LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums

Yaani nyie pro USA na NATO sijui hua ni utoto au kutokua na ufahamu wa kutosha wa Geopolitics ndio hua unawasumbua!?
Hapa ukweli umeongea kitoto mno,hoja Yako imekosa weledi na urali.
Hivi Kwa akili za kitoto kabisa ,hasa watoto wa darasa la sita au la saba wanapojadili mada hii hawawezi kutoa ulinganifu dhaifu kama wako.
Hivi kweli mmawezaje kulinganisha Nchi dhaifu kijeshi ya Iraq enzi za Sadam Husein dhidi ya nchi za NATO?
Kweli mtu umemaliza hata form four TU katika Discussion hawezi kulinganisha Iraq na NATO.
Nchi ya Iraq kuilinganisha na NATO hakiwezi kutoa majibu sahihi kua NATO ni umoja wenye nguvu za kijeshi Bora kabisa hapa duniani,kwa sababu Iraq ni nchi dhaifu sana ,wala haikua inaunda silaha zake zaidi ya ku modify vikombora vichache kutoka Urusi.
Waliweza kumodify kombora la kizamani la USSR la Scud B na kuliita El Abbas na jingine El Hussein, na vijisilaha vingine vidogo vidogo.
zaidi ya hapo Iraq hawatengenezi silaha.
Iraq hawakua na mfumo wa maana wa ulinzi wa anga ,hawakua na navy ya maana,wala airforce ya maana kuweza kulinganisha na airforce,navy na ground forcces ya NATO.
Hebu fikiria vizuri wewe mtoto, USA ambayo nyinyi mnaamini ndio number one super power inatengeneza Kila aina ya silaha hapa duniani na silaha nyingine ambazo hata nchi nyingine hawana,hebu fikiria nchi kama UK, German na nchi nyingine zote za NATO Kwa wakati huo huku ukiiondoa ufaransa ambayo haikuenda vitani pamoja na NATO,zitazame nchi hizo uwezo wao wa kuzalisha silaha na uwezo wao kijeshi kisha zilinganishe na Iraq ndio mtajua kua nyie ni watu wa aina Gan.

Leo hii NATO kupata ushindi dhidi ya nchi kama Iraq hii ni aibu kubwa mno.
Kumbuka Iraq haikua ikisaidiwa na nchi yoyote hapa duniani.

Hoja ya pili katika makala Yako ni kuilinganisha NATO na Urusi.
Hoja hii moja Kwa moja inaipa ukuu na heshima kubwa mno Urusi.
Na hoja hii ndio inatufungia mjadala wetu juu ya nani zaidi kati ya Urusi na USA.
Nadhani nyie pro NATO wote humu hua mnaipa Urusi heshima kubwa mno kwa kuilinganisha na NATO.

Kwa sababu nyote humu na sehemu nyingine duniani hua mnasema USA ndio superpower Sasa kama super power wenu peke yake hawezi kukabiliana peke yake na Urusi mpaka awe na ushirikiano na nchi nyingine kubwa kijeshi duniani za ulaya ambazo ndio zinaunda umoja wa NATO, basi maana yake huyo superpower wenu haiwezi Urusi akiwa peke yake.
Haya sio maneno yangu Bali ni maneno Yako wewe mwenyewe hapo juu,umesema kua NATO wakiingia vitani kamili dhidi ya Urusi basi Urusi itapigwa na Putin atanyongwa kama Sadam Husein.
Hapa wewe mwenyewe unakili kwa kinywa chako kua hakuna nchi moja ya ulaya Magharibi peke yake inaweza kuishinda Urusi peke yake bila kushirikiana na nchi nyingine zinazounda umoja unaoitwa NATO.
Kwamba hata super power wenu USA hawezi kuishinda Urusi bila nchi nyingine zinazounda NATO.
Hii ndio tafasiri ya hoja zako.
Mimi nilitarajia ungesema kua USA akiingia vitani na Urusi USA itaishinda Urusi na kumnyonga Putin.
Hapa Kwa maana nyingine umemaanisha kua Urusi moja inaweza kushindwa na nchi 32 pekee.
Nchi moja peke yake haiwezi kuipiga Urusi.

Labda nikuambie kitu Cha mwisho hapa unqpoona sio NATO pekee inayokabiliana na Urusi,Bali ni all collective west,sio TU wanapeleka silaha,Bali pia wameiwekea vikwazo ili idhoofike kiuchumi ishindwe kugharamia vita.
je kwa akili Yako wewe unavyoona Urusi hii ya Putin Hadi tarehe hii ya Leo imeshindwa kugharamia vita baada ya kuwekewa vikwazo?

Unajua kua USA akitaka kupitisha ajenda yake hashindwi?
alikataliwa na UN kua Iraq isipigwe kwa sababu Haina WMD lakini kwa ubabe USA wakaenda kumpiga.

Sasa kwa Nini wasimpe Ukraine uanachama wa NATO kibabe kisha wapate sababu ya kuingia vitani kama NATO, ili kumpiga Urusi?

Kumbuka Kuwait na Kosovo hazikua Wanachama wa NATO lkn NATO walizipigania.

Hata Iraq na Libya zilipigwa na NATO.

Lakini pia napenda nikuambie kua,wanajeshi wa NATO wanashiriki vita hii Kwa jina la marcenaries(mamluki) je wamebadilisha Nini.?

Mfano mwingine NATO waliweza kuyaangusha makombora na droni za Iran zilizokua zinaelekea kuipiga Israel,lakini zelensky kawaomba na kuwasihi waweke No fly zone wamekataa alipoona Israel imepata huduma hiyo akawalaumu sana alisema kwa Nini mnatubagua sisi Ukraine mbona Israel mmeipa huduma ya kudungua makombora yaliyopigwa na Iran?

Jibu ni kwamba Urusi sio sawa na Iraq wala sio sawa na Iran.
Ila napenda nikuhakikishie kua Urusi nae ana washirika ambao NATO wakiingia hawatakaa wakitazama,nao wataingia kuisaidia Urusi.
Ni akina nai hao? Mimi sijui ila wapo.
Je vita itakuaje?
Mimi sijui.
Tafakari.
 
Yamkini Russia ameshatumia uwezo wake kwa zaidi ya 80% dhidi ya Ukraine. NATO mpaka sasa sioni kama imeshatumia hata 40% ya uwezo wake kumpa Ukraine. Kusema kwamba Russia anaweza kutunishiana misuli na NATO huko ni kuikosea NATO.
Wachambuzi wengi sana wa vita hii hua mnasumbuliwq sana na utoto.
Hivi wewe kijana wa kitanzania pengine ni mkaguru kwa kabila unawezaje kujua stock ya silaha za Urusi na hata za NATO?
Hivi wewe kweli unazijua Siri za jeshi la Urusi kuliko Shoigu,Putin na Medvedev?
Ok sawa tufanye hoja Yako Iko sawa,Sasa hizo aslimia 80 za silaha za Urusi zilizokwisha tumika,je zimetumika kupiga milimani ,maporini na baharini?
Hakuna silaha za NATO zilzoharibiwa?
Au hakuna wanajeshi wa Ukraine na NATO waliokufa na silaha zao zilzoharibiwa?

Hata hivyo unaonaje hoja Yako kuwa inaipa Urusi ukuu mkubwa sana?
Kwa sababu Urusi peke yake inapigana na nchi zote zA NATO ambazo kwa ujumla ni nchi 32 ambazo yumo superpower wa Dunia Ndugu Marekani.
Je kati ya NATO na Urusi nani ni mkubwa hapa?
Maana hapa Kwa Sasa hivi hatuiongelei Tena a Ukraine,Bali tunaiongelea NATO.na ndani ya NATO yumo world superpower USA
Je huoni hapa Urusi ndio kubwa?
Labda nikukumbushe Urusi sio Iraq wala Yugoslavia wala libya.urusi ni Urusi.
Kwa misaada ya silaha, vikwazo na fedha NATO wanazoipa Ukraine na kwa sababu Urusi imebakiza 20%ya silaha zake nadhani huu ndio wakati mwafaka wa kuingiza rasmi jeshi la NATO kwenda kuimaliza Urusi rasmi.

Maana kwa makadirio Yako wewe jasusi wa Dunia kua huenda Urusi imeshatimia 80% ya silaha zake,wakati (NATO)hapa sio Ukraine Tena kua haijatumia hata 40% ya silaha zake.
Mie hua mnanipa Raha sana kuilinganisha Urusi peke yake dhidi ya NATO ambayo ndani yake Kuna super power wa Dunia,hii maana yake super power peke yake hawezi kuingia vitani na Urusi.
Ninashukuru sana kwa kutambua ukuu wa Urusi kijeshi bila kificho.
 
The Ukrainian military used a Ukrainian-made Palianytsia drone missile to strike Russian forces for the first time, President Volodymyr Zelenskyy announced on Aug. 24.
 
Je ni sahihi moscow kuzingirwa na adui lakini ni kharamu washington kuzingirwa na urusi? Hizi akili za wapi? Au ni kutojua geopolitics na historia ya dunia? Cuban missiles saga ya kipindi cha John fitzergad kennedy hamuijui nyie pro usa au humu tunajadiliana na vitoto vya seko?
 
Mpaka sasa hivi wanajeshi wa Ukraine zaidi ya 5,000 wameshazika hapo Kursk mass Graves, supply chains ya silaha, vyakula katika front line imeshakatwa, hivyo wanajeshi wa Ukraine na NATO walioko kursk watajifia uko mbele au kusalimu amri.
 
Kuna hoja za ki form six zinaendelea hapa . US angeweza kupambana na mataifa makubwa 50? Chini ya vikwazo lukuki ? NATO ni kundi kubwa sana lingeingia live mwanzoni waone moto. Hao west wakifa askari mia saba tayari maandamano wasingeweza
Mkuu, vita ni mbinu bora, askali bora, vita ni akili, mikakati. uwezo wa kifedha, uwezo vifaa vya kisasa vya vita n.k. Kwa uju.mla vita havitaki hasira bali mikakati yenye UMAKINI. Ona sasa Putin amekuwa Mpole anaona bora liende.
 
Tayari madaraja ya Muda yameshatandikwa NATO na Ukraine soldiers wanapata kichapo kikali , yaani NATO na Ukraine soldiers ni kama wako kwenye banda la kuku, hawatoki, chini artillery na machine kali za AK 47, juu Fighter jets SU-34, na drones majeshi ya NATO na Ukraine hawana pa kujificha maana ni sehemu ya mashamba ya ngano na misitu tu.
 
NATO na USA hawamwezi Russia, Russia ana makombola zaidi ya 6000+ ya nyukilia wakati huo NATO na USA wanamakombola 5000 combine, hivyo NATO na USA kuivamia Russia hiyo suicide mission hakuna mtu wa kusalimika uko Ulaya na Marekani. Ukiongeza na makombola 1000 ya China, hapo NATO na USA watakuwa wanabweka tu. Tayari Russia ameshatega makombola yake kwenye miji mikuu karibu yote ya NATO na USA, ndo maana juzi kati Putin alikuwa anasema NATO wanapofanya upuuzi wao waangaliye population ya miji mikuu yote ya Ulaya NATO na USA maana hakuna mtu wa kusalimika.
 
Baada ya muda NATO na Ukraine soldiers wataisha hapo Kursk. Front line imeshakatwa. Hii mbinu ni sawa na aliyotumia brigadier Warden, Major general Mayunga aka Kambale kipindi cha vita ya Kagera, wanajeshi wa Uganda waliokuwa upande wa Tanzania walizungukwa wakajikuta hawana Cha kufanya bali kusalimu amri. Sammy ni mkoa wa Ukraine uko mpakani na Russia, na ndo supply route yao, majeshi ya Russia wameshakata hiyo supply chain kila siku ndege za Russia na drone zinaruka na kupiga kila kitu kichotembea.
 

Attachments

  • Screenshot_20240824-184228.png
    58.3 KB · Views: 1
  • Screenshot_20240823-210917.png
    442.5 KB · Views: 1
  • Screenshot_20240823-210757.png
    342.2 KB · Views: 1
  • Screenshot_20240823-210206.png
    515.1 KB · Views: 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…