LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
hakuna anaeongea ukweli kila mtu anapiga propaganda, takwimu zinazotolewa na ukraine na urusi zote ni za uongo kila mtu kapoteza mara kadhaa zaidi ya hao sema huwez sema ukweli wakati watu wako vitani unashusha morali na kuingiza uoga
Sawa,

Ila ukiangalia mtiririko wa matukio utajua aliyeelemewa na vita na anayepoteza watu wengi zaidi
 
Tulieni tunakuja msiwe na haraka tuna vitu heavy sana hatujabeba magunzi

Screenshot_20220228-182608_WhatsApp.jpg
 
Russia ametumia uweledi mkubwa sana katika hichi wanachokiita operesheni ya kijeshi..ndo maana hata imechukua mda mrefu lengo ni kupunguza madhara makubwa kwa raia..mara nyingi majeshi ya Russia yamekutana na resistance ya wananchi lakini wamekua wakitumia busara sana wao wanaatack tu miundombinu ya jeshi na wanajeshi.
Ingekua ni wamarekani hii operesheni ingeisha ndani ya siku 3 sababu wao wanaua tu hawajali kama walivyofanya iraq
. Huyu raisi wa ukraine asalimu amri kuokoa mauaji ya raia kwan yeye ndo anamotivate raia wasio na millitary knowledge kuvaa combat na Russia akija anapiga tu akijua ni wanajeshi.
 
Huyu raisi wa ukraine asalimu amri kuokoa mauaji ya raia kwan yeye ndo anamotivate raia wasio na millitary knowledge kuvaa combat na Russia akija anapiga tu akijua ni wanajeshi.
Mkuu bora hata angekuwa anawapa hizo combat hao raia, jamaa anachotoa ni bunduki tu na gumboots utadhani wanaenda kwenye kazi za shambani, huku wakipigana na jeans/tracksuit wakijificha kwenye mavazi ya uraia. Wanatumika kama ngao.

images.jpeg
images (1).jpeg
 
Mkuu bora hata angekuwa anawapa hizo combat hao raia, jamaa anachotoa ni bunduki tu na gumboots utadhani wanaenda kwenye kazi za shambani, huku wakipigana na jeans/tracksuit wakijificha kwenye mavazi ya uraia. Wanatumika kama ngao.

View attachment 2136605View attachment 2136606
Combat hazina msaada hapo, mnapigania mjini maadui zenu wamevaa sare na wanajeshi wenu wamevaa sare zao mnazijua. Combat zinazuia risasi ama kitu gani zinaongeza
 
Na kwa akili yako unafikiri huo umoja wa nchi za Ulaya na Usa watakubari Russia aichukue Ukrain unapaswa kufikirisha akili yako vyema mzee wangu
Kwa kauli yako hii ni wazi wewe ndiye hufikirishi akili yako...Russia Hana Nia ya kuchukua Ukraine Bali anataka Yale majimbo mawili yawe huru na tayari ameyatambua....halafu anataka uongozi wa sasa wa Ukraine uondoke madarakani na uwepo uongozi wenye mwelekeo wa kulinda maslahi ya Russia
 
Kwa kawaida kwanza tukubali Russia wanajua nini wanafanya kuliko sisi, zile misafara ya gari zao jana kutembea umbali ule unafikiri hawakufanya assessment ya kwamba nini kinaweza kutokea? Mbona misafara imefika salama? tujue kwamba kuna wataalamu zaidi wa mambo ya kivita huko Russia kuliko sisi tunavyosoma taarifa mitandaoni.

Nadhani utakubali kwamba Russia haikutumia nguvu kubwa sana wakati wa uvamizi kwa Ukraine ilitumia nguvu kidogo na silaha ambazo sio nzito sana, ila baada ya mazungumzo kufeli na kuzagaa propanganda mitandaoni kwamba wanajeshi wao wanakufa sana hapo ndio wakawa serious, mara taarifa kwamba Russia imeshindwa kuingia Kyiv, sasa nini kimewezekana mbona wako Kyiv na jeshi la Ukraine halionekani lilipo.

Kwa mtazamo wangu ni kwamba Russia LABDA walitaka wafanye uvamizi mdogo ili kuwavuta Ukraine kwenye mazungumzo ila walipoona mazungumzo yamefeli na Rais wa Ukraine kasaini kujiunga EU hapo ndio kaamua kuwa serious.

wewe ni shahidi nini kimetokea, Ukraine leo hamna habari ya kuandikwa kuhusu jeshi la Ukraine kila unapoangalia wanaongelea heavy missiles without resistance yyte kutoka jeshi la Ukraine na Russia wameanza kutumia heavy missiles zenye high accuracy kitu ambacho mwanzo hawakufanya.

Kama ulifuatilia ule mgogoro wa juzi juzi wa Israel na Hamas, Israel toka inaanza ilikua inatumia silaha nzito zenye high accuracy toka mwanzo na walikua wanafanya vitu ambavyo Russia anafanya sasa kama kutoa taarifa kwamba atapiga sehemu flan mda flan hivyo wananchi waondoke.

Kwa kuangalia kama Russia wangetumia nguvu hii toka mwanzo wa Uvamizi unadhani Ukraine ingeweza kuwithstand vita mda wote huu?


Mda huo huo NATO wameshamaliza vikwazo vyao kuweka na wamesema hawapeleki jeshi Ukraine na hawaweki No fly zone kwa sababu italeta mtafaruku direct na Russia.

Hao wote wanajuana uwezo wa kivita acha sisi tunaosoma taarifa wanazoamua kurelease wao, leo hii unaskia Russia au US kila mmoja ana nuclear warhead 5000+ hizo ni taarifa wanazoamua kuachia hadharani ila deep inside si ajabu kila mtu ana zaidi ya 10,000+.

Leo hii utakuta watu wanasema Russia hakutegemea vikwazo vikubwa namna hiyo anafikiri washauri wa Putin hawawezi kufanya analysis za nini NATO zitafanya mara wakishaanza kuivamia Ukraine na watatokaje.

Kikubwa ninachounga mkono ni kwamba kila mtu ana mtazamo tofauti kuhusu hii vita na kila mtu ana upande anaotaka ushinde kwa sababu zake binafsi either mapenzi juu ya nchi/uhasama/chuki/ au vyovyote lakini hiyo isipelekee watu wabishane kwa matusi, hoja/mitazamo ndio mpango.
nadhani jamaa kakuelewa sanaa
maana anaiongelea RUSSIA kama anaiongelea CHAD
jamaa nayaheshimu sana mawazo yake na hua namkubali mnooo ila kwa hapa kajifanya MUCH KNOW sana mpaka katupiga CHAII
 
Eti wanaongea kwa lugha ya unyonge kabisa "Demanding Russia" demand maana kuiasa Russia. Siyo "Forcing Russia"

Hapo Putin anacheka tu huku akila bagia home. Yaani hapo ndio mwisho wa uwezo wao. Hakuna kitu kingine cha kufanya zaidi ya hapo.
Ushabiki kwenye level yake, hii ndio bongo land
 
Combat hazina msaada hapo, mnapigania mjini maadui zenu wamevaa sare na wanajeshi wenu wamevaa sare zao mnazijua. Combat zinazuia risasi ama kitu gani zinaongeza
Combat zinasaidia kutambulisha wanajeshi wa pande zote wanaopambana (waweze kuwindana wao kwa wao) na kuwatofautisha na raia ili kuwakinga raia wasidhurike.

Kitendo cha kupigana vita huku baadhi ya watu wakijifananisha na raia wa kawaida (kwa kuvaa nguo za raia) ili kupunguza uwezekano wa wao kushambuliwa (kuchukuliwa kama raia wa kawaida) na kuongeza uwezekano wa wao kushambulia kina hatarisha usalama wa raia wa kawaida ambaye hahusiki hata na mapigano. Raia wa kawaida waweza kudhaniwa nao ni ktk wapiganaji waliojificha kwenye mavazi ya raia na hivyo kushambuliwa/kuuawa.
 
Back
Top Bottom