LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
Urusi ndiye anayeipa teknlojia North Korea. Na North Korea ni jirani wa US.
Umejichanganya kabisa Kaka.

North Korea ni adui mkubwa sana wa USA, labda kama ulikuwa unataka kusema South Korea hapo sawa.

Lakini North Korea Mdau wake mkubwa ni Urusi, China, na Muiran.

Muiran ni sababu ya kutoelewana kwake kabisa na USA ndiyomaana naye kaamua kujiunga na URUSI, CHINA na NORTH KOREA akiamini siku yoyote USA akizingua Taifa lolote mojawapo na hayo basi naye atayaunga mikono kama ilivyo kwa USA kuungwa mkono na UK, FRANCE, na GERMAN.
 
Urusi ana sababu nyingine kuivamia Ukraine, hiyo ya NATO ni mojawapo
Hivi Ukraine si ni nchi huru?
Sasa mbona kama Russia anawapangia wenzie? Kwani ye hofu yake nini km NATO wakiweka hizo silaha huko Ukraine? Ye si anasifiwa ana nguvu za kivita,na jeshi nk!

Basi km ni hivyo anawaogopa NATO
 
Kwani mie nimesemaje hapo huu kaka nimesema urusi wana Deposit ya Rasmali na Technology-sasa huyo hata ukimwekea vikwazo ni sawa unajitekenya mwenyewe.
How unajitekenya ? Hapa ndio vina work vizuri kwa sababu ni maskini tuu.
Bado anauza raw materials ku survive,ukisema havitafanya Kazi ni useless..

Russia kwanza hata hata ubavu wakupigana na Iran nje ya nukes,hana.
 
Kwahiyo Putin ashindwe vita ili hali ana silaha ya nuclear?
Hii vita atashinda na atashindwa!!
Atashinda kwa maana anaweza kubadili uongozi wa Ukrain.
Atashindwa kwa maana huyo 'atakaemuweka' hataungwa mkono na wananchi wa Ukrain.
Nyuklia kwa sasa hazina nafasi, kwa vita hii.
 
Utamuuzia nani?
Kwani mmoja ya sababu ya Nchi za Ulaya kupuyanga puyanga kwenye issue hii ni kutokana na kwamba Ulaya inaihitaji Urusi kuliko Urusi anavyo ihitaji yeye.Pia bado kuna Nchi nyingi hazafungamana na NATO.
Population ya China+India tu ni zaidi ya 36% ya Watu wote Duniani,hii ni karibu Nusu ya watu wote Duniani-hili ni soko zuri na wote wana mashirikiano mazuri na Urusi.
 
Hivi hizo kilometa 10,tulizoambiwa bado hazijaisha tu?
Hapa uliuliza jana, ila hadi sasa hazijaisha. Tukiwaambia Russia imeonesha weakness wanaleta visingizio. Imagine Russia inamiliki anga la Ukraine, imeshambulia airbases na inafly air sorties free bila upinzani ingawa inasemekana (sijapata ushahidi wa picha, ndege kubwa haipotei tu hewani ilidondosha) Ilyushin Il-76 transport aircraft imedondoshwa jana na inasemekana ilikuwa na wanajeshi. Nimeona clip yenye roud bang na explosion na debris kubwa zikidondoka ila hakuna ushahidi kama ni transport aircraft, yaweza kuwa jet ilikuwa na mabomu mengi.

Russia inamiliki bahari nzima kuzunguka Ukraine inafyatua makombora ikijisikia, inafanya cyber attack kutokea Belarus. Kwenye ground ambako Russia ndio huwa ina nguvu sana bado inapata upinzani mkali. Sasa imagine uikutanishe na nchi zenye Navy, Airforce na cyber warfare imara. Achana na nuclear weapons hapa hazina matumizi
 
Unakitaka kujuwa nguvu za Russia
Nadhani Russia yuko peke yake anapigana ila upande wa pili wamejikusanya kijiji halafu unataka kufananisha? Ok una maanisha Russia vs Finland au Russia vs Poland nadhani jibu utakuwa nalo ila hawa nchi zote wamejiunga pamoja NATO plus USA ili kumkabili Russia tu mtu mmoja vs Kijiji. aje mmoja mmoja kama mwezi tu Russia hajabeba sijui Estonia, Belgium,,,,,
 
Hii vita atashinda na atashindwa!!
Atashinda kwa maana anaweza kubadili uongozi wa Ukrain.
Atashindwa kwa maana huyo 'atakaemuweka' hataungwa mkono na wananchi wa Ukrain.
Nyuklia kwa sasa hazina nafasi, kwa vita hii.
Swala la kuungwa mkono sio issue,hata hapa kwetu sidhani kama viongozi wa CCM huwa wana shinda but at the end huwa wanaongoza.Lakini pia Urusi bado ana option ya kuichukui Ukraine nzima na kuifanya sehemu ya Urusi.
 
Nadhani hawakutarajia upinzani, walijua watajipigia kiulaini
 
Asante kwa Nakala hii umenifundisha sana.Nitaitaji kujua zaidi.
 
Nyerere alitufundisha kuuchukia ubepari na kuuona ni kama ushetani. Akasahau kwenye nchi za Kibepari ndio kuna haki za kiraia kuliko hata nchi za kijamaa.

Ma nchi ya kijamaa ni ya ovyo sana. Unaenda kuanzisha vita kwa sababu zisizo na kichwa wala miguu. Warusi wapuuzi kabisa.
 
Sio chadema wala act wazalendo hawqjakemea mambo ya hovyo yanayoendelea ukrane
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…