Jasmoni Tegga
JF-Expert Member
- Oct 28, 2020
- 13,481
- 26,392
Kumweka Trump na vita kwenye sentensi moja ni kumkosea sana. Huyo jamaa alitolewa kwa figusu 2020 kwa sababu hakutaka kuingiza nchi kwenye vita.Vyovyoye atakavyofanya Trump Hana Cha kuitisha Urusi.
Kama ni vikwazo Urusi keshavizoea,
Kama ni vita Urusi Iko tayari Kwa hilo .
Akitaka kuingia vitani na Urusi ajiandae Kwa vita vya nukes.
Alishindwa kumpiga kiduku atamweza Putin?
Hata hivyo Trump sio mpenda mavita .
Trump anaweza kutishia vita dhidi ya maadui wake, lakini kamwe hawezi kuwaingiza watu vitani. Anaweza kumchapa Solemani pale Irani, lakini hawezi kamwe kuingia vitani. Anaweza kumkoromea Kiduku na kumwita mbilikimo, lakini hawezi kuzichanga naye.
Hiyo ndiyo sayansi na sanaa ya maridhiano katika medani za siasa. Bila kuonesha nguvu, huwezi kulipata jukwaa sahihi la kukaa meza moja ya mazungumzo ili kuzuia hatari kubwa zaidi mbeleni.
Joe Biden angekuwa mwenye maamuzi binafsi, kamwe Putin asingeingia Ukreni kuivamia. Na wala tusingekuwa na timbwili la Mashariki ya Kati. Maisha ya watu wengi mno yasingepotea bure!
Kitendo cha viongozi hao kushikiwa akili na watu wachache wapenda-vita na wanaojinufaisha kwa machafuko duniani, ndicho kimezitumbukiza nchi mbalimbali katika mtafaruku mkubwa, mdororo wa kiuchumi na umaskini hadi sasa.