Wanajaribu kuishusha bila mafanikio nahisi mtambo mpaka unaishiwaRussian airforce dominating the Ukraine's air.
#Leteni vivid videos maana naona huu uzi umejaa maneno mengi pasipo video au picha zenye uhalisia.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanajaribu kuishusha bila mafanikio nahisi mtambo mpaka unaishiwaRussian airforce dominating the Ukraine's air.
#Leteni vivid videos maana naona huu uzi umejaa maneno mengi pasipo video au picha zenye uhalisia.
North Korea anayo 40-50(nuclear bombs)Ni kweli Urusi ina Nguvu kubwa Sana za Kijeshi Tena Sana. Lakini hawezi hata siku moja kuthubutu kutumia kombola la Nyuklia kwenye Vita. Kombola la Nyuklia ni kwa ajili ya Duterrence(Kutishia). Kinachosababisha mpaka Sasa NATO washindwe Kuingia vitani kuisaidia Ukraine ni kwasababu Russia ana Nyuklia Waepons ambazo zikitumika Basi NO WINNER,All are LOSSERS.
Urusi ina Makombora 7500 ya Nyuklia kwa takwimu za NIT. Makombora 2500 yako tayari kufyatuliwa kuelekea Endeo lolote Lile Duniani litakapotumwa. Marekani ina Miji mikubwa 358 na Majimbo 54. Kombora Moja linaugeuza mji kuwa Majivu kabisa. Kama Mrusi akituma Makombora yote 2500 kuelekea Marekani,Basi ndani ya dakika 30 hakutakuwa na USA Duniani.
Kwa Upande Mwingine,Marekani ina Makombora ya Nyuklia 6800. Kati ya hayo, 3500 yako tayari kufyatuliwa ndani ya Dakika 5 wakipokea Order na Direction ya kuyafurumusha. Urusi ina Miji mikubwa 43. Endapo USA akiona Russia kashatuma Makombora Yake kuelekea Marekani na hakuna jinsi Basi ndani ya Dakika 5, Makombora 3500 ya Marekani yatakuwa njiani kuelekea Urusi kuteketeza Miji 43,Ndani ya Nusu saa hakutakuwa na Urusi Tena. Hiyo inaitwa MUTUAL ASSURED DESTRUCTION(MAD).
Haya Sasa,Tuseme wewe ni Raisi wa Russia,utarusha hayo Makombora kuelekea Marekani au utafanya juhudi za majadiliano?
Mwishoni mwa Vita baridi kabisa (1988) Nchi za Marekani na Urusi Zilikuwa na Akiba ya Makombora 127,000 (Laki moja na elfu ishirini na Saba). Kati ya hayo, 58,000 ya Urusi na 69,000 ya USA. Embu fikilia. Kombora Moja linafuta mji mmoja wa Dar. Je,Dunia ina Miji 127,000? Jibu ni Hapana.
Kwahiyo ndugu yangu usiwe na tempa unapokuwa unachangia hizi maada,tumia Logic utaelewa tu.
Urusi na Marekani wanajuana,wakikutana Anga Furani Kila mmoja anaangalia Nani anamaslahi makubwa na anamwachia ili kuepusha Vita.
Georgia Mwaka 2008 Marekani hakuingiza mguu kusaidia Nchi hiyo dhidi ya Uvamizi wa Russia kwasababu Marekani anajua hapo Russia ana maslahi Makubwa.
Iraq mwaka 2003 Russia hakutia Mguu kwasababu Marekani alikuwa na Maslahi Makubwa.
Libya mwaka 2011 Russia hakutia Mguu kwasababu USA alikuwa na Maslahi Makubwa.
Venezuera Marekani aliogopa Msululu wa wakimbizi kumiminika nchini Marekani hata Kama angeliamua Vita Urusi angelipisha Coz pale ni Maslahi Makubwa ya kiusalama kwa USA.
Syria pale Wote Urusi na USA wanamaslahi na ndio maana mpaka Sasa wameigawana kijanja. Urusi inamhitaji Assad kwasababu Anamdai pesa ndefu. Marekani anahitaji Mafuta ndio maana mpaka leo Majeshi ya Marekani yapo Syria kulinda Visima vya Mafuta.
Kuhusu Ukraine,hata Marekani anajua kabisa Maslahi ya Urusi ni Makubwa kwahiyo lazima akae pembeni. Atashiriki tu kijanja lakini sio moja kwa moja.
Kuhusu NORTH KOREA,Yeye Ana Mabomu 10 TU ya Nyuklia kwahiyo hata akiacha atupe Mabomu yake Marekani atateketeza Miji 10 ya Marekani Kati ya 358. Kwa upande mwingine,NORTH KOREA ana miji 7 Mikubwa. Marekani akituma Makombora Yake ya Nyuklia 3500 nadhani unaona kabisa Makombora Mengine hayana pa Kupiga kabisa.
MTz 255Dar.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Kuna mipaka yetu ina matatizo madogo madogo ,wanajeshi wanatumia nguvu kuhakikisha tupo salama. Hawa wataalam inabidi max asaidie watambulike kuisaidia nchi kimkakati.
Nasikia satan bado kalala ndaniKwenye historia yooote ya URUSI hakuna vita wamewahi shindwa? unazungumzi toka mwaka gani mpaka mwaka gani kwa mfano? kwa mfano hii vita inaitwa "first chechen war" alishinda au alishindwa? na hii "soviet-afghan war" urusi alishindwa au alishinda? na hii spanish civil war urusi alishindwa au alishinda?
Mturuki na russia ni marafiki. us alitaka aweke kibarakaka chake akashindwaHii habari ya zuio la Black Sea ina mkanganyiko kidogo, maana rais wa Ukraine ameisema kama request muda mfupi uliopita. Imezua mjadala maana kuna vyanzo vingine vinadai kuwa Uturuki haijathibitisha kufanya hivyo.
Sasa lengo halijatimia Hadi sasaKumbuka lengo lake ni kuonesha mobilization
Kwenye Vita kunapropaganda sana na muda mwingne kujua tarifa ipi ya kweli au uongo ni ngumu.MilardAyo nae kapost eti Warusi 3500 na nyungo zao 34 wamededishwa
Hata kama imechukuliwa , Hilo najua, je kule yeye alichemsha maandazi au Nyuklia? Hitler ilibaki kidogo ateke Urusi yotechenobyl ishachukuliwa mkuu ipo chin ya russia upo dunia gani
Huyu alikuwa kashiba...Yaan TZ tunamzidi NORTH KOREA?? are you serious mkuu?? Sisi tunaweza kujiendesha bila misaada??
Hawawezi kwa sababu ana nuclear Putin na Sasa Hivi Putin yupo full crazy .Putin is isolated now and that is dangerous he can go to world war 3 cause he is crazy now .Nimeona twitter kuwa moscow inasambaratika baada ya kuangushiwa nuc bomb?
Na ana ambition ya kuja kuwa RaisKumbe huyu former boxer Vitali Klitschko ndio Meya wa Kiev!?nimemsikia atoa tangazo kwamba atakayetoka usiku baada ya muda wa zuio atachukuliwa kama ni aduiView attachment 2132007View attachment 2132008
Asante Sana kwa hii habariSalaam Wakuu,
Thread hiiya Mwendelezo, itatumika kuangazia hali ya Usalama na matokeo yake katika Nchi Mzozo wa Ukraine na Urusi.
Tuzujane hapa kianchojiri..
Mvutano kati ya Ukraine na Urusi umefika kiwango cha zaidi kwa miaka mingi, lakini juhudi za kidiplomasia pia zinafanya kazi kwa bidii kutafuta suluhisho la mzozo huo. Kuna masuala mengi nyuma ya mzozo huo ambao ulianza miongo kadhaa iliyopita na kuhusisha nchi katika eneo zima. Hapa tunaangalia kile tunachojua kuhusu mgogoro huo.
Ulianzaje?
Mizizi ya hatua ya hivi punde kati ya nchi hizo mbili inaanzia Oktoba 2021. Hapo ndipo uwekaji mkubwa wa majeshi ya Urusi kwenye mpaka wa Ukraine ulipoanza. Ripoti za picha za satellite na kijasusi zimefichua kuwa zaidi ya wanajeshi 100,000 sasa wako karibu na eneo hilo. Wizara ya Ulinzi ya Urusi pia imetoa picha za mazoezi ya kijeshi. Vifaa vinavyohusika ni pamoja na bunduki za kujiendesha, mizinga ya vita, magari ya mapigano.
Ukraine imeibua wasiwasi juu ya majeshi hayo ya Urusi karibu na mpaka wake ingawa serikali yake pia ilisisitiza kuwa haiamini kuwa Urusi bado iko katika nafasi ya kuchukua hatua za kijeshi.
Msimamo wa Urusi ni kwamba kutumwa kwao kijeshi sio tishio kwa Ukraine na inasema ina haki ya kufanya chochote inachotaka na jeshi lake ndani ya eneo lake. Wengine wanasema huenda likawa jeshi kubwa zaidi la Urusi lililopelekwa karibu na Ukraine tangu Vita Baridi.
"Ukraine inataka kuimarisha usalama wake kwa sababu inahisi shinikizo kubwa kutoka kwa jeshi la Urusi, kwenye mipaka na pia ndani ya eneo la Kiukreni katika sehemu zinazokaliwa za Ukraine," anasema Orysia Lutsevych, mkuu wa Jukwaa la Ukrainia Chatham House huko London. Na njia moja ambayo inatazamia kufanya hivyo ni "kupitia muungano wa pamoja na Nato," anasema Lutsevych.
Lakini Urusi inaamini kwamba uwezo wa kupeleka wanajeshi kwenye mpaka wake ni haki ya uhuru. "Wako katika eneo la Urusi, hakuna anayeiambia Marekani mahali pa kuweka vikosi vyake katika eneo la Marekani," anasema Elena Ananieva, kutoka Taasisi ya Ulaya (RAS) yenye makao yake makuu mjini Moscow. "Kwa mataifa mengine inapaswa kuwa sawa"
"Kama nchi za Magharibi zinavyosema, kila nchi ina haki ya kuchagua jinsi ya kulinda usalama wake." "Lakini, tatizo kuu kwa mtazamo wa Russia ni tishio la Ukraine kujiunga na NATO na miundombinu ya kijeshi ya Nato kukaribia Urusi," anasema Ananieva.
Hii inatupeleka kwenye swali letu linalofuata.
Je, NATO itajipanua zaidi na kuijumuisha Ukraine kama mwanachama mpya?
Kando kupelekwa kwa wanajeshi katika mpaka wa nchi hizo mbili kumekuwa na kutoelewana kwa kidiplomasia kati ya Urusi na muungano wa kijeshi wa magharibi Nato.
"Upanuzi zaidi wa Nato kuelekea mashariki na kupelekwa kwa silaha, ambayo inaweza kutishia Shirikisho la Urusi, haikubaliki," kulingana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov.
Urusi inapinga vikali uwezekano wa upanuzi wa Nato na inataka hakikisho kwamba Ukraine haitajiunga na Nato. Ni msimamo unaoshirikiwa na mshirika wake wa karibu China. Lakini madai haya yamekataliwa na Nato na nchi wanachama wake. Kwa sasa kuna nchi wanachama 30 katika Nato, lakini nchi nyingine zinaweza kujiunga. Ukraine si sehemu ya muungano bali ni 'nchi mshirika'.
"Jamii ya Kiukreni na vyama vya kisiasa vinaamini kwamba hakuna njia bora ya kulinda Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi kuliko kuwa sehemu ya muungano wa pamoja wa usalama," Lutsevich anasema lakini pia anaongeza kuwa uanachama wa Ukraine kwa Nato unaweza usitokee katika siku za usoni.
Huko nyuma katika miaka ya 1990, baada ya kumalizika kwa Vita Baridi na kuanguka kwa Muungano wa Kisovieti, Nato ilitafuta njia za kujenga uhusiano wa karibu na mataifa mapya ya Ulaya ya Kati na Mashariki yaliyojitegemea.
Huu ndio wakati muungano huo ulipopanuka kuelekea mashariki zaidi, kumaanisha uwezo wake wa kijeshi na silaha umekaribia mpaka wa Urusi.
Kwa miongo kadhaa Kremlin imedai mara kwa mara kwamba nchi za Magharibi zilivunja ahadi ya kutopanua Nato. Madai hayo yanarejelea mazungumzo ya mwaka 1990, kati ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani James A. Baker na kiongozi wa zamani wa Usovieti Mikhail Gorbachev.
Lakini viongozi wa Magharibi hawakubaliani na kusema hakukuwa na mpango wowote rasmi kuhusu kutopanua Nato hadi Ulaya Mashariki zaidi na kwamba muungano huo unashikilia 'sera ya mlango wazi.'
Ikiwa Ukraine itakuwa mwanachama wa Nato (kwa sasa haijatuma maombi ya uanachama), "italeta tishio zaidi kwa Urusi" kulingana na Rais Vladimir Putin.
Mnamo Novemba 2021, alisema kuwa uwepo wa Ukraine katika muungano, na uwezekano wa kutumwa kwa makombora yoyote ya masafa marefu yenye uwezo wa kushambulia miji ya Urusi au mifumo ya ulinzi ya makombora, sawa na ile ya Poland na Romania, itakuwa suala la "mstari mwekundu" kwa Moscow.
Lakini Katibu Mkuu wa Nato Jens Stoltenberg aliweka wazi kuwa "Urusi haina kura ya turufu au kusema" kuhusu uwezekano wa upanuzi wa muungano huo.
Akizungumza na BBC, mtaalam wa Urusi Ananieva, alielezea wasiwasi juu ya uwezekano wa upanuzi wa Nato. "Miundombinu ya NATO inasonga karibu na mpaka wa Urusi. Nato inapaswa kuzingatia kanuni ya kutogawanyika kwa usalama," alisema.
"Hakuna uwezekano kwamba Ukraine itakuwa mwanachama wa muungano. Nato inapaswa kufikiria mara mbili kuhusu usalama wake ikiwa Ukraine itakuwa mwanachama wa muungano."
Wakati juhudi za kidiplomasia za kutatua mzozo huo zinaendelea, utafutaji wa njia mbadala wa zabuni ya Nato ya Ukraine umeibuka.
'Finlandisation' ni nini na ina uhusiano gani na Ukraine?
Miongoni mwa viongozi wengi wa kisiasa wanaojaribu kutafuta suluhu la mzozo huo ni Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa. Kulingana na ripoti za vyombo vya habari alitaja neno la enzi ya Vita Baridi "Finlandisation" kwa waandishi wa habari wakati wa safari ya Moscow.
Iliripotiwa kwamba alipendekeza "Finlandisation ya Ukraine", kama sera iwezekanavyo ili kupunguza mvutano katika kanda.
Lakini baadaye, tarehe 8 Februari, Macron alikanusha kutoa maoni hayo yenye utata.
Neno hilo hurejelea hadhi ya Ufini kama jimbo lisiloegemea upande wowote wakati wa Vita Baridi. Nchi hiyo ilikuwa na mpaka mrefu na Muungano wa Sovieti lakini haikuegemea upande wowote.
Msimamo huu ulimaanisha kuwa Helsinki hangekuwa mwanachama wa Nato na Umoja wa Kisovieti haungeona Ufini kama tishio linalowezekana na Ufini ilitia saini mkataba mnamo 1948 na Moscow ilikubali kukaa nje ya Nato.
Hata hivyo, mkataba huo ulimalizika mwishoni mwa Vita Baridi na serikali ya Finland sasa inasema maamuzi kuhusu kujiunga na mashirika ya kimataifa kama vile Nato yanapaswa kuwa mikononi mwake pekee na si kwa nchi nyingine.
Ukraine imesema kwamba pia haitakuwa tayari kuambatana na sera ya "Finlandisation" ambayo ingezuia sera zake za kidiplomasia.
"Nadhani ni jambo lisilokubalika kabisa kwa Ukraine" Lutsevych anasema.
"Ukraine ilishambuliwa ilipokuwa nchi isiyoegemea upande wowote, na pili Putin haheshimu mamlaka ya Ukraine, iwe haina upande wowote au la.
"Ukraini inakataa wazo hili kwa sababu ni sehemu ndogo ya uwezo wa Urusi kudhibiti Ukraine."
Je, kweli Urusi inaweza kuivamia Ukraine?
Kwanza kabisa, Urusi imesema mara kwa mara haina mpango wa kufanya hivyo, lakini kwa baadhi ya taarifa hizi hazijawatia moyo. "Tayari wamevamia," anasema Lutsevych akirejelea mwaka wa 2014 wakati Urusi ilipotwaa rasi ya Crimea ya kusini mwa Ukraine, na kuwaunga mkono waasi wanaoiunga mkono Urusi walioteka sehemu kubwa za mashariki mwa Ukraine.
"Kuna zaidi ya watu 14,000 waliofariki, zaidi ya 33,000 wakiwa wamejeruhiwa vibaya sana. Jumuiya ya Ukraine tayari inalipa gharama kubwa kwa uvamizi wa Urusi."
Nato haikuingilia moja kwa moja katika mojawapo ya matukio hayo, lakini jibu la muungano huo lilikuwa kupeleka wanajeshi wa ziada katika nchi za Ulaya Mashariki kwa mara ya kwanza, zikiwemo Estonia, Latvia, Lithuania, Poland na Romania.
Nato pia iliimarisha ulinzi wake wa anga/uwezo wa polisi katika mataifa ya Baltic na Ulaya Mashariki.
Moscow inataka vikosi hivi vya ziada kuondolewa katika nchi hizo.
Lakini kwa sasa, Nato inasema haina nia ya kufanya hivyo.
Nini kitatokea sasa?
Juhudi za kidiplomasia za kutatua mzozo huo zinaendelea ili kufikia makubaliano ya amani na kupunguza mvutano huo. Mnamo tarehe 9 Februari, katika mahojiano na BBC, Balozi wa Urusi katika Umoja wa Ulaya, Vladimir Chizhoz aliweka wazi mapendekezo ya Urusi ya kupunguza mvutano kuhusu Ukraine.
Alionyesha kuwa Moscow inaweza kujibu vyema ikiwa Ukraine ingekuwa nchi isiyoegemea upande wowote. Hata hivyo, Ukraine na Nato hapo awali walisema hawako tayari kukubaliana na hili. Katika hatua nyingine ya hivi majuzi, gazeti la Uhispania El Pais lilichapisha waraka uliovuja wa Marekani ukieleza msimamo wake wa mazungumzo.
Katika waraka huo, ilisema: "Marekani ilikuwa tayari kujadili... ahadi za kujiepusha na kupeleka mifumo ya makombora ya kurushwa ardhini na vikosi vya kudumu na misheni ya kivita katika eneo la Ukraine."
Wanadiplomasia na viongozi wa Ulaya pia wamekuwa wakichunguza njia za kufufua mpango wa kusitisha mapigano wa 2015 kwa mikoa ya Ukraine inayodhibitiwa na watu wanaotaka kujitenga. Mkataba unaoitwa Minsk kati ya Kyiv na Moscow haujawahi kutekelezwa kikamilifu.
Mtaalamu wa Ukraine Lutsevych anasema "Kyiv hatakuwa tayari kutekeleza mpango huo isipokuwa kutakuwa na upunguzaji wa kasi na usitishaji mapigano." "Urusi inataka kutumia makubaliano haya kuunda klabu yenye silaha ndani ya Ukraine ambayo ina raia wa Urusi," anaongeza.
"Suluhu la mgogoro huo ni umoja wa Magharibi na Ukraine. Kilicho hatarini ni uhuru wa Ukraine."
NATO inatishia majibu gani?
Mnamo Februari 7, kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alisema katika mkutano na Rais wa Marekani Joe Biden kwamba Ujerumani 'imeungana' na Marekani katika kuweka vikwazo dhidi ya Urusi ikiwa itaivamia Ukraine.
Vikwazo vinavyowezekana vilivyopangwa vya Washington vitamaanisha kulenga benki kuu za Urusi na kupiga marufuku Urusi kutoka kwa mfumo wa malipo wa kimataifa wa SWIFT ambao ni muhimu kwa miamala ya kimataifa. Uingereza ilisema itawawekea vikwazo watu binafsi na biashara karibu na Kremlin.
"Urusi ilistahimili vikwazo vya Magharibi" anasema mtaalamu wa Urusi Ananieva alipoulizwa kuhusu athari zake kwa Urusi. "Imegeukia uingizwaji wa bidhaa kutoka nje. Katika baadhi ya sekta za vikwazo vya uchumi wa Urusi vimeongeza uzalishaji, na kilimo. Wakulima wangependa vikwazo vya Urusi virefushwe," anasema.
Nato haijapendekeza kuwa ingetumia nguvu za kijeshi kukabiliana na uvamizi wa Urusi. Ingawa mazungumzo ya kimataifa yanaendelea kwa sasa hakuna njia wazi ya jinsi pande hizo mbili zitakavyofikia makubaliano.
Nani mwenye uwezo iwapo vita vitatokea?
===
Tangu mwaka Mpya wa 2022 uanze,vyombo vingi vya kiusalama vya kimataifa vimekuwa vikiripoti juu ya tishio la nchi ya Urusi Kuvamia kijeshi nchi ndogo jirani ya Ukraine,ambayo zamani ilikuwa katika muungano wa umoja wa kisoviet (USSR),Kabla ya kusambaratika vibaya Sana kwa umoja huo mwishoni mwa miaka ya 1990.
Chanzo cha mvutano wa kijeshi kati ya Urusi na Ukraine na uwezekano wa vita kamili
NINI CHANZO CHA MGOGORO HASA?
Mnamo mwaka 2014, Urusi iliyafadhili kijeshi makundi ya vuguvugu Mashariki mwa Ukraine katika majimbo ya CRIMEA,DONBASS,DONETSK na LUHANSK ambayo wakazi wengi wa majimbo hayo wana asili ya Urusi na wanazungumza Kirusi kwa ufasaha.
Katika mapambano hayo,Majeshi ya waasi kwa msaada wa Urusi walifanikiwa kuyateka majimbo hayo kutoka kwenye mikono ya Serikali ya Kyiv. Jimbo la CRIMEA liliamua kuitisha kura ya maoni (Referendum) ya kujitenga na Ukraine na kujiunga na Urusi.
Majimbo mawili (Donestk na LUHANSK) yaliendeleza mapambano makali dhidi ya Majeshi ya Ukraine na kuchukua udhibiti KAMILI wa majimbo hayo. Katika Jimbo la DONBASS Majeshi ya Ukraine yalipambana Sana na hivyo waasi kushindwa kuliteka Jimbo Hilo kikamilifu.
MGOGORO KAMILI?
Tangu mwaka 2014,Ukraine ilianza kupokea msaada wa vifaa vya kijeshi kutoka kwa washirika wa NATO. Ikumbukwe kuwa,Ukraine sio mwanachama wa NATO wala Umoja wa Mataifa. Vifaa vingi vya kijeshi vilitoka nchi za Marekani,Uturuki na Uingereza. Jeshi la Ukraine liliimarika zaidi baada ya kununua DRONES za kisasa kutoka Uturuki.
DRONES hizi zinajulikana Sana hasa zilipofanya vizuri kwenye mgogoro wa kijeshi Kati ya Armenia na Azerbaijan. Mwishoni mwa mwaka 2021 mwezi Desemba, Majeshi ya Ukraine yalianza kuyateka upya maeneo ya DONBASS kwa kutumia mashambulizi ya Anga kutoka kwenye DRONES. Majeshi ya Ardhini ya Ukraine yakashinda Nguvu Majeshi ya waasi na kuliteka Jimbo lote la DONBASS. Baada ya ushindi huo wa Majeshi ya Ukraine katika Jimbo la DONBASS,ndipo Ukraine ikaanza mashambulizi ya Anga kwenye Jimbo la LUHANSK.
Baada ya Ushindi huo wa Majeshi ya Ukraine,ndipo Majeshi ya Ukraine yakaingia Frontline ili kuwasaidia waasi. Pia,kikundi Cha Majeshi ya kukodiwa kutoka Urusi maarufu Kama WAGNERS kiliamua kuanzisha mashambulizi dhidi ya Majeshi ya Ukraine. Hata hivyo,Majeshi ya Urusi,Waasi na WAGNERS kwa pamoja yalishindwa kudhibiti mashambulizi ya DRONES za Ukraine.
Tarehe 24 Desemba 2021, Majeshi ya Urusi yalianza kuingiza mifumo ya Ulinzi wa Anga-ANT AIRCRAFT MISSILES (S-300 na S-400). Ujio wa Mifumo hiyo ya Ulinzi wa Anga ulisababisha DRONES za Ukraine kushindwa kufanya mashambulizi ya Anga. Hali hiyo ilitoa upenyo wa Majeshi ya Urusi na waasi kuchukua udhibiti upya wa majimbo ya DONBASS na LUHANSK.
JE, ENDAPO URUSI IKIAMUA KUVAMIA NANI ATAIBUKA KIDEDEA?
Kutokana na Uwezo mkubwa wa kijeshi wa Urusi ukilinganisha na Ukraine,bila Shaka Urusi itaibuka kidedea na kuyateka maeneo mengi ya Ukraine Kama itataka hivyo. Ushindi huo wa Urusi hautakuja kwa urahisi,Urusi inaweza kushuhudia kulipuliwa kwa vifaru vyake vingi ambavyo vitaingia kwenye ardhi ya Ukraine kuliko vifaru 140 ambavyo Urusi alivipoteza wakati wa Uvamizi wa nchi ya GEORGIA. Hii ni kutokana na Ukraine kupokea msaada wa Siraha za kulipua vifaru (ANT-TANK MISSILES) Zaidi ya Tani 80 kutoka Uingereza. Mwaka 2014 Ukraine haikuwa na Siraha hizi.
JE,URUSI INAWEZAJE KUZUIA KUPOTEZA VIFARU VYAKE VINGI?
Kutokana na Ukraine kutokuwa na Mifumo ya Ulinzi wa Anga (ANT-AIRCRAFT MISSILES) ya Uhakika, Basi Urusi ana nafasi ya kutumia ndege za kivita kushambulia Mifumo yote ya Ukraine ya kulipulia Vifaru Kabla ya vifaru hivyo kuanza kuingia kwenye Ardhi ya Ukraine kwa Urahisi zaidi.
Kutokana na Ukraine kulijua hili,imeamua kupeleka Mifumo yake ya kulipulia Vifaru karibu na mpaka wa Poland upande wa Magharibi. Makombora haya yanaweza kushambulia vifaru vyote vya Urusi ambavyo vitaingia Ukraine upande wa kaskazini wa Ukraine kutokea Belarus. Je,Urusi ataweza kushambulia kwa ndege za kivita Mifumo hii ya Ukraine ya kulipulia Vifaru ambavyo viko kwenye mpaka wa Poland? Jibu ni Hapana.
Kwasababu Marekani imeonya kwamba, endapo ndege za kivita za Urusi zitakaribia kwenye mipaka ya NATO(Poland ni Mwanachama wa NATO) Basi Marekani hatasita kuzitungua ndege Hizo. Ikumbukwe kuwa, Mwaka 2017, ndege ya Kivita Ya Urusi iliyokuwa inafanya mission ya kuwashambulia waasi wa ISLAMIC STATE ilitunguliwa na Mifumo ya Anga ya Uturuki ilipokaribia Anga la Uturuki kwenye Mpaka wa Uturuki na Syria. Hili tukio liliharibu uhusiano wa kidiplomasia Kati ya Uturuki na Urusi.
PIA SOMA
1. Mzozo wa Urusi na Ukraine wafukuta zaidi
2. Historia Iliyojificha Kuhusu Ukraine na Urusi
===
UPDATESMarekani yadai ina orodha ya wanaopaswa kuuawa na Urusi itakapoivamia Ukraine
YALIYOJIRI FEBRUARI 21
Taarifa za kuaminika za Marekani zimesema Urusi inaandaa orodha ya watu watakaowaua au kupelekwa Kambini baada ya kuvamia Ukraine kutokana na mzozo unaoendelea.
Barua iliyotumwa kwa Umoja wa Mataifa (UN) imeonesha miongoni mwa wanaolengwa ni wapinzani wa Kisiasa, watu wa Dini na makabila ya wachache. Moscow imekanusha kuwa na mpango wa kushambulia Ukraine, lakini inatafuta hakikisho kwamba Ukraine haitajiunga na NATO.
YALIYOJIRI FEBRUARI 23Urusi kukabiliwa na vikwazo kutokana na mzozo na Ukraine
Urusi iko hatarini kukabiliwa na vikwazo kutoka Nchi za Magharibi kufuatia mgogoro unaoendelea kufukuta kati yake na Ukraine
Wakuu wa Umoja wa Ulaya, Ursula Von der Leyen na Charles Michel wamesema Umoja huo unatafakari kuwekea vikwazo Benki za Urusi zilizo na Matawi katika Majimbo yanayodhibitiwa na waasi wa Ukraine ya Luhansk na Donetsk. Hata hivyo, vikwazo hivyo vitahitaji ridhaa ya Nchi Wanachama zote 27
Bunge la Urusi limepitisha agizo la Rais Vladimir Putin kutambua Uhuru wa maeneo ya waasi Mashariki mwa #Ukraine, siku moja baada ya Rais Putin kulisaini na kuamuru Wanajeshi kuingia maeneo hayo
YALIYOJIRI FEBRUARY 24Ukraine yatangaza hali ya hatari
Bunge la Ukraine limepitisha azimio la nchi hiyo kuwa katika hali ya hatari kwa siku 30 kutokana na mzozo uliopo kati ya Nchi hiyo na Urusi.
Mamlaka nchini humo zimeruhusiwa kuzuia raia kutoka, kuzurura na kuzuia Mikutano ya Vyama vya Siasa na Taasisi kwa maslahi ya Taifa. Pia, Serikali imewalazimisha kujiunga na jeshi wanaume wote waliofikia umri wa kwenda vitani.
UN yaitaka urusi kuondoa wanajeshi Ukraine
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres amemtaka Rais wa Urusi, Vladimir Putin kurudisha Wanajeshi aliowapeleka Ukraine, akisema watu wengi wameshapoteza maisha na ni wakati wa kuipa nafasi Amani
Aidha, Rais Joe Biden amesema Urusi itabeba lawama kwa madhara yatakayotokea katika mzozo unaoendelea, akisisitiza Marekani pamoja na Washirika wake watajua cha kufanya
Papa Francis atangaza machi 2 kuwa siku ya kufunga na kuiombea Ukraine
Kufuatia kile kinachoendelea baina ya Urusi na Ukraine, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amesema hatari ya vita ilmesababisha maumivu makali moyoni mwake
Ametoa wito kwa watu wote kutumia siku ya Machi 2, 2022 ambayo ni Jumatano ya Majivu, kufunga na kuiombea Ukraine
Ripoti zinaonesha tayari Russia imeanza kuishambulia Ukraine. Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba amesema watashinda vita hivyo.
Putin: Atakayeingilia mzozo wa ukraine atapata pigo la kihistoria
Baada ya kutangaza mashambulizi dhidi ya Ukraine, Rais wa Urusi, Vladimir Putin ametoa onyo kwa Mataifa ya Magharibi kuingilia kinachoendelea baina ya Nchi hizo
Mara baada ya milipuko kuripotiwa katika Mji Mkuu wa Ukraine, Kyiv Putin alinukuliwa akisema, "Kwa yeyote atakayeingilia kutoka nje, atakutana na matokeo ambayo hajakutana nayo katika historia"
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliitisha Kikao cha Dharura mara baada ya Urusi kuanza mashambulizi
Watu 10 na wanajeshi 40 wafariki katika shambulio lililofanywa na Urusi
akriban Raia 10 na Wanajeshi 40 wa Ukraine wameripotiwa kuuawa katika mashambulizi ya Anga yaliyofanywa na Urusi leo Februari 24, 2022 katika Mji wa Odessa
Taarifa ya Vifo hivyo imetolewa na Msaidizi wa Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine alipozungumza na Waandishi.
Ukraine: Rais kumpatia silaha kila raia anayetaka kuipiga Urusi
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amewahamasisha Raia kuwa tayari kupigania Nchi yao, na kusema silaha zitatolewa mtu yeyote anayetaka kushiriki katika vita dhidi ya Urusi.
Kufuatia uamuzi wa Urusi kuvamia Ardhi yake, Ukraine imekatiza rasmi uhusiano wake wa Kidiplomasia na Taifa hilo. Picha kadhaa za Mitandaoni hivi karibuni zilionesha Raia wa Ukraine wakipewa Mafunzo ya Msingi ya Kijeshi taharuki ya mzozo huo ilipopanda.
Schalke o4 kuondoa nembo ya kampuni ya Urusi kwenye jezi
Klabu ya Schalke O4 imethibitisha kuwa itaondoa mara moja kwenye jezi zake nembo ya Kampuni ya Gazprom inayomilikiwa na Serikali ya Urusi
Kampuni hiyo inayofanya biashara ya mafuta na gesi ndio mdhamini mkuu wa klabu hiyo. Sehemu ilipokuwa inakaa nembo hiyo yatawekwa maneno yatakayosomeka ‘Schalke 04’. Hatua hii inakuja baada ya Urusi kuivamia na kuishambulia Ukraine kivita
UK: Mbunge ataka Abramovich azuiwe kumiliki Chelsea
Chris Bryant amehoji iwapo Roman Abramovich ataendelea kuwa mmiliki wa Klabu ya Chelsea huku akitaka kuzuiwa kwa mali zake kama sehemu ya vikwazo dhidi ya Urusi
Ameeleza kuwa Abramovich amewahi kukubali Mahakamani kuwa alihusika kulipa fedha kwa ajili ya ushawishi wa Kisiasa na kuwa ana uhusiano na Serikali ya Urusi
Wakati huo huo, taarifa zinaeleza kuwa Abramovich amezuiliwa kuishi Uingereza na maafisa wa uhamiaji wamepewa maelekezo ya kuhakikisha Abramovich hakai Uingereza
Hatua hii inakuja baada ya Urusi kuivamia na kuishambulia Ukraine kivita huku nchi kadhaa ikiwemo England zikiangalia namna ya kuiwekea vikwazo Urusi
YANAYOJIRI FEBRUARI 25
Mashirika ya ndege ya Uingereza yamepigwa marufuku kutua Urusi
Mashirika ya Ndege ya Uingereza yamepigwa marufuku kutua katika Viwanja vya Ndege vya Urusi pamoja na kupita kwenye Anga lake
Uamuzi huo unafuatia uamuzi wa Uingereza kupiga marufuku Shirika la Ndege la Urusi, Aeroflot kutua Nchini Uingereza. Marufuku ya Uingereza ni sehemu ya vikwazo vilivyowekwa ili kukabiliana na Uvamizi wa Nchini Ukraine.
UEFA: Fainali ya Klabu Bingwa Ulaya haitafanyika Urusi
Shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA) limehamisha fainali za michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kutoka Urusi kwenda Paris, Ufaransa baada ya Urusi kuishambulia Ukraine.
Fainali hiyo itakayofanyika Mei 28, 2022 itafanyika katika Uwanja wa Stade de France wa Ufaransa badala ya ule ulioko Urusi wa Gazprom Arena jijini Saint Petersburg.
Mara ya mwisho Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kuchezwa katika Dimba la Stade de France ilikuwa miaka 16 iliyopita wakati Barcelona ilipoifunga Arsenal.
Serikali: Watanzania walio Ukraine wawe watulivu
Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje imewataka Watanzania walioko Ukraine ikiwemo Wanafunzi, Wafanyakazi na Wafanyabiashara kuwa watulivu kipindi hiki cha mzozo wake na Urusi na kushauriwa kufuata maelekezo yanayotolewa
Wanafunzi wametakiwa kufuata maelekezo ya uongozi wa Vyuo, na kuendelea kuwasiliana na Ubalozi wa #Tanzania Nchini #Sweden kwa kuwa ndio unawakilisha Ukraine. Serikali inaendelea kufuatilia hali za Watanzania walio huko, ikielezwa hadi sasa hakuna aliyepata madhara yoyote.
Ukraine yaomba msaada wa majeshi yenye nguvu
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky ameomba Washirika wa Nchi za Magharibi waisaidie Nchi hiyo kukomesha mashambulizi ya Urusi
Amelalamika Mataifa yenye nguvu kuiacha Ukraine ijipambanie huku wakitizama kwa mbali. Amesema hata vikwazo vilivyowekwa havijamshawishi Rais Vladimir Putin kuacha kufanya mashambulizi
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Kwani watAnzania mnatka apigwe Nani!?Itakuwa umeona kwa kutumia jicho la chini
Hitler alivyo pigana na Russia akawakuta Russia wamejiandaa .Mpaka Sasa Hivi Russia wanahangaika kuchukia ukraine. It means Russian wali underestimate ukraine .Russians wao ndio wakuamua kumtoa madarakani na jeshi kuchukua nchi that will be niceNimeona twitter kuwa moscow inasambaratika baada ya kuangushiwa nuc bomb?