO bado wanamsoma Urusi hiyo Haipo,kwa sababu kwa tabia za NATO hua hawajisikii vizuri kuona watu wanakufa Kwa maelfu kama vile ilivyokua Bosnia and Herzegovina,Kosovo,Sarajevo n.k. hasa nchi iliyopo bara la ulaya.
Leo hii wa Ukraine wanakufa Kwa maelfu namna hiyo eti bado wanamsoma Urusi,hii sio kweli,ukweli wanaogopa majibu ya urusi.
NATO hawana uvumilivu huo wa kumsoma Urusi kama Wana uwezo wa kumpiga,maana Hali inazidi kua mbaya kwao Kila kukicha,miji inachukukiwa na watu wanakufa,wakimbizi wanazidi kujazana ulaya,uchumi wao unayumba na akiba zao za silaha zinazidi kupungua.
Wangekua Wana uwezo wangeshaingia mapema na kumpa Urusi pigo moja takatifu na kumaliza vita ili kuepusha maafa makubwa kama hayo barani ulaya,lkn wanaogopa kwa sababu Urusi inao uwezo thabiti kabisa ya kuwajibu vizuri na mara dufu kuliko wao.
NATO waliingia Yugoslavia ili kuepusha muaji ya kimbari,NATO waliingia Libya ili kuepusha mauaji ya ya kimbari.leo hii Kwa Nini waendelee kupoteza muda eti wanamsoma Urusi ambae anafanya mauaji kwa nchi ambayo wao ndio wameiponza ?
Wataendeleaje kumsoma Urusi ambae Kila siku anachukua maeneo?
Je wanasubiri ili afike wapi?
Kwa kifupi uwezo wa kuingia kwa Urusi kama walivyokua wanaingia kwa akina Iraq hawana,Urusi ni maji ya bahari sio maji ya mto.