LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
''Urusi inapigana na NATO'' umetumia vigezo gani kusema hivyo? Mimi pia sikubaliani na nchi za magharibi kwa vitendo vyao dhidi ya urusi, lakini siwezi kupuuzia nguvu ya NATO kijeshi, NATO Bado haijaingia vitani na Urusi
Duuh we kiboko ,
Wakati SMO inaanza majeshi ya URUSI yalifika mpaka miji mingi mikubwa na kukaa kwa muda.Ilikuwa ni makubaliano ya TURKEY ,ISRAEL na RUSSIA ndio yaliyowashiwishi RUSSIA kuondoa majeshi kwa makubaliano ya mazungumzo ya amani.Lakini ni NATO waliotibua mazungumzo na kumuahidi Zelensky msaada mkubwa wa kijeshi kuhakikisha wanamshinda RUSSIA. Katibu mkuu wa NATO tokea mwanzo anazungumza kushindwa UKRAINE katika hii vita ni kushindwa kwa NATO.Dola bilioni 150 zimeshatumika UKRAINE.
 
German Defense Minister Pistorius: International law allows deep attacks into Russia that has invaded another sovereign country.
Pistorius said the United States and Britain were free to β€œdecide this way” regarding the weapons they supplied to Ukraine. β€œInternational law allows this,” he said and asked not to be afraid of Putin’s threats
 
Mkuu kwa kifupi Mimi sidanganyi Bali nimeeelza kulingana na ukweli na Hali halisi ilivyo huko Ukraine na Urusi.
Kudanganya ni kuongea vitu ambavyo havipo kabisa kwa sababu ambazo mtu anazijua.
Kwa mfano naweza kudanganya kwa kusema Tanzania imewahi kupigana na Zambian wakati ukweli Tanzania haijawahi kupigana na Zambia,huo ndio uongo.
Lakini kuhusu NATO dhidi ya Urusi hayo ni mawazo na hoja zangu nilizozifanyia utafiti
Na kwa destiri hoja hujibiwa kwa hoja na tafiti hupingwa kwa tafiti.
Halafu umesema kua mbona Kila siku nairudia hoja hiyo?
Nairudia hoja hiyo Kwa sababu ndio jibu halisi na kwa kawaida jibu halisi hua halibadiliki kwa maana ukweli hubaki kama ulivyo.

Umesema kama NATO ingekua inapigana na Urusi basi tungeona makombora ,silaha na ndege kama F35 na F 57 zingekua zinapambana huko ulaya.

Iko hivi,
Vita huanza kidogokidogo hata vita hii ilianza kidogokidogo imebadiloa sura Hadi Sasa ukraine imevamia kursk na itabadikiaka zaidi.

Hivyo kama busara na hatua za amani zisipochukuliwa mapema na haraka tutashuhudia hizo silaha ulizozitaja zikitumika kishambuliana kati ya NATO na Urusi.
Haita chukua muda nyukilia zitaingia kwenye matumizi.
Tusiombe tufike huko.
Kosa moja Dogo TU linaweza kulipua vita ya tatu ya Dunia.
Mfano mdogo TU,kama Ukraine akipiga ndani ya Urusi kwa kutumia silaha za NATO,hapa watakua wamevuka mstari mwekundu aliochora urusi.
Usitegemee Urusi itakaa kimya.


Umenituhumu nadanganya.
Mimi sidanganyi wala sisemi uongo Bali natoa mawazo yangu kulingana na facts zulizopo na maoni ya military analyst wakubwa hapa duniani.
Kudanganya ni kuelezea kitu ambacho hakipo kwa maslahi Fulani ambayo Mimi Sina.
 
Sawa, umefafanua vyema kulingana na jinsi ulivyouelewa huu mgogoro, Sasa tusubiri hizo silaha zitakapoanza kutumika ndani ya urusi tuone vita vitachukua sura ipi..
 
Yaani mpaka sasa haujui kuwa kuna makombora maalum kwa ajili ya kugonga satellite ?
Yalishatumika yakapiga satellite ipi??? Yaani watengeneze wao, wajaribu wao na taarifa ya mafanikio waitoe wao wenyewe HALAFU MNAKUJA KUAMINI. Mimi kuhusu suala la kutengeneza sikatai ila ninachohoji ni EFFICIENCY YAKE.
Tuliaminishwa sana kuhusu defence systems za Urusi kuwa zinaona hadi nzi na mbu lakini leo hii tunashuhudia jinsi Ukraine anavyotuma Drones hadi Moscow na kupiga.
Sio kwa Russia tu lakini pia tuliaminishwa kuwa Israel ana defence system matata sana lakini mbona Hamas, Hizbullah na Iran wameweza kutuma makombora na mengi yakafika tena ya speed ya kawaida tu tofauti na yale ya hypersonic kama ya Mrusi. Ni kama tulivyoaminishwa kuhusu mfumo wa ulinzi wa USA pamoja na ndege zake za F16, F22rapter na F35 kuwa haviwezekaniki.

Hawa wakubwa wote wa dunia wana mambo mawili .1. Vitisho 2. Biashara

MIMI NITAAMINI SIKU NIKISIKIA SATELLITE IMEPIGWA NA KUHARIBIWA. NA NINAMSHUKURU MUNGU KWA KUNIPA AKILI KUBWA YA KUCHANGANUA MAMBO. SIDANGANYWI kama wengi wenu humu. Halafu hii vita ya Ukraine IMEWAUMBUA WENGI SANA NA BADO HAMBADILIKI.

Tuliozaliwa zamani tunakumbuka mengi kwenye vita ya Iraq ambapo kama kawaida yetu wabongo ni kulipa sifa zisizostahili kombora la Scud
 
Wewe sawa kama mimi. Wanasiasa ni watu wabaya sana.
Rais Zelensky anaongea propaganda ili aonekane anahimili vita ila kiuhalisia vita imemuelemea.
Kuna chombo cha habari nilitizama kama sio cha CGTN basi kimoja wapo cha USA kinaonesha jinsi raia wenyewe wanavyowageuka askari wao wa Ukraine.
Raia wana hasira kwamba kaka zao,baba zao na wame zao wanavamiwa hadi majumbani na kupelekwa jeshini kinguvu wengi hawana hata afya ya kupigana.
Hii imewapa raia wa Ukraine hasira dhidi ya jeshi lao.
 
Technology hiyo tayari Urusi wanayo mkuu,dah,jielimishe,upo nyuma sana kielimu.
Mimi kichwa changu kikubwa sana tofauti na wengi wenu humu ndio maana hamtanielewa. Ni kama kabla hata ya mgogoro wa Ukraine nilivyokataa kuamini kuwa Russia haiingiliki eti sababu ya Defence systems zake za S400 na S500. Mlisema hata jiwe likirushwa linadunguliwa , mimi nilikataa lakini kama kawaida yenu nyie mkawa mnaona mimi sijui.

SIKU IKATOKEA SATELLITE IMEPIGWA UNITUKANE KWA KUNIITA MWIJAKU
 
Mzee hii copy na paste unataka tuisome yote kweli
 
Mkuu mbona jambo dogo hilo halihitaji akili kubwa!??
Kwani ni technology gani imetumika kuipandisha satellite huko juu!?
Technology hiyo hiyo iliyotumika ndio hiyo itakayotumika kurusha vilipuzi hadi kuilipua hiyo satellite.
 

Mkuu Muite,
kwanza kabisa naomba nikusahihishe kidogo kuhusu tamko la Putin kuhusu nchi yoyote kuisaidia Ukraine.

Ni kweli Putin alitoa tamko hilo akimaanisha nchi yoyote au kikundi chochote mfano wa NATO wakiingia kuisaidia Ukraine atawapa vita ambayo hawajawahi kuishudia katika maisha Yao.

Ukweli ni kwamba onyo hilo la Putin limeheshimiwa na limefanikiwa.

Limefanikiwa kwa sababu hakuna hata nchi moja ama kikundi kama NATO ambacho kimeingia moja Kwa moja kijeshi kuisaidia Ukraine.
Zaidi wameingia kwa kujificha kivulini na mgongoni mwa Ukraine kinyonge zaidi Kwa kutoa misaada ya fedha na silaha isivyo kawaida Yao kama walivyozoea kuingilia kijeshi rasmi kwa kutangaza rasmi kwamba wanaenda kuisaidia nchi Fulani,kama walivyofanya kuipiga Iraq baada ya kuivamia Kuwait,
Kama walivyoisaidia Kosovo dhidi ya Yugoslavia,
Kama walivyoingia rasmi kuwapiga Al-Qaida na Watalabani huko Afghanistan,kama walivyoenda kuyapiga majeshi ya Libya yaliyokua yanamuunga mkono Col Muammar Gaddafi,kama melivita za USA UK na ufaransa zilivokua zikishamulia vituo vya jeshi la Syria na kama walivyokua wakidungua makombora na droni za Iran n.k.
Hadi Leo hakuna nchi yoyote imefnya hivyo kwa Ukraine Kwa sababu wanaogopa majibu ya Urusi.
Nasisistiza Tena NATO wanapigana na Urusi Kwa kificho hivyo Urusi inakosa uhalali wa kisheria kuzishambulia nchi zinazoisaida Ukraine.

Nakuambia hivi NATO ama nchi yoyote wameshindwa kuingia RASMI kama walivyoingiawa

Iraq dhidi ya Kuwait,
Afghanistan,
Libya na
Yugoslavia.

Hivyo alichokua anakisema Putin ni onyo kwa nchi yoyote itakayojiingiza moja Kwa moja kivita kama nchi za NATO zilivyojiingiza kwa Iraq,Libya, Afghanistan na Yugoslavia.
Kama waliweza huko wanashindwa Nini kwa Ukraine?
Mbali na hiyo mbona Ukraine kawaomba waweke no fly zone lkn wamekataa?
Mbona Libya na Serbia waliweka?

Hiyo ilikua miaka mingi sana.
Juzi hapa USA UK na France waliweza kudungua makombora na droni za Iran zisipige Israel,
Ukraine na yeye kawaomba NATO na west wamsaidie kuyadungua makombora ya Urusi wamekataa.
Wamempa ndege za F-16 lakini hawataki kuziweka kwenye viwanja vya ndege vya nchi za NATO.
Mkuu wameshindwa kufanya yote haya ni kwa sababu ya maonyo na Putin.

Mkuu Sasa nije kwenye makombora ya Urusi yenye kuweza kuzifuta nchi kama ufaransa na eneo kama Jimbo la Texas.
Hapa sintasema mengi.
Ukweli ni kwamba naona makala umeisoma,na Mimi nimeisoma,Sasa Mimi ni nani hata nisiamini wakati vigezo vya kisayansi vinaonesha kua uwezo huo upo?
Kwa Nini nisiamini Ikiwa Hiroshima na Nagasaki zilfanyiwa maangamizi makubwa mno miaka mingi iloyopita wakati sayansi na teknolojia ilikua chini kuliko Sasa hivi?
Na bomu hilo lililotumika likua halina nguvu kama mabomu ya nyukilia yaliyopo Sasa hivi,yanayomilikiwa na akina India Pakistan china UK France Korea kaskazini Israel USA na Urusi.

Kitu kingine kinachonifanya niamini ni madhara yaliyotokana na kuvuja TU kwa mionzi ya nyukilia kutoka kinu Cha nyukilia Cha USSR huko Ukraine katika mji wa Chernobyl,madhara ya kuvuja mionzi TU yalikua ni makubwa haijawahi kutokea hapa duniani,kiasi kwamba mamlaka za Dunia zililitangaza tukio hilo kua ni ajali kubwa zaidi kuwahi kutokea duniani toka kuumbwa kwa Dunia hii..

Naamini makala hiyo Kwa sababu nchi zote kubwa duniani zinamiliki nyukilia kama silaha ya mwisho na zinazizuia nchi nyingine zisiwe nazo.
Kumbuka silaha za nyukilia zinaweza kua zinafanana lkn zinazidiana uwezo,na kaa ukifahamu kua Urusi wako mbele sana kwenye sekta ya nyukilia.
Sababu ya mwisho inayonifanya niiamini habari hii, ni kua hakuna hata mwanasayansi mmoja wa masuala ya nyukilia, kutoka Magharibi wala mashariki aliepinga uwezo huo.
 
Mkuu mbona jambo dogo hilo halihitaji akili kubwa!??
Kwani ni technology gani imetumika kuipandisha satellite huko juu!?
Technology hiyo hiyo iliyotumika ndio hiyo itakayotumika kurusha vilipuzi hadi kuilipua hiyo satellite.
πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘βœ”οΈβœ”οΈβœ”οΈβœ”οΈβœ”οΈβœ”οΈβœ”οΈSwadakta.
 
Mkuu wala sisi wengine hatukudharau,utamdharauje mtu usiemjua?
Sisi tunachoomba wewe mwaga material facts humu watu tutoe tongotomgo.
Karibu Mkuu,
Tiririka mwamba.
 
mbona ya kawaida sana hayo ,hayana game change unapombambana na NATO au CHINA
Mkuu umejibu visivyo.
Yule jamaa aliekuambia Urusi ana makombora mengi ambayo bado hayajatumika of course sikujua ana maanisha aina au idadi.
Ila Mimi nikaweka aina ya makombora hayo kua bado hayajatumika kwenye vita ya Ukraine.
Sijasema yata change vipi game baina ya Urusi wakipambana na NATO au china.
 
Mkuu, Putin hana jipya; nadhani unakumbuka alisema operation hiyo ingemchukua just a week na atakaye ingilia atambamiza vibaya sana, leo ni zaidi ya mwaka, yupo yupo tu.
 
Kursk direction. The Armed Forces of Ukraine are approximately 700 meters from the Tyotkino village municipality building and continue to advance. Russian soldiers who don't flee will be eliminated.
 
Russia ni nchi pekee yenye makombora ya kutungua satelite.Walizindua miaka miwili nyuma na yana indefinite flight time,nikimaanisha chanzo chake cha nguvu ya kuyasukuma ni endelevu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…