Mwl.RCT
JF-Expert Member
- Jul 23, 2013
- 14,624
- 20,666
Isiwe Poland ------ Poland,Kwa nini abadilishe
Bali iwe Russia ---- Poland
Rejea tittle yako
Breaking news 'Poland anataka ku vamia Poland' this may be world war 3 .Tuombe
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Isiwe Poland ------ Poland,Kwa nini abadilishe
Unajua Biden is compromised ana ukraine barisma hunter Biden na China 31 million dollar waliomlipa hunter .Democratic party climate change akakata pipe line ya USA akampa deal Putin Sasa hapo Biden watamuumbua wizi Naona ndio maana Hataki kuchukua mali za PutinHata White House ya Bush ilitaka regime change ilipoivamia Iraq kwa sababu za uongo.
America really doesn’t have a leg to stand on.
Huyu Puttin ni chizi na mashabiki wake mtajionea muda si mrefu kuwa jamaa hamnazo.Ata Kichaa kabla ajavuka Barabara huwa anaangalia usalama kwanza. Putin Hawezi kuingamiza Russia kwa ujinga kama huo
wewe unashabikia UKRAINE ivamiwe, ? nchi iliyo huru na ivamiwe tu?Taarifa zimekaa kiupande mmoja, vyombo vya habari havipo huru na hii inaonyesha kumbe kupitia dunia kweli ndio sio na sio ndio kweli. Ukrain wamevunja daraja ili vifaru vya urusi visiingie kwenye mji wa Kiev ila watachelewesha tu lakini lazima tuingie. Frontline commando wa Russian hata cm ya Putin hapokei kwa namna alivyo na midadi. Huyu mwamba alimisi sana vita yaani mda wote ana kiss russia flag ndogo aliyofunga kwenye mkono wake wa kuume.
Bora dini ya mizimu kuabudu Wafu kuliko dini ya mungu inayotengeneza wafu kila siku.WAKRISTU duniani wanataka UKRAINE ilindwe bila vita, WAISLAMU duniani wanashabikia URUsi iipige ukraine na kuiangamiza, ni ipi dini bora? wapagani wafuate dini ipi?
ipi inataka amani na upatanisho, madhehebu hayo kwa Afrika Mashariki hayajaonyesha mrengo wowote.
Ukrain ni kama mtoto ambaye wa darasa la sita anadai kuolewa,hivyo Urusi kama mzazi wa kiume lazima am-adabishe kwa kujua binti yake hajitambui. NATO walikubaliana na Urusi wasisogee jirani lakini vinchi vidogo vidogo vimechukuliwa na NATO na kwa namna jiografia ya Ukrain kwa Urus hata wewe usingekubali uache NATO waje kwa ukaribu huo. Urusi madai yake ni sahihi na USA na NATO na wapuuzi wengine wanajua hiliwewe unashabikia UKRAINE ivamiwe, ? nchi iliyo huru na ivamiwe tu?
Salaam Wakuu,
Thread hiiya Mwendelezo, itatumika kuangazia hali ya Usalama na matokeo yake katika Nchi Mzozo wa Ukraine na Urusi.
Tuzujane hapa kianchojiri..
Mvutano kati ya Ukraine na Urusi umefika kiwango cha zaidi kwa miaka mingi, lakini juhudi za kidiplomasia pia zinafanya kazi kwa bidii kutafuta suluhisho la mzozo huo. Kuna masuala mengi nyuma ya mzozo huo ambao ulianza miongo kadhaa iliyopita na kuhusisha nchi katika eneo zima. Hapa tunaangalia kile tunachojua kuhusu mgogoro huo.
Ulianzaje?
Mizizi ya hatua ya hivi punde kati ya nchi hizo mbili inaanzia Oktoba 2021. Hapo ndipo uwekaji mkubwa wa majeshi ya Urusi kwenye mpaka wa Ukraine ulipoanza. Ripoti za picha za satellite na kijasusi zimefichua kuwa zaidi ya wanajeshi 100,000 sasa wako karibu na eneo hilo. Wizara ya Ulinzi ya Urusi pia imetoa picha za mazoezi ya kijeshi. Vifaa vinavyohusika ni pamoja na bunduki za kujiendesha, mizinga ya vita, magari ya mapigano.
Ukraine imeibua wasiwasi juu ya majeshi hayo ya Urusi karibu na mpaka wake ingawa serikali yake pia ilisisitiza kuwa haiamini kuwa Urusi bado iko katika nafasi ya kuchukua hatua za kijeshi.
Msimamo wa Urusi ni kwamba kutumwa kwao kijeshi sio tishio kwa Ukraine na inasema ina haki ya kufanya chochote inachotaka na jeshi lake ndani ya eneo lake. Wengine wanasema huenda likawa jeshi kubwa zaidi la Urusi lililopelekwa karibu na Ukraine tangu Vita Baridi.
"Ukraine inataka kuimarisha usalama wake kwa sababu inahisi shinikizo kubwa kutoka kwa jeshi la Urusi, kwenye mipaka na pia ndani ya eneo la Kiukreni katika sehemu zinazokaliwa za Ukraine," anasema Orysia Lutsevych, mkuu wa Jukwaa la Ukrainia Chatham House huko London. Na njia moja ambayo inatazamia kufanya hivyo ni "kupitia muungano wa pamoja na Nato," anasema Lutsevych.
Lakini Urusi inaamini kwamba uwezo wa kupeleka wanajeshi kwenye mpaka wake ni haki ya uhuru. "Wako katika eneo la Urusi, hakuna anayeiambia Marekani mahali pa kuweka vikosi vyake katika eneo la Marekani," anasema Elena Ananieva, kutoka Taasisi ya Ulaya (RAS) yenye makao yake makuu mjini Moscow. "Kwa mataifa mengine inapaswa kuwa sawa"
"Kama nchi za Magharibi zinavyosema, kila nchi ina haki ya kuchagua jinsi ya kulinda usalama wake." "Lakini, tatizo kuu kwa mtazamo wa Russia ni tishio la Ukraine kujiunga na NATO na miundombinu ya kijeshi ya Nato kukaribia Urusi," anasema Ananieva.
Hii inatupeleka kwenye swali letu linalofuata.
Je, NATO itajipanua zaidi na kuijumuisha Ukraine kama mwanachama mpya?
Kando kupelekwa kwa wanajeshi katika mpaka wa nchi hizo mbili kumekuwa na kutoelewana kwa kidiplomasia kati ya Urusi na muungano wa kijeshi wa magharibi Nato.
"Upanuzi zaidi wa Nato kuelekea mashariki na kupelekwa kwa silaha, ambayo inaweza kutishia Shirikisho la Urusi, haikubaliki," kulingana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov.
Urusi inapinga vikali uwezekano wa upanuzi wa Nato na inataka hakikisho kwamba Ukraine haitajiunga na Nato. Ni msimamo unaoshirikiwa na mshirika wake wa karibu China. Lakini madai haya yamekataliwa na Nato na nchi wanachama wake. Kwa sasa kuna nchi wanachama 30 katika Nato, lakini nchi nyingine zinaweza kujiunga. Ukraine si sehemu ya muungano bali ni 'nchi mshirika'.
"Jamii ya Kiukreni na vyama vya kisiasa vinaamini kwamba hakuna njia bora ya kulinda Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi kuliko kuwa sehemu ya muungano wa pamoja wa usalama," Lutsevich anasema lakini pia anaongeza kuwa uanachama wa Ukraine kwa Nato unaweza usitokee katika siku za usoni.
Huko nyuma katika miaka ya 1990, baada ya kumalizika kwa Vita Baridi na kuanguka kwa Muungano wa Kisovieti, Nato ilitafuta njia za kujenga uhusiano wa karibu na mataifa mapya ya Ulaya ya Kati na Mashariki yaliyojitegemea.
Huu ndio wakati muungano huo ulipopanuka kuelekea mashariki zaidi, kumaanisha uwezo wake wa kijeshi na silaha umekaribia mpaka wa Urusi.
Kwa miongo kadhaa Kremlin imedai mara kwa mara kwamba nchi za Magharibi zilivunja ahadi ya kutopanua Nato. Madai hayo yanarejelea mazungumzo ya mwaka 1990, kati ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani James A. Baker na kiongozi wa zamani wa Usovieti Mikhail Gorbachev.
Lakini viongozi wa Magharibi hawakubaliani na kusema hakukuwa na mpango wowote rasmi kuhusu kutopanua Nato hadi Ulaya Mashariki zaidi na kwamba muungano huo unashikilia 'sera ya mlango wazi.'
Ikiwa Ukraine itakuwa mwanachama wa Nato (kwa sasa haijatuma maombi ya uanachama), "italeta tishio zaidi kwa Urusi" kulingana na Rais Vladimir Putin.
Mnamo Novemba 2021, alisema kuwa uwepo wa Ukraine katika muungano, na uwezekano wa kutumwa kwa makombora yoyote ya masafa marefu yenye uwezo wa kushambulia miji ya Urusi au mifumo ya ulinzi ya makombora, sawa na ile ya Poland na Romania, itakuwa suala la "mstari mwekundu" kwa Moscow.
Lakini Katibu Mkuu wa Nato Jens Stoltenberg aliweka wazi kuwa "Urusi haina kura ya turufu au kusema" kuhusu uwezekano wa upanuzi wa muungano huo.
Akizungumza na BBC, mtaalam wa Urusi Ananieva, alielezea wasiwasi juu ya uwezekano wa upanuzi wa Nato. "Miundombinu ya NATO inasonga karibu na mpaka wa Urusi. Nato inapaswa kuzingatia kanuni ya kutogawanyika kwa usalama," alisema.
"Hakuna uwezekano kwamba Ukraine itakuwa mwanachama wa muungano. Nato inapaswa kufikiria mara mbili kuhusu usalama wake ikiwa Ukraine itakuwa mwanachama wa muungano."
Wakati juhudi za kidiplomasia za kutatua mzozo huo zinaendelea, utafutaji wa njia mbadala wa zabuni ya Nato ya Ukraine umeibuka.
'Finlandisation' ni nini na ina uhusiano gani na Ukraine?
Miongoni mwa viongozi wengi wa kisiasa wanaojaribu kutafuta suluhu la mzozo huo ni Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa. Kulingana na ripoti za vyombo vya habari alitaja neno la enzi ya Vita Baridi "Finlandisation" kwa waandishi wa habari wakati wa safari ya Moscow.
Iliripotiwa kwamba alipendekeza "Finlandisation ya Ukraine", kama sera iwezekanavyo ili kupunguza mvutano katika kanda.
Lakini baadaye, tarehe 8 Februari, Macron alikanusha kutoa maoni hayo yenye utata.
Neno hilo hurejelea hadhi ya Ufini kama jimbo lisiloegemea upande wowote wakati wa Vita Baridi. Nchi hiyo ilikuwa na mpaka mrefu na Muungano wa Sovieti lakini haikuegemea upande wowote.
Msimamo huu ulimaanisha kuwa Helsinki hangekuwa mwanachama wa Nato na Umoja wa Kisovieti haungeona Ufini kama tishio linalowezekana na Ufini ilitia saini mkataba mnamo 1948 na Moscow ilikubali kukaa nje ya Nato.
Hata hivyo, mkataba huo ulimalizika mwishoni mwa Vita Baridi na serikali ya Finland sasa inasema maamuzi kuhusu kujiunga na mashirika ya kimataifa kama vile Nato yanapaswa kuwa mikononi mwake pekee na si kwa nchi nyingine.
Ukraine imesema kwamba pia haitakuwa tayari kuambatana na sera ya "Finlandisation" ambayo ingezuia sera zake za kidiplomasia.
"Nadhani ni jambo lisilokubalika kabisa kwa Ukraine" Lutsevych anasema.
"Ukraine ilishambuliwa ilipokuwa nchi isiyoegemea upande wowote, na pili Putin haheshimu mamlaka ya Ukraine, iwe haina upande wowote au la.
"Ukraini inakataa wazo hili kwa sababu ni sehemu ndogo ya uwezo wa Urusi kudhibiti Ukraine."
Je, kweli Urusi inaweza kuivamia Ukraine?
Kwanza kabisa, Urusi imesema mara kwa mara haina mpango wa kufanya hivyo, lakini kwa baadhi ya taarifa hizi hazijawatia moyo. "Tayari wamevamia," anasema Lutsevych akirejelea mwaka wa 2014 wakati Urusi ilipotwaa rasi ya Crimea ya kusini mwa Ukraine, na kuwaunga mkono waasi wanaoiunga mkono Urusi walioteka sehemu kubwa za mashariki mwa Ukraine.
"Kuna zaidi ya watu 14,000 waliofariki, zaidi ya 33,000 wakiwa wamejeruhiwa vibaya sana. Jumuiya ya Ukraine tayari inalipa gharama kubwa kwa uvamizi wa Urusi."
Nato haikuingilia moja kwa moja katika mojawapo ya matukio hayo, lakini jibu la muungano huo lilikuwa kupeleka wanajeshi wa ziada katika nchi za Ulaya Mashariki kwa mara ya kwanza, zikiwemo Estonia, Latvia, Lithuania, Poland na Romania.
Nato pia iliimarisha ulinzi wake wa anga/uwezo wa polisi katika mataifa ya Baltic na Ulaya Mashariki.
Moscow inataka vikosi hivi vya ziada kuondolewa katika nchi hizo.
Lakini kwa sasa, Nato inasema haina nia ya kufanya hivyo.
Nini kitatokea sasa?
Juhudi za kidiplomasia za kutatua mzozo huo zinaendelea ili kufikia makubaliano ya amani na kupunguza mvutano huo. Mnamo tarehe 9 Februari, katika mahojiano na BBC, Balozi wa Urusi katika Umoja wa Ulaya, Vladimir Chizhoz aliweka wazi mapendekezo ya Urusi ya kupunguza mvutano kuhusu Ukraine.
Alionyesha kuwa Moscow inaweza kujibu vyema ikiwa Ukraine ingekuwa nchi isiyoegemea upande wowote. Hata hivyo, Ukraine na Nato hapo awali walisema hawako tayari kukubaliana na hili. Katika hatua nyingine ya hivi majuzi, gazeti la Uhispania El Pais lilichapisha waraka uliovuja wa Marekani ukieleza msimamo wake wa mazungumzo.
Katika waraka huo, ilisema: "Marekani ilikuwa tayari kujadili... ahadi za kujiepusha na kupeleka mifumo ya makombora ya kurushwa ardhini na vikosi vya kudumu na misheni ya kivita katika eneo la Ukraine."
Wanadiplomasia na viongozi wa Ulaya pia wamekuwa wakichunguza njia za kufufua mpango wa kusitisha mapigano wa 2015 kwa mikoa ya Ukraine inayodhibitiwa na watu wanaotaka kujitenga. Mkataba unaoitwa Minsk kati ya Kyiv na Moscow haujawahi kutekelezwa kikamilifu.
Mtaalamu wa Ukraine Lutsevych anasema "Kyiv hatakuwa tayari kutekeleza mpango huo isipokuwa kutakuwa na upunguzaji wa kasi na usitishaji mapigano." "Urusi inataka kutumia makubaliano haya kuunda klabu yenye silaha ndani ya Ukraine ambayo ina raia wa Urusi," anaongeza.
"Suluhu la mgogoro huo ni umoja wa Magharibi na Ukraine. Kilicho hatarini ni uhuru wa Ukraine."
NATO inatishia majibu gani?
Mnamo Februari 7, kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alisema katika mkutano na Rais wa Marekani Joe Biden kwamba Ujerumani 'imeungana' na Marekani katika kuweka vikwazo dhidi ya Urusi ikiwa itaivamia Ukraine.
Vikwazo vinavyowezekana vilivyopangwa vya Washington vitamaanisha kulenga benki kuu za Urusi na kupiga marufuku Urusi kutoka kwa mfumo wa malipo wa kimataifa wa SWIFT ambao ni muhimu kwa miamala ya kimataifa. Uingereza ilisema itawawekea vikwazo watu binafsi na biashara karibu na Kremlin.
"Urusi ilistahimili vikwazo vya Magharibi" anasema mtaalamu wa Urusi Ananieva alipoulizwa kuhusu athari zake kwa Urusi. "Imegeukia uingizwaji wa bidhaa kutoka nje. Katika baadhi ya sekta za vikwazo vya uchumi wa Urusi vimeongeza uzalishaji, na kilimo. Wakulima wangependa vikwazo vya Urusi virefushwe," anasema.
Nato haijapendekeza kuwa ingetumia nguvu za kijeshi kukabiliana na uvamizi wa Urusi. Ingawa mazungumzo ya kimataifa yanaendelea kwa sasa hakuna njia wazi ya jinsi pande hizo mbili zitakavyofikia makubaliano.
Nani mwenye uwezo iwapo vita vitatokea?
===
Tangu mwaka Mpya wa 2022 uanze,vyombo vingi vya kiusalama vya kimataifa vimekuwa vikiripoti juu ya tishio la nchi ya Urusi Kuvamia kijeshi nchi ndogo jirani ya Ukraine,ambayo zamani ilikuwa katika muungano wa umoja wa kisoviet (USSR),Kabla ya kusambaratika vibaya Sana kwa umoja huo mwishoni mwa miaka ya 1990.
Chanzo cha mvutano wa kijeshi kati ya Urusi na Ukraine na uwezekano wa vita kamili
NINI CHANZO CHA MGOGORO HASA?
Mnamo mwaka 2014, Urusi iliyafadhili kijeshi makundi ya vuguvugu Mashariki mwa Ukraine katika majimbo ya CRIMEA,DONBASS,DONETSK na LUHANSK ambayo wakazi wengi wa majimbo hayo wana asili ya Urusi na wanazungumza Kirusi kwa ufasaha.
Katika mapambano hayo,Majeshi ya waasi kwa msaada wa Urusi walifanikiwa kuyateka majimbo hayo kutoka kwenye mikono ya Serikali ya Kyiv. Jimbo la CRIMEA liliamua kuitisha kura ya maoni (Referendum) ya kujitenga na Ukraine na kujiunga na Urusi.
Majimbo mawili (Donestk na LUHANSK) yaliendeleza mapambano makali dhidi ya Majeshi ya Ukraine na kuchukua udhibiti KAMILI wa majimbo hayo. Katika Jimbo la DONBASS Majeshi ya Ukraine yalipambana Sana na hivyo waasi kushindwa kuliteka Jimbo Hilo kikamilifu.
MGOGORO KAMILI?
Tangu mwaka 2014,Ukraine ilianza kupokea msaada wa vifaa vya kijeshi kutoka kwa washirika wa NATO. Ikumbukwe kuwa,Ukraine sio mwanachama wa NATO wala Umoja wa Mataifa. Vifaa vingi vya kijeshi vilitoka nchi za Marekani,Uturuki na Uingereza. Jeshi la Ukraine liliimarika zaidi baada ya kununua DRONES za kisasa kutoka Uturuki.
DRONES hizi zinajulikana Sana hasa zilipofanya vizuri kwenye mgogoro wa kijeshi Kati ya Armenia na Azerbaijan. Mwishoni mwa mwaka 2021 mwezi Desemba, Majeshi ya Ukraine yalianza kuyateka upya maeneo ya DONBASS kwa kutumia mashambulizi ya Anga kutoka kwenye DRONES. Majeshi ya Ardhini ya Ukraine yakashinda Nguvu Majeshi ya waasi na kuliteka Jimbo lote la DONBASS. Baada ya ushindi huo wa Majeshi ya Ukraine katika Jimbo la DONBASS,ndipo Ukraine ikaanza mashambulizi ya Anga kwenye Jimbo la LUHANSK.
Baada ya Ushindi huo wa Majeshi ya Ukraine,ndipo Majeshi ya Ukraine yakaingia Frontline ili kuwasaidia waasi. Pia,kikundi Cha Majeshi ya kukodiwa kutoka Urusi maarufu Kama WAGNERS kiliamua kuanzisha mashambulizi dhidi ya Majeshi ya Ukraine. Hata hivyo,Majeshi ya Urusi,Waasi na WAGNERS kwa pamoja yalishindwa kudhibiti mashambulizi ya DRONES za Ukraine.
Tarehe 24 Desemba 2021, Majeshi ya Urusi yalianza kuingiza mifumo ya Ulinzi wa Anga-ANT AIRCRAFT MISSILES (S-300 na S-400). Ujio wa Mifumo hiyo ya Ulinzi wa Anga ulisababisha DRONES za Ukraine kushindwa kufanya mashambulizi ya Anga. Hali hiyo ilitoa upenyo wa Majeshi ya Urusi na waasi kuchukua udhibiti upya wa majimbo ya DONBASS na LUHANSK.
JE, ENDAPO URUSI IKIAMUA KUVAMIA NANI ATAIBUKA KIDEDEA?
Kutokana na Uwezo mkubwa wa kijeshi wa Urusi ukilinganisha na Ukraine,bila Shaka Urusi itaibuka kidedea na kuyateka maeneo mengi ya Ukraine Kama itataka hivyo. Ushindi huo wa Urusi hautakuja kwa urahisi,Urusi inaweza kushuhudia kulipuliwa kwa vifaru vyake vingi ambavyo vitaingia kwenye ardhi ya Ukraine kuliko vifaru 140 ambavyo Urusi alivipoteza wakati wa Uvamizi wa nchi ya GEORGIA. Hii ni kutokana na Ukraine kupokea msaada wa Siraha za kulipua vifaru (ANT-TANK MISSILES) Zaidi ya Tani 80 kutoka Uingereza. Mwaka 2014 Ukraine haikuwa na Siraha hizi.
JE,URUSI INAWEZAJE KUZUIA KUPOTEZA VIFARU VYAKE VINGI?
Kutokana na Ukraine kutokuwa na Mifumo ya Ulinzi wa Anga (ANT-AIRCRAFT MISSILES) ya Uhakika, Basi Urusi ana nafasi ya kutumia ndege za kivita kushambulia Mifumo yote ya Ukraine ya kulipulia Vifaru Kabla ya vifaru hivyo kuanza kuingia kwenye Ardhi ya Ukraine kwa Urahisi zaidi.
Kutokana na Ukraine kulijua hili,imeamua kupeleka Mifumo yake ya kulipulia Vifaru karibu na mpaka wa Poland upande wa Magharibi. Makombora haya yanaweza kushambulia vifaru vyote vya Urusi ambavyo vitaingia Ukraine upande wa kaskazini wa Ukraine kutokea Belarus. Je,Urusi ataweza kushambulia kwa ndege za kivita Mifumo hii ya Ukraine ya kulipulia Vifaru ambavyo viko kwenye mpaka wa Poland? Jibu ni Hapana.
Kwasababu Marekani imeonya kwamba, endapo ndege za kivita za Urusi zitakaribia kwenye mipaka ya NATO(Poland ni Mwanachama wa NATO) Basi Marekani hatasita kuzitungua ndege Hizo. Ikumbukwe kuwa, Mwaka 2017, ndege ya Kivita Ya Urusi iliyokuwa inafanya mission ya kuwashambulia waasi wa ISLAMIC STATE ilitunguliwa na Mifumo ya Anga ya Uturuki ilipokaribia Anga la Uturuki kwenye Mpaka wa Uturuki na Syria. Hili tukio liliharibu uhusiano wa kidiplomasia Kati ya Uturuki na Urusi.
PIA SOMA
1. Mzozo wa Urusi na Ukraine wafukuta zaidi
2. Historia Iliyojificha Kuhusu Ukraine na Urusi
Taarifa zimekaa kiupande mmoja, vyombo vya habari havipo huru na hii inaonyesha kumbe kupitia dunia kweli ndio sio na sio ndio kweli. Ukrain wamevunja daraja ili vifaru vya urusi visiingie kwenye mji wa Kiev ila watachelewesha tu lakini lazima tuingie. Frontline commando wa Russian hata cm ya Putin hapokei kwa namna alivyo na midadi. Huyu mwamba alimisi sana vita yaani mda wote ana kiss russia flag ndogo aliyofunga kwenye mkono wake wa kuume.
Hata White House ya Bush ilitaka regime change ilipoivamia Iraq kwa sababu za uongo.
America really doesn’t have a leg to stand on.
Putin iko sahihi kwa 100% lazima aweke ulizi wa wananchi wa urusi dhidi ya Marikani/ Nato, kwanini Ukuraini anataka kujiunga na jeshi la Nato kinyume na mikataba ya awali na Urusi, lazma Russia ategeneze buffer zone, kuzuia military base ya NATO just at her courtyard, Ukuraini italipa gharama kubwa kwa kucheza siasa za kijinga, Marikani haiwezi kija kumsaidia hapo atapigwa paka asalimu amriwewe unashabikia UKRAINE ivamiwe, ? nchi iliyo huru na ivamiwe tu?
Madame Judge, Karani mwenzanguwewe unashabikia UKRAINE ivamiwe, ? nchi iliyo huru na ivamiwe tu?
Ukrain hata Tanzania tuna mmudu vizuri tu na hata kama atatupiga ila baadae sana na lazima kwanza atangaze hali ya hatari kwa raia wake. Ila cc tukiivamia Urusi,Putin hawezi tangaza hali ya hatari na kwanza ataomba kombe la dunia lipigwe kwake Kwani hali ya ulinzi na usalama umeimalika zaidi
Mkuu umeangalia taarifa ya BBC ya saa ngapi? Maana saa 1 asubuhi ya leo Rais wa Ukraine alikuwa analalamika kuwa Urusi imelenga kumkamata yeye na familia yake kwanza. Vilevile, wamesema (BBC) majeshi ya Urusi yameteka Uwanja wa Ndege uliopo km 20 kutoka Mji Mkuu wa Kiev na yanatarajia kuingia Kiev muda wowote kutoka sasa.Yaani ukifungua JF Vita inapiganwa na Ukraine kazidiwa hatari..Ila ukiangalia international news unaona Mambo tofauti from reporters ..naona hapa BBCwanajeshi wa Russia wamekufa na ndege zimetunguliwa za Russia...
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Huyo Mungu kwiyo🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣Take it from me, hakuna vita hapo!
Kwa watu wa dini wenye mioyo minyoofu, hiyo ni ishara kubwa sana kwamba sasa uovu wa wanadamu umefikia kikomo kama ilivyokuwa wakati wa Gharika na Sodoma na Gomora.
Mungu yule wa Gharika na Sodoma na Gomora ndiye yule yule ambaye tunaye sasa. Hajabadilika.
Amekuwa na subira kwa muda mrefu, sasa:"Enough is enough "