LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

LIVE Special Thread: Yanayojiri Mgogoro wa Ukraine na Urusi. Nini chanzo na hatma ya mzozo?

Live coverage on JamiiForums
We jamaa unaongea nn aisee, Yani Us amvamie Russia anatafuta nini hasa? Kuna maslah yyte ? Ana rasilimali yyte ili akamuibie? Au amvamie ili awafurahshe nyie mashabiki mandazi ? Russia ashavunjwa vunjwa uwezo wake kitambo Sana Kwa njia ya akili Tu bila kutumia nguvu , Russia ni maskini the same to Iran and north Korea , ....!!! Hii vita wa kuwahurumia ni Raia wa Ukraine , lakini West na US wamenuia hii vita isiishe ili wamuadhibu vikali Russia economically ..na atachapika haswa , hawataki apate kisingizio cha kutanua uwanja wa vita , Ila corridor itakayotumika ni humo humo tu Ukraine , nje watawatangazia hawana mpango wa kupigana na Russia na mtashangilia mkifkri wameufyata Ila kimya kimya wanasuport humohumo Ukraine , vyombo vya habar vitaendelea kuripoti uharibifu unaofanywa na Russia Ukraine na mtashangilia kumbe watu Wana mission nyingine , Japan ndo anajua vizur akili za wazungu zikoje , baada ya mwaka mmoja maraia wa Urusi wataanza kuuza figo ili wajikimu kimaisha ....!!
Yaani atumie cost kubwa kupata kitu ambacho anaweza pata elsewhere kwa less cost.

Ujinga wa hivi anaweza kufanya ni Russia kama ambavyo anafanya huko Ukraine saizi na bado hajatoboa keshaingia kwenye mgogoro mkubwa wa Uchumi.

Russia saizi kazipita Iran na N.Korea kwa mbinyo wa vikwazo.👇

Screenshot_20220308-092453.png
 
Russia ana natural resources kama zote uyo ndo mzalishaji no2 wa oil duniani na gas no1. Vikwazo kwa Russia havijaanza leo wala jana lakini jeshi lake haliyumbi, kwanini Russia ni moja ya superpower countries??
Hata N.Korea jeshi haliyumbi, point ya vikwazo sio tuu kuwabana serikali bali kuumiza watu wa ndani Ili wabadili kiongozi.

Kwa.sasa Russia anaongoza kwa kuwekewa vikwazo ngoja tuone mwisho wake

Screenshot_20220308-092453.png
 
Mkuu utakuwa mwehu Sana ukilinganisha Russia na Ukraine , Russia kuivamia Ukraine ni kama wewe ukapigane na mtoto w darasa la Kwanza , haijalishi utampiga Kias gan Ila Kwa jinsi atakavyokubishia itashangaza wengi ... Hata hvyo hii vita Russia hashindi , mda ndo mwamuzi
Na Hali iko hivi huko kwenye battleground,toys wa Russia wanakata tamaa maana hawaelewi wako vitani kufanya nini huku wenzao wako fire 🔥🔥 kulinda Nchi yao kwa morale

Screenshot_20220308-092309.png


Screenshot_20220308-092413.png
 
Mrusi kaamua kuutokomeza ubabe wa Kimagharibi. Alichofanya Putin binafsi naona yupo sawa, kwani Magaharibi, hususan USA, wanajifanya wao ndio polisi na wababe wa dunia na wanachotaka wao lazima kiwe. Imefikia mahala, wanakuwa kama wapo Hollywood wanacheza filamu, wanawaonea mataifa madogo, lakini hata hayo mataifa mengine madogo yanawahenyesha sana lakini hawajifunzi wakatia adabu.

USA hawana ujanja wala ari ya kupigana wao wenyewe, wanawasukumizia wengine mizozo yao. Sasa hivi wamemuingiza mkenge Ukraine. Ghuba huko wamemuingiza Mkenge Saudi Arabia na nchi zingine za Kiarabu kuwa ndio "frontline" yao kwa Wa Iran na nchi zingine huko zenye watawala wasikubaliana nao.

Vietnam, waliwahenyesha, Taliban wamewahenyesha mpaka sasa hivi wanaugulia majeraha. Somalia ndio hawana hamu kabisa, wameifanya Kenya kuwa ndio frontline yao, ni heri Tanzania walistuka mapema.

Ukraine haitabaki salama mpaka isalimu amri, Na USA hataki hii vita iishe haraka kwaani ikiisha, front line yao waliokuwa wanaiunda ndio itakuwa imeshasambaratishwa na Warusi wanakuwa karibu zaidi na nchi za NATO, itazimeza moja moja, sio kwa kuzivamia bali kwa zenyewe kutii amri yao wataponyanyuliwa sauti.
Faiza sijui habari zako unapata wapi.
1. Ni Ukraine walioomba tangu miaka 20 kujiunga na NATO na hawakupokelewa hasi sasa. Je nchi ndogo haina madaraka kuchagua inapopendelea kujiunga (hata kama haapokelewi)?
2. Dhambi za Marekani ni dhahiri. Dhambi za Urusi hupendi kuona? Vita yake dhidi ya Waislamu kwenye Kaukazi (pamoja na Chechniya), kushambulia Afghanistan, zamani Chekoslovakia, Hungaria? Vitisho dhidi ya mataifa ya Ulaya?
3. Putin kusema eti Ukraine si nchi, haistahili kuwa nchi huru - ukimkubali je unaona Tanzania ni nchi? Kwa nini? Ukikubali uhuni wa Putin, basi hakuna nchi ambayo ni salama.
4. Hadi sasa naona hakuna aliyeshambulia Urusi tangu miaka 80, lakini Urusi imeshambulia nchi kadhaa. Sasa Ukraine.
 
"I will defend my homeland with my tongue, and with a pen, and with a sword, as long as I have enough life."

Putin congratulated Russian women on International Women's Day and quoted Catherine II.View attachment 2142875
Anatumia nguvu Sana kuhalalisha uvamizi Ili watu wake mamuelewe lakini wapi Hali halisi ya majeshi yake iko hivi 👇

Screenshot_20220308-092413.png
 
Si ndio maana juzi nikasema ukiniambia nipange list ya top ten militaries ukiachana na weapons of mass destruction sitaiweka Russia top four.

Tatizo la Russia ni uchumi ila watu wanafanya kama hawalioni. Tangu nijiite T-14 Armata ni 2017, mara ya kwanza nakiona ilikuwa ni Victory Day Parade mwaka 2015 walipokuwa wanatimiza miaka 70 baada ya ushindi wa WW2. Tangu hapo mpaka leo T-14 Armata haijawa incorporated kwenye vikosi. Bajeti hamna, kila kitu kinachelewa. Kama Ularvagonzavod hawana bajeti sasa makampuni mengine yatakuwaje. Kwa Marekani makampuni kibao yanaendesha project na hela zipo.

Armata universal platform nzima haijawa tiyari kwenye matumizi. Vifaru vyote vya Russia vinapigwa kasoro T-14 inayoogopwa sana ila haiko mass produced na haijapimwa zaidi wala kuwa tested vitani. Hata Ujerumani kwenye WW2 mwishoni ilikuwa na much feared King Tiger tank ila havikutengenezwa vingi na vilikuwa vizito mwishowe havikuleta impact. Ukija kwenye IFV za Russia akina BMP wote wanapigwa, Bumerang ambayo ni mpya nayo shida ni zilezile za Armata. Ukitazama IFV za Marekani zile Bradley zimetumika sana vita mbalimbali zinapiga kazi nzuri kuliko hata military planners walivyotaka.

Sasa ardhini ambako Russia ndio ana nguvu zaidi ndio anapigwa hivi, angani na majini itakuwaje. Nabaki nina imani kiasi na submarines zao ila ukitoa nuclear subs ambako inazidiwa na Marekani kwenye technology na quantity bado ukiniambie nichague diesel electric submarines nikachukua zile Kilo class na Lada class wakati kuna state the art subs zenye Air Independent Propulsion System (AIP) ziko Sweden na Germany.

Kwa Germany Siemens wababe wa teknolojia ya nishati walishirikiana na ThyssenKrupp wazoefu wa silaha za majini. Mitambo yetu ya umeme wa gesi pale Ubungo naona imeandikwa Siemens. Kwa Sweden wao ndio wa kwanza kutengeneza. Kwa Sweden kampuni yao ya Kockums ya kutengeneza meli na submarine ndio walikuwa earliest pioneer wa usable AIP duniani hadi US Navy ikawa inaomba subs zao ifanyie drills, wao hawatumii subs zisizo nuclear powered. Kockums inamilikiwa na Saab Group hapo Sweden na ndio hao hao watengenezaji wa ATM za NLAW zinazopiga vifaru vya Urusi kila siku na pia wanazo 4.5 generation fighter jet ile Saab JAS-39 Gripen inayosemekana inaweza kuwa bora zaidi ya Su-30 variants zote. Russia hana muunganiko mzuri wa teknolojia kwenye sekta mbalimbali, vigumu sana uwe na silaha nzuri wakati kampuni zako haziwezi kutengeneza vizuri magari ya kiraia, meli za mizigo, ndege za kiraia, etc.
Asante kwa hii informative comment 👏
 
Generali wa pili wa Urusi auawa Ukraine.Mfumo wa mawasiliona wa jeshi la urusi wafumuliwa na hackers,mawasiliano yote hadharani. Uhaba mkubwa wa chakula na mafuta unawakabili majeshi ya uvamizi. Morali ya jeshi imeshuka kwa kiwango kikubwa baada ya mashambulizi ya kitaalam ya jeshi la Ukaraine. Kremlin:Vladimir Putin azidi kuchanganikiwa,hasa ukizingatia ushahidi wa uhalifi wa kivita unazidi kuzunguka kwenye mitandao ya kijamii. Majenerali wa Vladimir Putin wanahoji busara ya Putin kutumbukiza Urusi vita vya 'kipuuzi' kabisa. Jumuiya ya kimataifa inazidisha kibano vikwazo vya uchumi.-Toyota ,Nissan wamesitisha uzalishaji magari Urusi.
 
Back
Top Bottom